National Health Insurance Fund (NHIF) - Kero za wananchi

Bima ya Afya kuna tatizo la kiufundi hasa linapokuja suala la malipo kwa baadhi ya hospitali. Agha Khani hosp (Dar) ilikuwa inatoa huduma nzuri lakini wamesitisha kutoa huduma kwa wagonjwa wanaotumia NHIF. Mikoani ndo wanaangaishwa sana. Ndugu yangu alinyimwa huduma bugando hosp.
 
yote ni shida tu, unaweza kuwa na kadi na ukasumbuka sana tu. mfano waweza andikiwa dawa ikakosekana hospital ukapewa fomu ukachukue dawa kwenye famasi, ukifika huko utaambiwa dawa hamna kumbe kwenye hilo duka dawa ipo ila wanaogopa kukupa kwasababu bei yake imepanda halafu NHIF hawarekebishi bei, unaweza ukazunguka maduka yote mjini na fomu yako unaambiwa hamna dawa, mwisho unaamua kuinunua kwa cash unaipata na utagundua kua bora ungelitambua hilo mapema na ukainunua kuliko muda uliopoteza na gharama ya usafiri uliyotumia. nacho washauri ndugu zangu ukienda na fomu yako ya bima kwenye famasi ukiambiwa dawa hamna wambie unataka kununua kwa cash utapewa, ukionesha fomu ya bima tu umekosea hutapata dawa.
 
Wasumbufu sana.Ingekuwa ni hiari nisingejiunga.Nilifuatilia huduma ya miwani bila mafanikio.Baada ya kuona usumbufu nikalazimika kulipa cash!Unaenda hospitali dawa hupati,unazunguka na mafomu kwenye maduka ya madawa hawataki kukupa dawa.Wizi mtupu!
 
Ingalikuwa Bima ya Afya ya Taifa NHIF ni ya Hiyari kujiunga, Nisingejiunga kamwe milele na milele.
 
Ni wezi wakubwa.
Mimi tangu januari mwaka jana sijapata,juzi wakanambia eti kuna data nilizokosea kujaza au nijaze upya tu maana fomu wameziweka mahali wasipopakumbuka.
 
HIi NHIF ifutwe tu haina tija kwa mtanzania, kwanza wana kadi za aina mbili. ya Kijani na ya pink km sikosei, hii ya kijani inathaminika sana ndo viongozi wengi wanatumia lkn hii ya pink ambayo ndo watu wengi wanayo maskini kwenye mahospitali mengi hawaitaki kabisa kuiona. sa NHIF mpo kwa ajili ya viongozi tu au? na hawa watu wa chini wanaotoa michango yao kila mwezi pesa zao zinakwenda wapikm hawapati huduma?

Kiongozi hiyo kadi ya njano si kwamba wanapewa viongozi tu bali ni kila mtu kutokana na kiwango anachokatwa. Yaani hii inategemea na mshahara wako. Sina kumbukumbu za hivi karibuni ila mwaka 2007 walikuwa wanawapa hiyo kadi wenye mshahara wa around 620,000/= kwa mwezi. Kutokana na mishahara kupanda najua nao watakuwa wamesogeza juu zaidi kwa sasa.
 
Hawa jamaa waliacha kutoa huduma kwa wale wanaotumia kadi za NHIF. Bado wanaendelea na huo mgomo au wamesharudisha huduma!!.
 
Hospital nyingi na maduka ya dawa hayatoi huduma kwa mtu mwenye kadi ya NHIF. Ni kwamba hawa jamaa hawalipi hizo huduma na wana madeni ya muda mrefu. Wana matatizo gani!!. Na kama ni hivyo kwanini tuendelee kukatwa hela zetu kila mwisho wa mwezi!!. Na walizotukata tangu hizo huduma zisitishwe tutarudishiwa!!!.
 
Hivi inawezsekana ni kweli hospital zote, maana hata regency na pharmacy ya mlimani-city hawakubali. kama ni hivyo kuna haja ya kukataa makato ya hela.
 
yani natamani nijitoe kwenye hili chama la NHIF. yani wanauzi unaenda hospitali unaambiwa hawatoi huduma kwa kadi za NHIF
 
Tarehe 19 mwezi huu NHIF wanatimiza miaka 10 tangu ianzishe na wanatarajia kufanya sherehe ya kukata na shoka ambapo waziri mkuu Pinda atakuwa mgeni rasmi. source MICHUZI: MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KUTIMIZA MIAKA 10

Hivi ni kweli hawa wanajua kwamba wateja wao tangu huu mwaka uanze hawapati huduma karibu hospital zote na pharmacy kwa kutumia hizo kadi zao!!!.

Hivi wanajua ni usumbufu gani wateja wao wanaupata wanapofunga safari ndefu kwenda kupata huduma halafu unaambiwa hupewi huduma kwa hiyo kadi!!!.

Hivi Wanajua kwamba watu imebidi wajilipie wenyewe gharama za matibabu wakati wanakatwa hela kila mwezi kwa ajili ya hiyo ya bima Afya!!!.

Hivi hawaoni aibu kuita waandishi wa habari na kutangaza kwamba eti wanampango wa kusherehekea miaka 10 badala ya kutumia huo muda kuweka sawa huduma zao.

Nalaaani sana hii kitu. na pengine muone aibu sana kufanya hiyo sherehe. Na tambueni zenu si nyingi!!!.
 
Cha kushangaza zaidi, madawa kibao na vipimo utaambiwa bima ya afya hailipii so inabidi ulipie mwenyewe, ila hushangai kusikia eti wamegharamia sijui semina elekezi za jk!!!!
 
