Natoa ombi kwa uongozi wa JamiiForums mumualike Naibu Waziri wa Afya aje afafunue na kujibu dukuduku na maswali ya watanzania

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Natoa hii rai sababu sasa tunakoelekea ni pabaya maana idadi ya maambukizi ya wagonjwa wa Covid -19 inazidi kuongezeka.

Mgonjwa wa kwanza kulipotiwa ilikuwa ni March 16 na leo ni April 19 kakini idadi inavyoendekea kuongezeka inatia hofu naashaka kwa sisi wananchi wa hali ya chini.

Napendekeza Dk Faustine Ndugulile mumualike na ahojiwe live sababu yeye ni mtaalamu wa masuala ya afya.

Kwanza kabisa kama mtaalamu aje atuambe ukweli kabisa juu ya namna ambavyo wanakabiliana na hili janga kama taifa.

Pili aje aweke wazi ni mask gani? ambazo zinaweza kujikinga na hili janga sababu maabukizi ya ndani yamepamba moto.

Pia aje atueleze kama watanzania kwa nini idadi ya wagonjwa wanao pona ni kama haiongezeki kwa kasi ila maabukizi yanazidi kupamba moto?

Pia aje afafanue je kuna haja ya kubadili mkakati wanaoutumia sasa hivi ili waweze kuokoa maisha ya watanzania kabla hawajaelemewa na wagonjwa.?

Pia aje atueleze kama total lockdown inawezekana kwa jijinkama Dar es salaam.

Natoa hii rai sababu kwenye kipindi kimoja ambacho alialikwa naona kama hakufafanua mambo kwa uwazi sana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom