Natembea na mtoto wa rafiki yangu pia nimezaa na mke wa mtu

Status
Not open for further replies.

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
8,382
7,909
Hii ni stori ya kweli yaaani ni mimi mwenyewe, ni hadithi ndefu ila kwa kifupi ni kwamba natembea na binti wa rafiki yangu ila wazazi wake hawajui sasa yapata miaka 3 hivi, nilimsomesha hadi cheti kwenye chuo fulani, hivi navyoandika huu uzi nipo nae wazazi wake wakijua kuwa yuko kazini, ila nimempeleka akaishi kwa rafiki yangu mwingine, ndiko anakokaa.

Halikadhalika nina mpenzi mwingine yeye ni mke wa mtu natembea nae yapata miaka 4 nafanya kwa siri sana sasa akabeba mimba, nikawa naendelea kula tu mpaka akajifungua, watoto mapacha, walipofikisha umri wa miezi 8 sakaja nao hotelini maana tunaishi miji tofauti akaniambia wanao hawa, duh acha nistuke ila dalili ni wazi watoto ni wangu, hapa sasa nimemiksi,

Je, wazazi wa yule binti wakijua kuwa mie rafiki yao natembea na mtoto wao sijui itakuwaje na yule jamaa akijua kuwa watoto si wake itakuwaje na mke wangu wa ndoa akijua hayo sijui itakuwaje.

Je, nifanyeje nijinasue kwenye kizaazaa hiki, naomba mawazo
 
Hauna cha kufanya mzee,umeshaharibu maisha ya watu,sijui ukisema ni kazi ya shetani kama watakuelewa,mi nafikiri tamaa zimekuzidi.tubu haraka.
 
Binti mrudishe kwao, na vunja mahusiano na mke wa jamaa maana unahatarisha maisha yako. Nasiku akijua hizo habari na wew unaendelea na wapenziwako hao, ndoa yako itaingia katika mgogoro mkubwa kama si kuvunjika.
 
Hakuna ushauri endelea mzeee yatayokukuta utatua hapo hapo shida ya nini wewe si kidume cha mbegu
 
Hongera kwa kuwa kijogoo!
Dawa umpe mimba mtoto wa rafiki yako pia, halafu na mkeo. Then uulizie kama guiness book wanaweza kukuingiza. Hapo utakuwa maarufu na ku-gain through ur mess (ukimpata na huyo mke wa rafiki yako aka mkwe wa kambo, itakuwa bomba zaidi), the more the merrier, so they say!
 
Binti mrudishe kwao, na
vunja mahusiano na mke wa jamaa maana unahatarisha maisha yako. Nasiku
akijua hizo habari na wew unaendelea na wapenziwako hao, ndoa yako
itaingia katika mgogoro mkubwa kama si kuvunjika.

Na mkewe pia amrudishe kwao maana mwanaume asiyejiheshimu namna hii hastahili kuitwa mume!
 
Kwa ufupi wewe ni mpuuzi kwelikweli yaani hata kama umeishaamua kuwa mzinzi umekosa wengine mpaka uparamie mtoto wa rafiki yako na mke wa mtu? Kwa kweli wewe nu mtu mzima hovyooooooooooooooo
 
Huyo binti wa rafiki yako muache haraka saana, sababu unampotezea maisha. Tabia ya kutembea na binti mdogo hali umeoa inamuharibia mwelekeo wake wote wa maisha ukifananisha kutembea na dada mtu mzima. Jitahidi muwekee msingi unaoeleweka (kama vile kumtafutia kazi) then umuache; hilo nakusihi sana ni kheri hata angekuwa ni binti ambae wazazi sio marafiki zako. Pia tumia ustaarabu wa kujiweka mbali na wazazi wake, futa mazoea ya kale na ua huo urafiki unavo fanya sio ustaarabu kabisa kaka.

Huyu mke wa mtu asikuumize kichwa, anajua nini anafanya; tena hata inawezekana hao watoto sio wako ni wa mumewe hivo anything is possible. Kikubwa kama kweli unaamini ni watoto wako fanyeni DNA test maana damu nzito ili utambue kabisa. Ila tu kama umejenga mazingira kwa huyo mwanamke una niya ya kumuoa na kuwa nae (maana sometimes wanawake huwa tunakuwa wajinga - kaona umeoa bado anaweza dhani utamuacha mke na umuoe yeye) then itakuwa tatizo. Kwa sasa huyo mke wa mtu ni kimeo, usipoangalia utavunja ndoa yako na hata mabaya yanaweza kukukuta zaidi mme wake akijua... na kama unaniya kweli ya kuwa nae jiulize; kama alikuwa akilala na wewe na ana mume ukiwa nae wewe kipi kitamzuia kulala na wengine? Tulia kwa mkeo kaka.

Ushauri kwako mwenyewe, inawezekana mkeo hakutoshelezi... lakini fanya hayo mambo kwa akili sio kwa njia ya kuchimba kaburi kama unavofanya sasa. Kwa kiasi kikubwa hilo umefanya na huyo mtoto wa rafiki yako ni ushenzi na kwa kweli jitahidi usije fanya tena hivo.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom