Wakuu mimi nimechoshwa na hawa jamaa wa mfuko wa bima ya afya NHIF kwani ni miezi saba sasa tangu waanze kunikata pesa kila mwezi lakini kadi mpaka leo ni kitendawili. Nashindwa kutibiwa kwani ukienda hospitali unaulizwa kadi, ukitoa barua ya mwajiri hospitali wanakataa kwamba hawaziamini.
Naomba kwa mdau/wadau ambao wako katika jamvi hili na wako karibu na uongozi wa NHIF wafikishe kilio hiki vinginevyo natarajia kujitoa katika mfuko huu.
Nawasilisha.
Naomba kwa mdau/wadau ambao wako katika jamvi hili na wako karibu na uongozi wa NHIF wafikishe kilio hiki vinginevyo natarajia kujitoa katika mfuko huu.
Nawasilisha.