lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,147
- 33,302
Mgogoro Kati ya Ukraine upo kweli na Vita kubwa sana yaweza Kutokea baina ya Urusi na Ukraine wakisaidiwa na NATO.
Chokochoko hapo ni Marekani tu ndio ambae anampa kiburi na kumdanganya Ukraine.
Nia ovu ya Marekani Ni kuwa na wanachama wengi wa NATO walio karibu na Urusi na hasa wale walikua wasoviet walionitenga. Lengo kuu Ni kumzunguka Urusi.
NATO wanatishia kumuonya Urusi asijaribu kuingia/kuvamia Ukraine. Wanaonya kuwa Urusi akiingiza majeshi Ukraine atakiona.
Hapa wanatishia tu.hakuna watakachokifanya Kama Urusi akiamua kuingiza,na hajaamua. Zaidi watakachokifanya Ni kujaribu kumpa silaha Ukraine,na ambazo zinaweza kuishia mikononi mwa Urusi.
Kwa Nini nasema NATO wanatishia tuu,Ni kwa sababu Ukraine sio mwanachama wa NATO,na NATO akiingiza jeshi lake hata kwa kurusha risasi moja tu kuelekea Urusi basi hiyo itakua Vita kamili,amabapo Urusi itatoa jibu kamili kabisa kwa NATO,au kwa lugha nyingine Risasi hiyo itajibiwa kikamilifu na Urusi.
Sasa hapo kitakachochotokea Ni Vita kamaili. Na Vita Kati ya Urusi na NATO itakua sio viita ya Risasi na Bunduki,Wala ndege,Bali Vita vya Makombora. Wote tunajua Hawa mahasimu wawili yaani Urusi na NATO uwezo wao kwenye Makombora.
Je, Ni Nani Yuko tayari kwa upande wa NATO kukubali Makombora mapya na ya zamani ya Urusi yatue kwenye nchi zao kwa ajili ya Ukraine ambae hata sio mwanachama wa NATO?
Tena kwa mgogoro amabo hata yeye Ukraine Ana ukorofi wake?
Urusi hatishii, atavamia kweli na hakuna wa kumfanya kitu.
Katika mgogoro wa Ukraine na Urusi Ni Ukraine na Urusi kweli ndio Zina maslahi sio NATO,NATO lengo la Ni kujitanua tu.
Ukraine yeye anataka kujiunga na Magharibi kweli lakini ndani yake Kuna majimbo yanataka kuwa upande wa Msahariki (Urusi).
Haya majimbo yakijitenga Ukraine inabaki Nusu,hivyo haiko tayari kwa Hilo.
Urusi in Maslahi makubwa kuliko NATO na hata Ukraine,Urusi bado inaipenda Ukraine,lakini Ukraine haiipendi Urusi. Urusi inaogopa Ukraine ikijiunga na NATO kwa sababu NATO itakua kubwa Sana na itakua mlangoni pa Urusi.
Ukraine inawapiga waasi amabao Ni Warusi wa asili. Ukraine ikijiunga na NATO Crimea inaweza kuchukuliwa Tena na Ukraine kwa msaada wa NATO. Hizo Ni sababu chache tu za kwangu kuonesha jinsi Urusi ilivyo na maslahi makubwa na Ukraine.
Kwa maslahi hayo ndio maana nasema Urusi hatishii atavamia kweli na hajali matokeo yoyote Yale tofauti na nchi Kama Ufaransa Ujerumani Italy na wanachama wengine wa NATO labda kidogo Marekani atajitutumua kuonesha Yuko pamoja na Ukraine, lakini ki ukweli wale NATO hawana maslahi makubwa kwao zaidi ya kutanua huo umoja ambao Marekani ndio anafaidika zaidi.
Kwa Ni I Naamini Kuwa Urusi hatishii na atavamia kweli.
Urusi aliwahi kuivamia Georgia kwa ujinga Kama huu wa Georgia kuwapiga waasi wanaotaka kujitenga wa Southern Ossetia na Abkhazia. Urusi alikuja juu na kushusha kipigo kwa Georgia na NATO wakibaki kupiga kelele bila kufanya chochote ingawa walikua wakimpa kiburi Georgia.
Urusi ilikwenda mbali zaidi kwa kumpinga Georgia Hadi ndani na Urusi kuyapa Uhuru majimbo hayo mawili ya Southern Ossetia na Abkhazia kibabe tu. NATO walipiga kelele na UN walipiga kelele Urusi walitia pamba masikioni.
Baada ya mgogoro wa Ukraine kuanza kipindi kile kupelekea Rais aliekuwepo Ukraine wakati ule kupinduliwa na kukimbilia Urusi,baada ya Majimbo ya Luhansk na Donesk kutaka kujitenga Urusi iliingia Ukraine kiana na kujitwalia Jimbo la Crimea iliyokua sehemu ya Ukraine NATO na UN waliishia kupiga kelele huku wakiwa Kama watazamaji wa nyumba inayoungua bila msaada.Urusi hapa hakutishia alifanya kweli.
Mgogoro wa Waasi wa Syria waliokua wakiungwa mkono na Marekani Uingereza,Ufaranza,Uturuki,baadhi ya nchi za Ulaya, Sehemu kubwa ya Waarabu na Israel ili kumtoa Assad.
Urusi peke yake ilipinga Assad kuondolewa na kwa jeuri kabisa katikati ya hao wote ikapeleka majeshi yake na kupigana na yoyote aliekua anataka kumtoa Assad na hatimae leo Assad yupo madarakani zaidi ya miaka nane.
Urusi Tena ikapeleka vifaa vya kijeshi nchini Venezuela kumuunga mkono Raisi Nikolas Maduro ambae Marekani Uingereza na nchi nyingi za Amerika ya KUSINI kufanya kila hila kutaka Maduro aondoke madarakani kisiasa ama kijeshi.Urusi alipeleka vifaa vya kijeshi na wataalamu wa kijeshi nchini Venezuela kumlinda Maduro na Hadi leo yupo miaka kadhaa Sasa. Hii ya Venezuela sio maslahi muhimu Sana kwa Urusi ila kuweka heshima tu.
Kwa Urusi kule Ukraine Ana maslahi makubwa ya muhimu na ya kweli kabisa. Hivyo nchi yoyote duniani huwa inaingia vitani kupigania maslahi yake.
Urusi hapa iko tayari kupigana Vita kabisa na haijali matokeo ya Vita Bali maslahi kwanza. Lakini NATO hasa wa upande wa Ulaya Hawa hata Vita ikianza wao hawoni umuhimu wa Vita. Kwa hiyo NATO wanatishia tu lakini Urusi Hatishii Bali ataingia kweli Kama akiona ujinga unaendelea. Nimeonesha mifano hapo juu ya Georgia, Crimea, na Syria. Urusi hakutishia Bali aliingiza majeshi kweli na Hali halisi tumeiona. Kama mnadhani utani subirini mtaona Kama Urusi ataogopa kuivamia Uraine.