Natoa siku saba (7) kwa ridhiwani kikwete la sivyo........

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
Natoa siku 7 kwa Ridhiwani Kikwete aende mahakamani kama alivyoahidi umma pale NEW AFRIKA HOTEL kama hatoombwa radhi na dr slaa na mtikila
Ridhiwani alisema hawa wazee ni makanjanja (dr slaa & Mtikila) kwa kumuita yeye ni bilionea hali yeye hana hizo mali anamiliki shamba la ekta 1.5 na account tatu ambazo hakusema zina kiasi gani ndani yake.
Ridhiwani aliujulisha umma kwamba hawa wazee wetu, wametoa tuhuma zisizo na ukweli na jamii isiwaamini kwa maneno yao.
Lakini pia kwa mikogo Ridhawani alisema kama wakimuomba radhi atawasamehe lakini kama hawata fanya hivyo hatawashitaki kwa kumchafulia jina. siku saba zake zimekwisha na sasa anajifanya mbogo kuhusu swala ili.

hivyo basi mimi kama mwanajamiii

natoa siku saba kwake aende mahakamani kama alivyosema, ama la na umma ujue Ridhiwani

1----anamiliki hizo mali zilizotajwa (dr slaa na mtikila )
2-----Serikali inamlinda kwa kutomchungaz na kumchukulia hatua
3-----Kikwete anajua uchafu (ubilionia wa kimjini mjini) wa Ridhiwani ndio maaana Ridhiwani sio
muoga
4-----Hiyo tuhuma za ubilionea ni za kweli na yeye hatakuwa amethibitisha ni kweli kwa kutokwenda mahakamani kama alivyo tishia

5---- taifa limchukulie kama tajiri wa mashaka na sio mtuhumiwa tena maana kama angekuwa amesingiziwa angekuwa mahakamani kama alivyosema, yeye ni mwanasheria ni hakika kama Dr slaa amemsingizi hatakwenda mahakamni ili kumpa usingizi yeye na familia yake, kwa misingi kwamba Dr slaa amekuwa mwiba kwao na hakuna jinsi wanaweza kuhacha nafasi hadimu kama hii, ikiwa imepatikana.
6----Pia kama jamii tutakoma kabisa kusikiliza malalamiko yake baada ya hizo siku saba. case closed na yeye hatabaki kuwa bilionea wa mashaka.

7----Polisi wanapashwa kumchunguza na kutujulisha umma maana huo ni ushahidi tosha kwamba ana ubilionea wa kukwapua mali za umma kwa kushindwa kwenda mahakamani.
8----CCM kama kweli wanapiga vita matajiri wasioeleweka wamvue gamba huyu mtoto wa raisi
9----Baada ya hizo siku saba yeye ridhiwani awaombe radhi dr slaa na mtikila kwa kuwaita makanjanja kwenye vyombo vy habari,
10----mwisho kabisa kama ridhiwani hatokwenda mahakamani wakuu tuasisi mpango wa zomea zomea kwa huyo bilionea na familia yake kila wanakoonekana.

siku saba nilizotoa kwa Ridhiwani afanye kama alivyosema, maana alitoa ufafanuzi mzuri tu, na ilimghalimu sana kukodi pale NEW AFRIKA HOTEL kwa hivyo alikuwa anajua anachosema na kama hatofanya hivyo ina maana alijaribu kudanganya umma.
kwa hivyo hayo mambo 10 hapo juu pia yatamuhusu na sisi wananchi tuanze utekelezaji wa hayo 10 kwa kuanzia vyuo vikuu mpaka mpaka mitaani,
na mengine wakuu mtakayoona ni muhimu sisi wananchi kuyafanya kwa watu kama hawa ni muhimu kutoa fundisho kwa watu wanaotupotosha kila siku.
ili litakuwa funzo hasa wanasiasa na familia zao kwenda kwenye vyombo vya habari na kukanusha kwa kiburi habari muhimu na tuhuma za ukweli zinazowahusu. na tutafanya hivyo kwa kila kiongozi hatakaye kanusha vitu vya ukweli kwa maslahi binafsi.
SASA RIDHIWANI JINYONGE MWENYEWE AU JIOKOE KWA KWENDA MAHAKAMANI.

