National Health Insurance Fund (NHIF) - Kero za wananchi

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Wakuu mimi nimechoshwa na hawa jamaa wa mfuko wa bima ya afya NHIF kwani ni miezi saba sasa tangu waanze kunikata pesa kila mwezi lakini kadi mpaka leo ni kitendawili. Nashindwa kutibiwa kwani ukienda hospitali unaulizwa kadi, ukitoa barua ya mwajiri hospitali wanakataa kwamba hawaziamini.

Naomba kwa mdau/wadau ambao wako katika jamvi hili na wako karibu na uongozi wa NHIF wafikishe kilio hiki vinginevyo natarajia kujitoa katika mfuko huu.

Nawasilisha.
 
Mkuu mambo ya misaada yanaurasimu. Unajua NHIF unachangia sehemu na serikali inatop up, sasa kwa tanzania kitu chochote ambacho serikali inamkono kiko chini ya kiwango.
 
Mdau kama hauna kadi nenda pale NHIF makao makuu watakupa barua ya muda na utatibiwa wewe au kama ni mtt watakupa barua kwa ajiri ya mtt,mzaz au mke na atatibiwa..
 
Wakuu mimi nimechoshwa na hawa jamaa wa mfuko wa bima ya afya NHIF kwani ni miezi saba sasa tangu waanze kunikata pesa kila mwezi lakini kadi mpaka leo ni kitendawili. Nashindwa kutibiwa kwani ukienda hospitali unaulizwa kadi, ukitoa barua ya mwajiri hospitali wanakataa kwamba hawaziamini.

Naomba kwa mdau/wadau ambao wako katika jamvi hili na wako karibu na uongozi wa NHIF wafikishe kilio hiki vinginevyo natarajia kujitoa katika mfuko huu.

Nawasilisha.

Pole sana mkuu,

Binafsi naichukia sana NHIF kuliko ninavyoweza kueleza kwa sababu wanafanya mambo yao kienyeji sana. Wanakata pesa za watu bila utaratibu unaoleweka...Kuna jamaa yangu anayefanya kazi hapo NIHF alinambia kuwa ni lazima wanaopata zaidi wawalipie wenye kipato kidogo!!!????

Kuhusu kujitoa nadhani haiwezekani kwa sababu ni lazima (kwa mujibu wa sheria) kila mfanyakazi wa serikali au taasisi ya umma awe mwanachama wa NIHF!!!!
 
Ndio huo utaratibu kwa jina la kiingereza unaitwa CROSS SUBSIDIZATION. Yaani mwenye kipato kikubwa anamchangia mwenye kipato kidogo na mwenye afya, yaani asiyeugua mara kwa mara, anamchangia mwenye afya mbovu yaani yule ambaye anaugua na kwenda hospitali mara. kwa mara.
 
Wafanyakazi wa NHIF mbona hamtoi ufafanuzi ni kwa nini kadi zina chelewa??
 
Nipo kituo kimoja ja afya ambacho kinapokea NHIF, Lakini cha ajabu ni kwamba kuna kipimo kinacho gharim 5000 tu za kitanzania eti hakilipiwi ni NHIF, SASA SIONI UMUHIMU WA HUU MFUKO, kama unachagua baadhi ya vipimo na baadhi ya madawa.
naomba mnipe ukweli wana jf, au kuna kaujanja hapa.
 
Kuna staff wetu nae alienda kwa kituo cha afya akaambiwa NHIF hailipii kipimo cha Typhoid mbona nimechoka, sasa basi si waseme wanataka vipimo gani tufanye.
 
Nasikia huwa Inategemea na kadi uliyonayo, kuna kadi nyekundu ambazo baadhi ya vipimo na madawa huwezi kupata ila kwa wenye kadi ya kijani wanatibiwa na kupewa madawa yote, pia waweza kuhudumiwa kwenye hospitali kubwa. :A S-coffee:
 
Wakuu habari za mchana wanajamii.
Mimi ni mtumishi wa sekta ya afya na mshahara wetu basic salary ni 95700/=, na tunatumia brown card za NHIF na tunakatwa 2% kama sijakosea. Na green card nasikia unatakiwa kuwa na basic salary inayoanzia 1.2m.
Kuna ubishi hapa naomba msaada, je kwa basic salary inakatwa hii hii 2% au kila basic salary inapoongezeka na % nayo inaongezeka? Na je mwalimu anakatwa % ngapi coz naye nakumbuka kama anatuimia brown card.
Haya mambo naona nikaenda ya msingi coz kunamgonjwa alilazwa mwezi mmoja nikaambiwa anatakiwa kuruhusiwa hata kama hajapona coz taratibu za bima haziruhusu. Lakin pia kuna jamaa hapa yeye anasema yule wa green card anakatwa % yake na yule wa brown % yake. Je ipi ni sahihi.
Samahani kwa usumbufu utakaojitokeza
 
Makato ni asilimia 3 (3%) kwa mwajiriwa na asilimia 3 (3%) kwa mwajiri.
Lkn kwa maelezo yao hao watu wa NHIF wanasema wameondoa hayo matabaka ya kuwa na kadi za rangi tofauti.Walishawahi kuja kutubabaisha ofcn kwetu na sanaa zao.
 
Mkuu kwa ufahamu wng mdogo, 3% mwajiri+3% mwajiriwa.
Kwa kiwango chochote cha mshahara.
Brown card kwa mwenye mshahara wa chini ya 1.2M,

Green card kwa mstaafu+au mfanyakazi mwenye mshahara unaozidi 1.2M na kwa hospital zote hata zile executive.
Mkuu walifanya makosa sana kukuambia mgonjwa harusiwi kulazwa kutokana na sheria ya NHIF, kwa hospital wanatakiwa kutoa taarifa kwa maofisa wa bima na sio kumtoa mgonjwa kama hajapona. Huu ndo mchango wangu.
 
asante mkuu nimekupata, nitalifanyia kazi
 
Pengine uko na mgonjwa anatumia huduma ya bima ya afya nhif
ulipanga kumpeleka aghakan hospital hiyo imeamua kutsitisha matibabu na mfuko huo sababu
halisi ya kutolipwa na mfuko huo

mkurgenzi mkuu wa nhif alipoulizwa alijaribu kuficha ukweli kabla ya mmoja wa wafanyakazi kuweka
wazi tatizohalisi...mkuurgenzi huyo amesema wameweka watu kuwaelekeza waende hospital gani
wagonjwa watakaofika hapo aghakan hospital kwa ajili ya matibabu

humba alisema mchakato wa bei ndio kiini haswa cha aghakan kusitisha huduma..unajua wizara ya afya ilikuwa kwenye mchakato wa kutengeneza bei mpya..sasawakaomba mpaka decemmber ..ikawa bado wakaandika mpaka february so mpaka feb 1 awajapeleka ikawabidi aghakan hospital kuvunja mkataba

hata hivyo wadadisi waanasema hospital hiyo inadaiwa pesa nyingi sana na hospital ya aghakan na mbaya zaidi wamekuwa wakienda kudai na kusihia kupewa cheki hewa wakifika wanaambiwa bank pesa aipo
wamelalamika jinsi walivyokuwa mwanzoni na jinsi mkurugenzi huyu anavyotaka kuwalipa anavyotaka yeye huku wao wakiendelea kulipia umeme wafanyakazi....

Iwapo wewe mhusika wa nhif ni wakati muafaka kudai kwa nini awawalipi na kwanini wawachagulie hospital ya kwenda wakati mnalipa green pesa ndefu tuuu huku watu wakila kuku na kubadilsha magari kama mkurugenzi wa nhif....

Pengine hii iwe fundisho kwa mifuko hii inayoanzishwa kwa nia njema na kukutana na wachache wakiikodolea macho hapo hapo... Nimewiwa kuandika hapa maana habari zilizotufikia ni kwamba wagonjwa waliokuwa wakitibiwa na kadi za nhif wamepwa mwisho jioni hii ndugu wawe wamewahamisha kutoka kwenye hospital hiyo huku mkurgenzi wa nhif akipigiwa simu bila kupokea
 
Mifuko yote: LAPF, PSPF, NSSF, GEPF etc wanakula bata ilhali wanachama ziiiiiiiiii.
 
Back
Top Bottom