Natofautiana na wenzangu kuhusu suala la Katiba Mpya

  1. Rev Masanilo,
  2. genekai
  3. ,Mian
  4. Ferds na
  5. Dr Ndege ya uchumi :
Kuna kazi kubwa sana ya kuelimisha jamii ya watanzania kujua nini maana ya katiba na msingi wake nini,
Ili watanzania wajue mapungufu ya katiba yanasababisha kero nyingi sana pamoja na kuwaacha wananchi wakihangaika wenyewe wanakosa pa kukimbilia na wanakosa mtetezi,na huyo mtetezi akijirundikia mishahara minono bila kuangalia wanaolala kwenye mbavu za mbwa tutakuwa tunawakashifu watu bila sababu wakatin tunajua hawajui NI MAANA YA KATIBA.
nfano ni SOKOMOKO ambaye hajui sababu ya kupanda kwa mishahara ya wakubwa wakati walio wengi wanaambulia vihela vya chai ya asubuhi tuu sh 150,000/= kwa mwezi.

ENYI WATU WENYE ELIMU YA DARASANI KILA MTU KWA WAKATI WAKE ATAMBUE WAJIBU WAKE WA KUMUELIMISHA MWENZAKE ELIMU YA URAIA NA KATIBA.
 
http://www.tanzania.go.tz/images/constitutioneng.pdf

Kwa manufaa ya SOKOMOKO soma hiyo katiba kwa umakini then uje na wazo hapa tutakupima kama umeelewa na watu wengine wasojua mapungufu ya Katiba yetu,hata wanasheria wa TANZAGANYIKA LAW OF SOCIETY (TLS) nao wamedai Katiba mpya nawapa senks bigup,ila wameniangusha sana kwenye ripoti yenyewe eti FAIR AND FREE not UNFAIR AND FREE LOL
 
Habari zenu wanaJF,

Napenda nitofautiane kidogo na wenzangu kuhusu hili suala la Katiba mpya. Kwangu mimi kipaumbele cha kwanza ni mishahara mikubwa na posho nono wanazopewa wabunge. Kama kweli wabunge wetu ni wazalendo wangeanza na hili na kuhakikisha kabla ya bunge la bajeti 2011/2012 limefanikiwa na kinachobakia kwenye mishahara ikaenda kuongezewa kwa waalimu na wauguzi. Maana watu watakuwa busy kwa miaka mitano kudai katiba mpya huku watoto wetu wakipewa elimu mbovu na huduma mbaya za afya kwakuwa wauguzi na waalimu maslahi yao yamemezwa na waheshimiwa wabunge!

Halafu mwaka 2011 baada ya kikao cha bajeti waanze mchakato wa katiba mpya sambamba na kubadilisha katiba zao za vyama maana hata huko kwenye vyama katiba hazikidhi matakwa ya wengi. Sipendi kutolea mifano ila ipo mingi sana kwenye baadhi ya vyama vyetu kuna uditekta, kujuana na undugu.

Nawakilisha....

Suala la Katiba ni mchakato wa muda mrefu, wala watu wasidhanie tukianza mchakato mwaka huu 2010/2011 labda 2015 tutakuwa na katiba mpya ambayo tutaingia nayo kwenye uchaguzi wa 2015. La hasha ! hilo halitawezekana 2015 katiba yawezekana itakuwa ni hii hii. Suala la katiba mpya sio suala la zima moto, ni bora muelewe.
 
Sasa kama unajua ni la Muda Mrefu kwa nini Lisianze Mapema, wewe kama unajua unasafiri unakwenda mbali utaondoka Mapema ili uwahi kufika au hutaenda kabisa kwa kisingizio eti ni safari ndefu?
 
Habari zenu wanaJF,

Napenda nitofautiane kidogo na wenzangu kuhusu hili suala la Katiba mpya. Kwangu mimi kipaumbele cha kwanza ni mishahara mikubwa na posho nono wanazopewa wabunge. Kama kweli wabunge wetu ni wazalendo wangeanza na hili na kuhakikisha kabla ya bunge la bajeti 2011/2012 limefanikiwa na kinachobakia kwenye mishahara ikaenda kuongezewa kwa waalimu na wauguzi. Maana watu watakuwa busy kwa miaka mitano kudai katiba mpya huku watoto wetu wakipewa elimu mbovu na huduma mbaya za afya kwakuwa wauguzi na waalimu maslahi yao yamemezwa na waheshimiwa wabunge!

Halafu mwaka 2011 baada ya kikao cha bajeti waanze mchakato wa katiba mpya sambamba na kubadilisha katiba zao za vyama maana hata huko kwenye vyama katiba hazikidhi matakwa ya wengi. Sipendi kutolea mifano ila ipo mingi sana kwenye baadhi ya vyama vyetu kuna uditekta, kujuana na undugu.

Nawakilisha....

Katiba iliyopo inaruhusu hiyo mishahara na posho nono.

Ukipewa swali la kukokotoa mduara wa duara lenye kipenyo cha xcm.

haukimbilii tu kuandika.

mduara = 22/7(xcm).

mwalimu anayejua hesabu atakupa 0%.

Lazima uweke formula

Mduara = pai*kipenyo.

then unaweka figures:

mduara = 22/7*xcm

hapo mwalimu atakuelewa.

hata ukikosa jibu, utaambulia maksi za formula.

formula ni katiba.

tukipunguza mishahara bila kurejea katiba na kuifanyia marekebisho, wenye mishahara yao watakuwa na haki ya kushitaki na katiba itawatetea.

sawa kijana?

next time utumie akili yako vizuri kabla ya kuweka bandiko.
 
sokomoko:swala la mishahara,dr wa ukweli alilizungumzia lakini kwasababu wabunge wenu wa chama cha majambazi wapo wengi walipotezea,kwa hiyo swala la kuanza na mishahara ya wabunge mm si ungi mkono hoja,waanze na katiba.
 
Katiba iliyopo inaruhusu hiyo mishahara na posho nono.

Ukipewa swali la kukokotoa mduara wa duara lenye kipenyo cha xcm.

haukimbilii tu kuandika.

mduara = 22/7(x).

mwalimu anayejua hesabu atakupa 0%.

Lazima uweke formula

Mduara = pai*kipenyo.

then unaweka figures:

mduara = 22/7*x

hapo mwalimu atakuelewa.

formula ni katiba.

tukipunguza mishahara bila kurejea katiba na kuifanyia marekebisho, wenye mishahara yao watakuwa na haki ya kushitaki na katiba itawatetea.

sawa kijana?

next time utumie akili yako vizuri kabla ya kuweka bandiko.

Mkuu Unafikri Sokomoko hajui hilo Jaambo? Basi tu anataka kujifanya Hamnazo tu
 
Ndio napata Sipendi kabisa kujihusha na Chama cha Kijani kwa Sababu Naogopa kuambikuzwa namna wanachama wao wanavyofikiri kwa maana kufikri ki CCM ni Maafa kwa Taifa
 
katiba iliyopo inaruhusu hiyo mishahara na posho nono.

Ukipewa swali la kukokotoa mduara wa duara lenye kipenyo cha xcm.

Haukimbilii tu kuandika.

Mduara = 22/7(xcm).

Mwalimu anayejua hesabu atakupa 0%.

Lazima uweke formula

mduara = pai*kipenyo.

Then unaweka figures:

Mduara = 22/7*xcm

hapo mwalimu atakuelewa.

Hata ukikosa jibu, utaambulia maksi za formula.

Formula ni katiba.

Tukipunguza mishahara bila kurejea katiba na kuifanyia marekebisho, wenye mishahara yao watakuwa na haki ya kushitaki na katiba itawatetea.

Sawa kijana?

