Natoa Hoja dhidi ya Waziri Masha

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Nina miezi miwili tangu nirejee nyumbani Tanzania toka kwenye mawindo ya maisha huko magharibi mwa dunia.

Sasa tangu nimerejea hapa nyumbani nilijitahidi kwa kina kufuatilia mwenendo wa mambo mengi, ila jambo moja nimelikuta kama nilivyoliacha nalo ni nnchi kuwa na Waziri wa mambo ya ndani alie likizo ya muda mrefu.

Nawaza hilo kwasababu Lawrence Masha amechukua njia ya ukimya wa hali ya juu katika maswala ya usalama wa ndani ya nnchi yetu....Hivi karibuni kulitokea mauaji ya Kinyama kule kisiwani Ukerewe ambapo mamia ya raia wasio na hatia waliuawa kwa risasi za majambazi, na kibaya zaidi inadaiwa polisi wetu walihusika kwa namna moja ama nyingine.

katika harakati za kuelekea kufunga mwaka tumeshuhudia ajali z abarabarani zikipoteza maisha ya mamia ya watu nnchi nzima ....mtendaji huyu amekaa kimya...zaidi ya yote raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania amekua akitoa pole na hata mara moja moja akijitahidi kutolea maelezo juu ya matukio hayo, wakati huohuo Waziri mkuu amekua na kazi kubwa kuhamasisha usalama wa ndani ya nchi....

Sasa natoa hoja kuwa Masha L. waziri na Naibu wake wajiuzulu wenyewe kazi ili tuweze kupatiwa waziri mtendaji katika wizara hiyo nyeti maana LIKIZO yake haijulikani inaisha lini.
 
nimeambiwa na jirani hapa kua Masha amejikita kwenye Kampeni za Ubunge kule kanda ya ziwa maana anawasiwasi wa kupoteza jimbo
 
nimeambiwa na jirani hapa kua Masha amejikita kwenye Kampeni za Ubunge kule kanda ya ziwa maana anawasiwasi wa kupoteza jimbo

Hapa ndipo umuhimu wa kuwa na mawaziri wasiokuwa wabunge unapoijia. Yaani kazi yao iwe ni kutumikia nchi tu na si kuonesha constituent kuwa yupo karibu nao ili wasimtose.
 
Angalia sana asikujue jina, utaambiwa wewe jambazi sugu!!!! take care. Hawatakawia kusema umenaswa kwenye kamera za CCTV
 
Apewe kamanda JPM - John Pombe Magufuli,tuone kazi kweli Masha yuko long time likizo.lakini tusieme sana kwani ni swhiba wa mkulu pale juu,tusije anza tisha na cctv bure.
Lakini ukweli ndio huo arudi toka likizo au ajiuzulu hukohuko akiwa likizo pamoja na naibu wa Kagasheki sijui ambae anajiita balazi,sie atuitaji ubalozi wake baki utendaji makini kwa wananchi,jamani hivi wadanganyika tutaambiwa nini uchaguzi ujao,kwani kila lililo sema limeshindikana-maisha bora =o.kasi mpya =o, hali mpya =o.
Hebu JPM apewe wizara nyeti na sio za vitoweo????? afaynye kazi si tuliona alivyokuwa Ujenzi mambo aliyofanya-wonderful ingawa nabii asifiwi kwao.
natoa hoja??????
 
Sahau kuziuzulu.Tanzania hakuna hiyo.huyu Masha majuzi tu alikuwa Davos,na Rais na Gavana mwenye swimming pool!Ingekuwa Tanzania ina rule of law,Masha asingekuwa Waziri kwa conflict of interests ,na shughuli zake za uwakili
 
tatizo la ujambazi halitokani na utendaji wa waziri wa mambo ya ndani ingawa linaweza kuthibiotiwa kwa kiasi fulani na utendaji mzuri wa polisi. tatizo hili la ujambazi hapa kwetu linatokana na mfumo mzima wa maisha yetu kijamii na kiuchumi.
 
Wee kichuguu huna hoja, kama siyo tatizo la waziri wala polisi kumbe ni tatizo la nani? Kama matatizo kama hayo yanatokana na mfumo mzima wa maisha yetu kijamii na kiuchumi,kumbe Masha na Mwema wana kazi gani? Na kama wao hawana uwezo wa kukemea wala kushughulikia hayo matatizo ya kiuchumi na kijamii, kumbe ni kazi ya nani? Tuache ushabiki, Masha ile wizara imemshinda.
 