Hivi kwa nini isiwe ni hiari kujiunga na huu mfuko wa bima ya afya? Fomu zangu za kujiunga zilitumwa mwaka jana septemba kadi nimezipata wiki iliyopita!!!! Nilitamani kuandika barua waache kunikata mshahara wangu coz sikuwa na kadi ya kuniwezesha kupata huduma. Kwa zaidi ya miezi 5 nililazimika kijilipia/kulipia huduma za matibabu kwa familia yangu! Sipati picha kama kutoa kadi inachkua miezi ya kuhesabu., sijui itakuwaje hapo ntakapoanza kuzunguka na likadi lao Arusha nzima nikitafuta hospt inayokubali kutoa huduma ya afya kwa hilo likadi!! Nakatwa pesa nyingi sana hadi sioni umuhimu wa hii bima ya afya zaidi kuona kama ni mpango wa kuchukua pesa yangu bila hiari! NHIF nina maswali mengi kuliko majibu!
 
Nadiriki kusema NHIF wanaadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ni wizi mtupu, sioni manufaa ya mfuko huo hata kidogo. Tangu nijiunge katika mfuko huo (kwa kulazimishwa na muajiri kwamba ni lazima kwa mujibu wa sheria) sioni faida yake hata kidogo zaidi ya maumivu kutokana na hela ninayokatwa kila mwezi zaidi ya elfu 60 ukijumlisha ya kwangu na muajiri.

Hivi karibuni nilipatwa na tatizo ikaonekana kipimo hicho kinapatikana Agakhan pekee lakini ninatakiwa kwenda na cash kujilipia, nikaona sio sahihi kwa kuwa ninakatwa hela ya kutosha kila mwezi. Nikaomba ushauri kwa baadhi ya wahusika wa hospitali hiyo, wakaniambia huwa kuna utarartibu ukiwasiliana na watu wa NHIF watakuandikia barua ya kwenda kutibiwa huko Agakhan bila kulipa afu wenyewe wanajua wanavyolipana. Nikafunga safari hadi NHIF makao makuu, nikajieleza shida yangu nikaambiwa inawezekana kupata huduma hiyo ila muhusika hayupo nimsubiri, alipofika muhusika nikamweleza huyo bwana alinipa majibu ya ajabu sana hadi nikaishiwa nguvu. Kwakuwa nilikuwa na shida nikaenda Agakhan nikajilipia.

Sasa nashindwa kuelewa:

1.Mfuko huu una manufaa gani kwangu kama ninapohitaji msaada kutoka huko sipati?
2.Ina maana NHIF ni kwa ajili ya kupewa dawa za malaria tu?ilishatokea nikaenda hospitali nataka kufanya check up nikatoa orodha ya vipimo ninavyohitaji,nikaambiwa vyote ni vya kulipia isipokuwa malaria.
3.Kadi yangu ni ya kijani( Green Card);wakati napewa niliahidiwa kupata huduma standard, je ndo haya manyanyaso kila ninapoenda kutibiwa??

Najua wahusika wa NHIF wanasoma JF hayo ni malalamiko yangu, hivyo mnavyo andaa sherehe za miaka 10 inaniuma sana najua moja ya source ya fund mnayotumia kuandalia sherehe hiyo ni makato ya mshahara wangu. Huduma zenu mbovu kupindukia ni heri mfuko wenu UFUTWE ili kila mtu ajue ustaarabu wa matibabu yake. Au kama wapo wanaonufaika basi iwe hiyari na siyo kulazimishana kwa kisingizio eti ni "KWA MUJIBU WA SHERIA".

Yapo mengi sana ila naomba niishie hapo najua wahusika mtaupata ujumbe.
 
Usiumizwe Kichwa na green card wala brown card,Mimi ninayo hiyo Green card ila sijaona inanisaidia nini..kila nikienda hospital au pharmacy ninazoziamini naambiwa wamesitisha huduma ya NHIF kisa hawalipwi...sijui hii pesa tunayolipwa inafanya kazi gani...Nawachukia sana,nikimuona mkurugenzi wao kwa media namuona kama the worst leader I have ever seen
 
huduma za NHIF zimesitishwa pale AGHAKHAN, ni pigo kwa wengi kwani Aghakan ni kati ya hospitali ambazo zinawaheshimu sana wagonjwa wa Bima ya Afya. ilikuwa unachagua Dr wa kumwona awe specialist au general na pia ilikuwa unapata vipimo bila mikwaruzo kama hospitali nyingine.

wengi tumeona hiyo tofauti baada ya kuanza kutibiwa TMJ

hiyo miaka 10 wanaadhimisha nini kama si wizi tu? hizo hela wangeenda kulipa huko mahospitalini
 
Wakuu mimi nimechoshwa na hawa jamaa wa mfuko wa bima ya afya NHIF kwani ni miezi saba sasa tangu waanze kunikata pesa kila mwezi lakini kadi mpaka leo ni kitendawili. Nashindwa kutibiwa kwani ukienda hospitali unaulizwa kadi, ukitoa barua ya mwajiri hospitali wanakataa kwamba hawaziamini.

Naomba kwa mdau/wadau ambao wako katika jamvi hili na wako karibu na uongozi wa NHIF wafikishe kilio hiki vinginevyo natarajia kujitoa katika mfuko huu.

Nawasilisha.

Acha kulalamika ovyo,nenda ofisini kwao chukua form ijaze warudishie watakupa kadi
 
Back
Top Bottom