Natofautiana na wenzangu kuhusu suala la Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natofautiana na wenzangu kuhusu suala la Katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Sokomoko, Nov 29, 2010.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wanaJF,

  Napenda nitofautiane kidogo na wenzangu kuhusu hili suala la Katiba mpya. Kwangu mimi kipaumbele cha kwanza ni mishahara mikubwa na posho nono wanazopewa wabunge. Kama kweli wabunge wetu ni wazalendo wangeanza na hili na kuhakikisha kabla ya bunge la bajeti 2011/2012 limefanikiwa na kinachobakia kwenye mishahara ikaenda kuongezewa kwa waalimu na wauguzi. Maana watu watakuwa busy kwa miaka mitano kudai katiba mpya huku watoto wetu wakipewa elimu mbovu na huduma mbaya za afya kwakuwa wauguzi na waalimu maslahi yao yamemezwa na waheshimiwa wabunge!

  Halafu mwaka 2011 baada ya kikao cha bajeti waanze mchakato wa katiba mpya sambamba na kubadilisha katiba zao za vyama maana hata huko kwenye vyama katiba hazikidhi matakwa ya wengi. Sipendi kutolea mifano ila ipo mingi sana kwenye baadhi ya vyama vyetu kuna uditekta, kujuana na undugu.

  Nawakilisha....
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kwenye red, hii ipo kwenye katiba za hivyo vyama?
  Akili yako huwa siielewi kabisa! kama vile unatope na sio ubongo!
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Watu wengine sijui huwa wanawaza kitu gani! Katiba kwako si muhimu zaidi punguzo la mishahara......!
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Once agin, Hila zako za Kishetani hazitafanikiwa, Tunakupotozea
   
 5. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sijasema kuwa Katiba sio Muhimu..... ila kwa mtazamo wangu suala la mishahara ya waheshimiwa linabidi lijadiliwe kwanza au ikiwezekana sambamba la kudai katiba sio kuwekwa kiporo. Nadhani umenifahamu.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu bila shaka umeamka na hang over! KATIBA mbele kama tai ndugu yangu.
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu unataka kusema hata Dr wa kweli ana hila za kishetani maana alipokuwa mjengoni alilisema sana hili jambo labda kumbukumbu zangu ziwe hazifanyi kazi vizuri.
   
 8. F

  Ferds JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mawazo mazuri ila washabiki wameyakataa, tungojee pongezi kutoka kwa wachambuzi wa mambo ndugu yangu
   
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sawa lakini next iwe suala la posho za waheshimiwa pamoja na mawaziri unless mnakubaliana na expenses kubwa kupindukia kwa kujilinganisha na nchi matajiri wakati sie ni nchi masikini.....
   
 10. m

  mian Member

  #10
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe lakini msingi wa mamboyote haya unatakiwa uanzie kwenye katiba...kwani katiba ikishakaa sawa na ikaweza kuwabana wanaojilimbikizia mali ikiwemo kijilipa mishahara mikubwa na kugawana vya watanzania basi tunakua tumemaliza...Katiba tuliyo nayo ni ya zamani sana...wakati wa chama kimoja na misingi yake iliangalia upande huo mmoja...sheria zetu ziko kwa kiingereza...tume ikishamtangaza mshindi wa Urais basi hata maakama hainanguvu ya kuhoji...kwa kifupi tume inapewa mamlaka ya kikatiba kututeulia Rais kwa kipindi cha miaka mitano..na tume hiyo inateuliwa na huyo huyo Rais..JAMANI...Hata hili linahitaji AKILI???Tuamke Watanzania, Tuifanye nchi yetu mahali bora kwa Wajukuu zetu.
   
 11. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unamaana gani kwenye hizo rangi nyekundu?
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Huu nao ni mtazamo tu!
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huwa unaniacha hoi sana na fikra zako! Hujui kubana matumizi si sera ya CCM! KATIBA ikiwa inamnyima raisi nafasi ya kutengeneza baraza kubwa la Mawaziri, na kuwa na wabunge wengi hasa wa VITU maalumu bila shaka gharama za uendeshaji zitapungua
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Unajua mtu Ukisoma vilaza unawapeleka unavyotaka, nimeandika hivyo ili ukiseme kile hasa ulichokuwa unataka kukisema na kweli umeingia Mkenge kama Kenge aliyetishiwa maisha nchi kavu anavyoyakimbilia maji. Sasa kama Lengo lako lilikuwa ni Kumtaja Dr. wa Ukweli kwa nini umezunguka hivyo? Ndio maana nikasema Hila zako za Kishetwani tumezishtukia
   
 15. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  hebu tumia akili japo kidogo,mabadiliko ya katiba ni kitu muhimu kuliko unavyofikiria especialy kwa tanzania ya leo,

  hivi umeipitia katiba japo vipengele kumi tu? kama ungekua umeipitia sidhani kama ungeandika hiyo post isiyo na kichwa wala miguu
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Siwezi kubishana na wewe mjadala upo wazi na hulazimishwi kuchangia ukiona thread yangu we kula kona!
   
 17. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0

  Katiba kwanza. Kwa nini?...katiba ita-ainisha kila kitu ikiwemo miongozo ya mishahara. Nani apate ngapi, kwa nini na lini. Itaweka vigezo vya kiutu kuhusu masuala ya kupandisha mishahara n.k Itaweka pia wazi kwa wote nani anapata nini na kwa nini. Kwa sasa kila kitu ni siri mbona nchi nyingine mishahra ya viongozi ipo mtandaoni bana?
   
 18. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  KWA NINI USIWE WAZI? KUNA KITU UNAFICHA FICHA, HUMU WANA JF WANASEMA WAZI. CDM WALIPUZINDUA KAMPENI WALIELEZA WAZI KUWA SUALA LAO LA KWANZA NI KUDAI KATIBA, BILA KATIBA KILA KITU HAKIENDI. MISHAHARA NA MARUPURUPU VYOTE VINATOKANA NA KATIBA MBOVU. KATIBA MAKINI ITAONDOA HAYO YOTE. ANGALIA VIDEO

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Lazima unichukie tu maana nimekuharibia Lengo lako, Eti katiba siyo Muhimu LoL!
   
 20. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Nakuunga mkono mwana wasu...........tuanze na mishahara then katiba kama tunataka mabadiliko ya kweli
   
Loading...