National bank of commerce (n.b.c ltd) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

National bank of commerce (n.b.c ltd)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Sep 22, 2009.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa mteja wa benki hii ya biashara ya kwanza tanzania baada ya azimio la arusha tangu mwaka 1998.
  Kazi inayoniweka hapa mjini ni biashara zangu za kati, na nimekuwa nikibank na nbc kwa kipindi chote tangu nimefungua akaunti mwaka huo wa 1998.
  Matatatizo ya hii benki yangu ni mengi sana, na hayana idadi.
  Juzijuzi niomeomba mkopo na umekuwa approved.
  Watengeneza dokyumenti wamenitengenezea kwa haraka sana na nikasaini mapema mno.
  Nimefurahishwa sana kwa kitendo hicho cha kupata documents kwa wakati muafaka.
  Sasa hatua inayofuata hapo ni kwamba dokumenti hizo zinarudi makao makuu kwa ajili ya kusainiwa na wakuu wa benki.
  Tangu mwanzoni mwa mwezi huu documents zilipoenda kusainiwa hazijarudi,
  kila nikiulizia naambiwa kuwa ziko kwa company secretary,
  siku zinaenda na msimu wa biashara yangu u mbioni kumalizika.
  Hakika huyu company secretary wa nbc ni kikwazo kwetu sisi wafanyabiashara wa sme.
  Tatizo lingine la benki hii liko upande wa atm.
  Nilipoteza atm kadi yangu tangu mwezi wa nane, nilipeleka police report na nikalipia tozo kwa ajili ya kadi mpya.
  Kibaya ni kwamba kadi hazitoki wanadaieti system inasumbua.
  Sasa ni zaidi ya mwezi nahangaikia kadi.
  Jana na juzi kulikuwa na sikukuu ya idd.
  Nikaenda na check book yangu mlimani city tawi ambalo limeandikwa mlangoni kuwa liko wazi siku zote za jumamosi, jumapili na siku za mapumziko yanayotambuliwa na serikali.
  Huko mlimani city nikakuta tawi limefungwa,
  nikaenda kwenye tawi jingine la nbc lenye kutoa huduma kama hizo lililopo sea cliff.
  Huko nako nikakuta hali si hali, na kwenyewe benki imefungwa.
  Hakika usumbufu nlioupata hauelezeki.
  Sasa nauliza, hii benki yetu tuliyowapa makaburu kwa bei ya dezo wanaipeleka wapi benki yetu??
  Je nini dira yake kipindi hiki cha taharuki ya uchumi na ushindani mkubwa wa kibiashara??
  Kama kuna nlichodanganya kwenye hili naomba nikosolewe ndugu waungwana
   
 2. K

  Kimambo Member

  #2
  Sep 22, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  pole sana ndugu yangu tataizo hilo wanalo sana ATM card unaweza kuipta hata baada ya miezi mitatu, foleni ndio usiseme nafikiri na nadhani kwa kuwa tuko kwa soko huru changua benki nyingine ambazo hakuna foleni na huduma ni chap cahap toka lini ukakuta foleni ya ATM EXIM bank au Diamond Trust bank,

  Uchaguzi u mikononi mwako na tukiondoka kama mia hivi nadahni kuna impact kubwa
   
Loading...