Huyu Mheshimiwa tangu sakata lake na Mengi amekuwa kimya mnoooo!! mpaka inakuwa kama Wizara haina Waziri. Sijui labda ndiyo ushauri aliopewa labda na wazazi wake au washauri wake na sasa pilikapilka za kampeni zinawadia ndiyo tusahau kabisa kumsikia mpaka labda baada ya uchaguzi kama atashinda na kupewa tena wizara ama hiyo hiyo au nyingine maana mkuu alishasema anataka kuwa na vijana wengi kwenye baraza lake la mawaziri na huyu ni mmoja ya hao ambao hawajala chumvi nyingi.
 
yaani na bahati mbaya hata Naib wake hayuko busy, yanapotokea majanga ya kitaifa kuhitaji ufafanuzi wa kina wa watendaji wakuu wa Wizara hiyo,....
mimi kwa upeo wangu wa mambo ..."by implication ...." masha amejiuzulu kutoka katika nafasi ya uwaziri wa mambo ya ndani, unless kukatolewa ufafanuzi wa kina.
 
Hii 2010 ni mawaziri wachache sana watakuwa kazini. Majimboni hakukaliki. Safari hii vitenge, khanga na pilau havitoshi. CCM ni kama vile imegawanyika ingawa sio rasmi. Ni juhudi binafsi tu zitawarudisha watu Bungeni. Mawaziri walio salama ni wale wa jimbo la Ikulu tu akina mama SS.
 
Huyo amechukua technic ya rais wake, kama kuna jambo burning na linakusumbua basi anakaa kimya media na wananchi wanapiga kelele tu mpaka wanachoka wananyamaza soo linaisha, sasa kila kiongozi anaiga tabia iyo, na as long the tactic works, wanaitumia, so wameona ukikaa kimya then no body talks about you then your safe! kwa sasa ndio mchezo tena!

Si ndio ilivyo kwa kina lowassa, karamagi, rostam, chenge, mkapa, sumaye etc hata kesi za kina mramba zitaisha ivyoivyo kwa sababu wako kimya na hawajibu hata wakishambuliwa vip na media!
who can blame them as long as it work!
 
Wabongo bwana..mya be jamaa anafanya kazi kimya kimya kwani lazima wewe ujue kila anachokifanya?unataka awe kama Maghufuli kila jambo na waandishi wa habari pembeni
 
Je ni waziri Masha pekee katika baraza zima la mawaziri ambaye 'yuko kimya kama vile yuko likizo'?. Kama ni hiyo ndo hoja, mbona mawaziri wengi watatakiwa kujiuzulu.
 
Wabongo bwana..mya be jamaa anafanya kazi kimya kimya kwani lazima wewe ujue kila anachokifanya?unataka awe kama Maghufuli kila jambo na waandishi wa habari pembeni
sasa umesahau kuwa Waziri ni mtumishi wa umma, kama anafanya kazi zetu ni lazima tujue nini anafanya, hebu fikiri juu ya sakata la majambazi kule ukerewe, kweli waziri anafanya kazi kimya kimya... labda anamtumikia mkewe na watoto wake. lakini kama anawajibika kwa niaba yetu ni lazima tujue.
 
Hii concept ya mtu ajiuzulu tu eti kwa sababu hasemi kitu au hasikiki kwenye media outlets etc, imepitwa na wakati sasa, I am sorry to say.

Could it possibly be that he is quiet because the mechanism is in place and churning away and doesn't require his input? Really, does he have to say anything and/or be seen to be deemed "effective"? If this is so, aren't we going back to the old populist politics of Tanzania of years past?

Mwacheni Masha afanye kazi yake na wizara yake. Waziri wake mdogo yupo, idara zake zinafanya kazi na ziko in the public eye etc
 
Hii concept ya mtu ajiuzulu tu eti kwa sababu hasemi kitu au hasikiki kwenye media outlets etc, imepitwa na wakati sasa, I am sorry to say.
KWAMBA UNAWEZAJE KUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI, ambaye hawezi kuisaidia nchi kuandokana na ujambazi na uhalifu.

Tangu lini waziri anajifungia ofisini eti anafanya kazi.....basi hiyo ni fashion ya aina yake, maana hata kukemea hawezi , aah huyu kimeo
.
 
nimeambiwa na jirani hapa kua Masha amejikita kwenye Kampeni za Ubunge kule kanda ya ziwa maana anawasiwasi wa kupoteza jimbo

Mpwa wala hilo sio swala la kuuliza kwani Masha anakazi kubwa kutetea jimbo lake na habari nilizo zipata kwa kusikia na masikio yangu na kuwepo pale mwanza mjini ni kuwa jamaaa hawamtaki wananchi wenyewe na sio ati kundi la watu wachache ni wengi wao hawa mtaki period nilishangazwa sana.

Niumejiuliza sana kwanini hawa watu hawamtaki wakati yeye ni mzawa wa pale kabisaa na anatatizo gani na kwao?

mnasumbuka bure tu.. kama Masha angekuwa wa kujiuzulu angejiuzulu zamani tu! Hivi mnataka tuanze kuhesabu.. kama hamuamini tafuteni hapa JF kwa kusearch jina la "Masha" labda mtajua tumetoka naye mbali. Kwa kadiri ya kwamba aliyemteua haoni tatizo ndivyo hivyo tena.
 
Back
Top Bottom