Mkullo naye tunamsubilia pale Zitto atakapomwaga mambo bungeni, ikibainika ni kweli naye tumpe wakati mgumu kila kona hanakotokeza.
:bounce::bounce::bounce::bounce::bounce:
NI HAYO TU WAKUU:
 
Duh maneno mengiiii!!ye katoa sik 7 na wewe unampa siku 7 ..mwisho wa siku utafanya kama alivyofanya!! ungempa siku moja ningekuona mkweli..otherwise ni walewale tu....utekelezaji sufuri.
 
Isue ya siku saba alianza kuitoa Sokoine ambae alikuwa maarufu kama mzee wa siku saba!
 
mkuu soma vizuri hiyo article ina maazimio tayari ndani yake,
ina maana baada ya hizo siku saba zangu hayo maaziamio yana apply by defult
yakwamba yeye R1 ni bilionea wa kuchakachua mali za umma

Duh maneno mengiiii!!ye katoa sik 7 na wewe unampa siku 7 ..mwisho wa siku utafanya kama alivyofanya!! ungempa siku moja ningekuona mkweli..otherwise ni walewale tu....utekelezaji sufuri.
 
Inawezekana hakumaanisha kwamba baada tu ya siku 7 kuisha atakwenda mahakamani. Nadhani alimaanisha mchakato wa kuwapeleka mahakamani ungeanza baada ya siku 7 kumalizika ngoja tusubiri tuone.
 
Tutamjadiri mtu mpaka lini?. Mnatujazia upupu kwenye seva yetu bila sababu.
 
Mabilioni wa Watanzania mikononi mwa katoto ambaye hata hajafanya kazi ya kumletea mamilioni!!!!!Jamani tunaliwa waziwazi na tunakubali kuporwa mali yetu kiasi hiki!!!! Enough is enough na moto uliowashwa na unaoendelea kuwashwa na CDM usizimike, tuuendeleze hadi kieleweke
 
Umempa siku nyingi sana, 7!!!!!!!!!! ungempa masaa tu kwa sababu ungeanza kuhesabu siku zako baada ya zake alizowapa slaa na mtikila sijui zingebaki ngapi. Ok tunangoja hizo saba zako ziishe. nakupongeza kwa hilo.
 
lakini ameshasema hataki tena haya mambo kuvungumumziwa
na hataki maisha yake kwenye media, sasa nani alimuita kuzungumza na wahandishi wa habari?
Inawezekana hakumaanisha kwamba baada tu ya siku 7 kuisha atakwenda mahakamani. Nadhani alimaanisha mchakato wa kuwapeleka mahakamani ungeanza baada ya siku 7 kumalizika ngoja tusubiri tuone.
 
Huyu dogo alipata gpa ya ngapi pale mjengoni?.maana kwa mtu aliyekwenda shule hawezi kufanya hayo.kwanza nasikia alikuwa kilaza sana class
 
hiyo ni swali la msingi sana, hata mimi nina mashaka na weledi wake

Huyu dogo alipata gpa ya ngapi pale mjengoni?.maana kwa mtu aliyekwenda shule hawezi kufanya hayo.kwanza nasikia alikuwa kilaza sana class
 
Hapa tanzania mtoto wa rais nae ni rais sasa wewe nani unayempa siku saba rais wetu kipenzi riziwani wakati alitusaidia kumwingiza baba yake ikulu kwa gharama hizo hizo?.....mwacheni apumzike km baba yake kikwete anavyowashauri watz wawaache akina mkapa wapumzike..................hata hivyo ikulu uliishakuwa mradi wa kifamilia wa kikwete na intelijensia inajua sasa inabidi tuwe wavumilivu kidogo..............huwezi kumpa siku saba rais riziwani...kamwe!
 
Mimi nitatumia nguvu ya umma

hapa tanzania mtoto wa rais nae ni rais sasa wewe nani unayempa siku saba rais wetu kipenzi riziwani wakati alitusaidia kumwingiza baba yake ikulu kwa gharama hizo hizo?.....mwacheni apumzike km baba yake kikwete anavyowashauri watz wawaache akina mkapa wapumzike..................hata hivyo ikulu uliishakuwa mradi wa kifamilia wa kikwete na intelijensia inajua sasa inabidi tuwe wavumilivu kidogo..............huwezi kumpa siku saba rais riziwani...kamwe!
 
kama hatokwenda mahakamani
sisi kesi tumeimaliza na ukweli utakuwa umethibitika
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom