Natoa mikopo ya dharura kuanzia Tshs laki 5

GREAT VISIONAIRE

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
365
453
Natoa mikopo kwa watu binafsi wenye shida za dharula.uwe na bond yenye gharama sawa ama zaidi ya mkopo utakao. Maximum ni milioni 3.muda wa kurejesha ni kati ya mwezi mmoja na miezi mitatu. Riba asilimia 15.
Pm ukihitaji huduma
 
je una vibali na leseni ya kukopesha watu..

kama huna kuwa makini sana watoto wa kihuni watakufundisha adabu..

utapewa dhamana magumashi na mwisho wa siku hela hawakulipi na dhamana yao wanaichukua na huwafanyi chochote..

ngoja watoto wa kitaa waje kukukopa ndio utajua biashara za kienyeji hazifai... fuata sheria bila shuruti
 
Mpwa siku hizi wale wadai kodi wamejaa kila sehemu kua makini utatumbuliwa kama hauna leseni.
 
Utapata hasara kubwa ambayo utajutia maisha yako yote, nilijaribu mke wangu alijaribu na kuna rafiki yangu kapoteza 40m . Mambo haya ni magum kwasababu ni biashara illegal vijana wakikuingiza mjin huna pa kuwapeleka utabakia mikwala tu na mwisho utakaa kimya. Mwisho wa siku we ndio utaonekana tapeli.

Duc in Altum
 
Katangaza biashara yake hajaomba ushauri nasaha! Jifunze kufahamu bandiko
 
Natoa mikopo kwa watu binafsi wenye shida za dharula.uwe na bond yenye gharama sawa ama zaidi ya mkopo utakao. Maximum ni milioni 3.muda wa kurejesha ni kati ya mwezi mmoja na miezi mitatu. Riba asilimia 15.
Pm ukihitaji huduma

Mkuu...bond ya gharama sawa na mkopo? Dah...kwahiyo kama nataka kuuza gari langu kwa 5 m (thamani ya gari), naweza kuja kwa kwa gia ya kuchukua mkopo alafu nika default ili uchukue gari?
Ushauri: Chukua kitu chenye thamani hata mara mbili ya huo mkopo...ili mtu akishindwa kulipa utaweza kuuza na ku recover pesa yako na interest yako pia..vinginevyo utajikuta unafanya biashara ya kununua vitu vya watu
 
GREAT VISIONAIRE
""FANYA HIVI, NASAIDIA WATU WENYE MATATIZO MBALIMBALI ENDAPO WATAKUWA NA VITU VYA KUWEKA REHANI KWA MAKUBALIANO KATI YA MIMI NA MWENYE TATIZO.""
*kuzungumzi mpaka masuala ya riba its another case!

Umemshauri vema.
Ndio maana nikamwambia afanye makubaliano ya mauziano (re-purchase agreement) unakua na wakili/mwanasheria wako kila kitu.

Hatopata tatzo lolote...not otherwise.
 
bond ya 500,000/- --->>pikipiki.
bond ya 1mil ---->>???
bond ya 2mil ----->>???
bond ya 3mil ----->>???
 
HIVI Hizi BIASHARA Zenu Mnaziendesha Kwa Kufuata SHERIA Na Taratibu Za NCHI?? Au Mnajikusanyia Mapesa Ya RIBA Tu, Pasipo KULIPA KODI Za NCHI!!?? HII Biashara Na Ile Ya WENYE Majumba Wanayopangisha Kwa KODI KUBWA, Tena Kwa Miezi 6-12!! NA Madalali WANAODAI KODI Ya Mwezi 1 Kutoka Kwa ANAYELIPIA Pango!! NI BIASHARA Ambazo SERIKALI Inapaswa Kuitazama Kwa Jicho KALI Mno!! KUNA Mapato Yanapotea!!!
 
Back
Top Bottom