Natoa wito kwa waTz wenzangu juu ya wabunge wetu

ngwendu

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
1,964
174
Imekuwa ni wimbo kwa wabunge wetu kudai kulipwa hela nyingi kwani wakienda majimboni kwetu wananchi tunawaombe hela. na hata wananchi wakienda Dodoma wanaomba nauli za kurudia makwao. sasa waTz wenzangu, tudai haki yetu kila tuwaonapo wabunge wa wajimbo yetu wakipita popote pale. kwani wanadai hela nyingi ili waje watugawie. mimi nitakuwa wakwanza nikimuona mbunge wangu kwani haya wanasema hadharani bila hata kificho wala aibu. sasa tusione aibu wenyewe wameweka wazi.
 
Back
Top Bottom