National housing corporation kufa katika kipindi cha miaka 20-30 ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

National housing corporation kufa katika kipindi cha miaka 20-30 ?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Maundumula, May 24, 2012.

 1. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Habari wandugu,

  Mimi si mjuzi wa mambo ya ujenzi lakini kuna swala nimekuwa nikitafakuri kichwani na kujiuliza maswali.

  Hili shirika letu la nyumba la Taifa linamiliki nyumba nyingi zilizojengwa miaka ya 60 na kwa elimu yangu ndogo nafahamu kwamba haya majengo yote yanakuwa na umri, na kinapofika kipindi inabidi yaagushwe chini kwa sababu za kiusalama. Mathalan jengo lililojengwa mwaka 1953 sasa hivi lina miaka 59 hii ndio kusema baada ya miaka 20 litakuwa na miaka 79.

  Je itapofika wakati wa kuyaangusha haya majengo si ndio itakuwa mwisho wa shirika lenyewe? au utapofika wakati wahusika watafumbia macho na kuendelea kulamba kodi? Ukizingatia kasi ya kujenga nyumba mpya za NHC ni ndogo je hili shirika lita survive hiki kipindi cha msukosuko?
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mbona mjini Dar wameanza kuyaangusha mengi sana wanaingia ubia na watu binafsi na wanaweka vitu vipya. Unaishi wapi wewe?
   
 3. Ben Mugashe

  Ben Mugashe Verified User

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 939
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Well pengine nilipitwa, kama wanafanya hivyo basi wameona mbali Hongera zao

  Mimi nilifikiri bado wanauza viwanja hapo city centre
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hapana, nyumba za NHC zilikuwa zinauzwa kabla Kikwete hajachukuwa madaraka, wajanja wachache waliuziana, Kikwete alipoingia kitu cha kwanza alizuia nyumba zote za serikali zisiuzwe.

  Unakumbuka wakati wa Mkapa walivyogaiana nyumba karibu ya bure? zingine zilikuwa za NHC.
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nina mashaka kama mafisadi hawajachukua viwanja vya shirika la nyuma
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka Ribosome,

  Nadhani na ile nyumba ya Mkapa pale Sea View karibia Bank M alinunua NHC , hope walimpa bei halisi kutokana na thamani ya nyumba na eneo. Heko Kikwete kwa kuokoa jahazi.
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Unampa heko ya kuokoa jahazi lipi wakati na yeye kachukua ile nyumba ya serikali pale migombani!! Aliahidi kuwa atazirudisha zile nyumba za serikali walizojiuzia bei poa mbona mpaka sasa kafyata mkia!! Huyu ni muuza sura tu kazi kuzurula dunia nzima sio mtendaji.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Usongo huo.
   
Loading...