National form II Results aibu!!

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
matokeo ya kidato cha pili 2009 yametoka ambapo 35% ya watahiniwa wote wamefeli,

Nini maoni yako,
 
Noo you got it wrong....nilimaanisha kama ni website our ubao gani wa matangazo tukaangalie..please
 
Noo you got it wrong....nilimaanisha kama ni website our ubao gani wa matangazo tukaangalie..please
Hapa ilitakiwa uniombe nikupe detail zaidi, sio kuniuliza source, hata hivyo kuanzia saa 2 usiku fuatilia vyombo vya habari vitatangaza kwa undani suala hili,

mimi nataka maoni kuhusiana na haya matokeo mabaya ya mtihani.
 
Nyie watu wa JF mnakimbilia source badala ya kujadili mada, Source ni waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi,

Mkuu Kaitaba watu wanaogopa kupoteza muda kwa kujadili hewa humu ndani. Source ni muhimu sana,
 
Mambo kaitaba, nashukuru kwa kuleta hja hii.
Tatizo la serikali yetu wadanganyika ni priorities, hivi leo ukiulizwa priority katika wizara ya elimu ni ipi utaweza kujibu, hebu tujiulize kidogo, mpango wa mem ulikuwa na lengo gani? shule za kata zililenga nini? walimu wa vodafasta waliletwa kwa nini? je wizara ya elimu inawza kutupa malengo yake kwa mwaka na mpango kazi wakufikia malengo hayo. tusimtafute mchawi waache wanasiasa waendelee kudharau wasomi et kwasababu wao walisoma hawakupata maendeleo mpaka wakaingia katika siasa.

kw kujibu hoja yako.
Unapozungumzia kufeli, lazima uzungumzie mazingira ya upatikanaji wa elimu, tukianzia walimu, vitabu, muda, majengo,nk. h
hivi hujui wanafunzi siku hizi huingia form 1 mwezi wa nane et second selection, huyu akifanya mtihani wa form two unategemea afaulu?
 
Ah, linchi letu hili tulishajikatia tamaa siku nyingi,tuna vuna tulichopanda sasa.Hizo shule za kata jamani zinatujeruhi kweli!
 
Matokeo ya mitihani ya form two nation wide yametoka. AIBU tupu. Mark ya ku pass ni 30. 33% ya wanafunzi laki 3 waliofanya mtihani wamefeli. That means they got below 30!!! Sasa wangeweka 50 ingekueje!!

Apparently they are the worst results in recent years. Somebody awajibishwe na kama vipi Waziri wa elimu ajiuzulu!!

Its a shame! Ngoja nitafute data zaidi.
 
Hii aibu tumeitaka wenyewe kwa kuanzisha hizi krash progam za walimu wa miezi miwili.
 
hapa hajiuzulu mtu. Akale wapi, utamaduni huo ni ulaya na marekani sio africa kulikoungua shoka ukabaki mpini
 
Nimekuelewa, baada ya kugundua kuwa sio hewa, sasa toa maoni yako,

Kama sina nitoe tu mradi nifurahishe genge/Kaitaba. Mi sijawahi kuona watu wanahamasishwa kutoa maoni humu ndani. Topic na unyeti wa thread ndiyo chachu ya kutoa maoni KAITABA. Yaani chema chajiuza. Kuna mbinu nyingi za kuhamasisha kutoa maoni bila ya kusema toa maoni.
1. Chakarika tafuta database weka hapa watu waipitie na kujionea wenyewe

2. Wewe muanzisha mada unatakiwa kuchagiza kwa kutoa maoni yako ambayo yatakaribisha response ya watu negative au positive. Siyo unaweka taarifa hapa halafu unataka maoni maoni gani sasa kama watu wamefeli!. Unaleta thread kama "KIPIMAJOTO" bana

Ushauri: Soma thread zilizochangiwa sana humu ndani mwanzo mpaka mwisho ujifunze jinsi ya ku-catalyse maoni mkuu.
 
Mi nadhani imefika mahali tukubali kuwa mfumo wetu wa elimu tumeuharibu kabisa na sasa hivi haufai kabisa.

Kuliberalise suala la elimu kumefanya kuwe na hizi shule za St Academy na st kayumba.,, ambapo inaonekana kuwa wenye kipato ndio wenye uwezo wa kupeleka watoto wao shule zenye unafuu ambazo ni za Private

Sikumbuki enzi za mwalimu kama kulikuwa na private ngapi ukiacha shule za seminari za kikriso na kiislamu,

tulipo hapa kila mtu anatafuta mtaji aanzishe shule kwa maana imekuwa biashara

Upande wa waaalimu wamekosa motivation na kusema kweli mweyekiti wao keshasema ndo matokea ya hizi shule za kata za chap chap na walimu wa voda fasta,, majengo tu hayawezi kufaulisha wanafunzi tunahitaji walimu, vifaa vya kufundishia pamoja na mishahara mizuri.

kwa hiyo nilimshangaa waziri aliposema kuwa hakuna mantiki ya kulinganisha shule za Umma na za binafsi...sawa lakini kweli serikali imekubali hali iwe hivyo? Tunatengeneza taifa la namna gani? watanzania wangapi wana uweza wa kulipia ada za milioni moja kwa mwaka na zaidi kwa mtoto mmoja?

Ninadhani tunahitaji hapa kujisahihisha..tumeshaharibu vya kutosha itafika mahali watu wanamaliza vyuo vikuu hawawezi kupata kazi..kwa sababu wana bora elimu na sio elimu bora.


Sasa sio lazima kila mtoto aende sekondari ndo maana kulikuwa na zile shule za ufundi baada ya darasa la saba. tusing'ng'ania kupeleka kila mtoto sekondari....

pili, waalimu waende shule kusomea ualimu....nchi za wenzetu mfanoi ujerumani mwalimu anasomea chuo kikuu miaka 6! akitoka hapo anaenda kufundisha watoto! sisi tunapeleke walimu 3 months tuko serious kweli!

Mi ningekuwa waziri ningejiuzulu, hata kama sera hajaitengeneza yeye..haitoshi tu kusema eti wamefeli 34%..hiyo ni kubwa mno kwa wanafunzi wa form 2!
 
Serikali ilisema mtu akifeli f.2 hatorudia ataendelea tu! sasa nani ajishughulishe!!
 
Back
Top Bottom