Next time utumie akili yako vizuri kabla ya kuweka bandiko.
mkuu ukianza hesabu ndo utamchanganya kabisaaa!
 
  1. Rev Masanilo,
  2. genekai
  3. ,Mian
  4. Ferds na
  5. Dr Ndege ya uchumi :

Kuna kazi kubwa sana ya kuelimisha jamii ya watanzania kujua nini maana ya katiba na msingi wake nini,
Ili watanzania wajue mapungufu ya katiba yanasababisha kero nyingi sana pamoja na kuwaacha wananchi wakihangaika wenyewe wanakosa pa kukimbilia na wanakosa mtetezi,na huyo mtetezi akijirundikia mishahara minono bila kuangalia wanaolala kwenye mbavu za mbwa tutakuwa tunawakashifu watu bila sababu wakatin tunajua hawajui NI MAANA YA KATIBA.
nfano ni SOKOMOKO ambaye hajui sababu ya kupanda kwa mishahara ya wakubwa wakati walio wengi wanaambulia vihela vya chai ya asubuhi tuu sh 150,000/= kwa mwezi.

ENYI WATU WENYE ELIMU YA DARASANI KILA MTU KWA WAKATI WAKE ATAMBUE WAJIBU WAKE WA KUMUELIMISHA MWENZAKE ELIMU YA URAIA NA KATIBA.
Kweli Ndugu
Hasa Sokomoko angeelimika japo kidogo,! ingekuwa bomba sana. Maana bado ni mbimbimbu sana wa swala la Katiba mpya!
 
Kweli Ndugu
Hasa Sokomoko angeelimika japo kidogo,! ingekuwa bomba sana. Maana bado ni mbimbimbu sana wa swala la Katiba mpya!

Utabakia kukata viuno tu nchi ishauzwa hii mmekalia kudanganywa na kuchezeshwa ngoma
 
Kila kitu kinaanzia kwenye katiba mpya. Inakuaje mtu ni mjumbe wa baraza la wawakilishi, mbunge wa kuteuliwa, waziri na vyeo vyote analipwa mshahara kwa kazi gani?
 
Sokomoko,
Kama ulifuatilia mdahalo kati ya mbowe na Hamad rashid, Mbowe alisema kuwa swala la kupunguza mishahara ya wabunge hawatalishughulikia kwa sababu hawajashinda uchaguzi mkuu wa Rais. Wakati huohuo anawadanganya wananchi kuwa Chama chake kitaongoza harakati za kbadilisha katiba. Hivi tujiulize, Chama kinachokiri kushindwa kuendesha mchakato rahisi kama wa kupunguza mishahara ya wabunge kinaweza kuendesha mchakato wa kubadili katiba? Hii ni sawa na mtu anayeahidi kujenga ghorofa wakati anakiri kuwa hawezi kupaka rangi kibanda!
Hawa wapinzani wetu hawako serious. Ndio maana kuna jamaa mmoja alisema "wapinzani gazeti la sani"! na mwingine akasema "hawajajipanga" na mwingine akawaambie "(they) MUST reform and restructure".
 
Kila kitu kinaanzia kwenye katiba mpya. Inakuaje mtu ni mjumbe wa baraza la wawakilishi, munge wa kuteuliwa, waziri na vyeo vyote analipwa mshahara kwa kazi gani?

jyfranca,
Ina maana maisha Tanzania yanasimama mpaka katiba mpya ikija? tukubaliane kuwa maisha yanaendelea na kadri yanavyoendelea vile vinavyoweza kurekebishwa virekebishwe wakati mchakato wa katiba unaendelea. Katiba mpya hata tukikubaliana leo kuwa tunaitaka, mchakato wake hauwezi kupungua mwaka mmoja. Sasa kwa muda huo tusiboreshe mengine? Ndio maana Sokomoko akaja na wazo la kutoa kipaumbele kwenye mambo yenye immediate effect wakati tunaendelea na yale yenye long term effect.
 
Back
Top Bottom