Natazamia kusikia mazungumzo kati ya KAFULILA na viongozi wa CCM..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natazamia kusikia mazungumzo kati ya KAFULILA na viongozi wa CCM.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Dec 18, 2011.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote binafsi nitoe sikitiko langu kwa baadhi ya vijana ambao wameanza kuonesha kujikweza kwa nafasi walizo nazo na katika kuelekea kule ambako wao huita ni kupata "umaarufu." Lakini niwapongeze sana wana NCCR Magezi ambao wao wameamua kuchukua uamuzi mgumu na kuonesha kuwa Ruzuku kwao si zaidi ya nguvu ya Chama na ni wito wangu kwa vyama vingine manake kuna kina Kafulila wengi ndani ya vyama vya siasa hapa Nchini vyama vingine navyo vichukue maamzui kama ya NCCR ili watu waweze kutambua, kuthamini na kuheshimu uwezo wa chama. Haiwezekani Kafulila huyu huyu afukuzwe CHADEMA na leo tena yamkute hayo hayo NCCR lazma ana tatizo.

  Baada ya utangulizi huo niseme tu pamoja na tarabu zingine ambazo zitafuatwa na pande zote mbili ili kuapta haki ya kila mmoja na vile vile kutokana na taratibu za rufaa kuweza kuchukua muda mrefu ni wakat wa Kafulila kama ataamua kuendelea katika medani za siasa basi aanze mazungumzo na Chama Tawala (CCM). Sababu ya msingi ikiwa kwamba si rahisi kwa CHADEMA na hata KAFULILA mwenyewe kurudia matapishi yao na hata kama Kafulila akiamua kurudi Chadema si rahisi vile vile wahusika kumpokea kwani yeye kwao ni SISIMIZI. Lakini pili naamini vile vile alikotoka Kafulila (Jimboni) itawachukua muda mpaka kuelewa maana ya Mbunge wao kufukuzwa uanachama hivyo naamini kuwa wananchi bado wana imani na yeye hivyo kuwa tayari kwenda naye kokote atakako kwenda.

  Lakini jingine ni kuwa atokako Kafulila ni vyama vitatu ndivyo vyenye nguvu huko vikiwemo CCM, CHADEMA, na NCCR sasa vyama hivi viwili si vyake tena hivyo kilichobakia ni hicho kimoja ambacho kama atapata mshauri mzuri na akaamua kufanya uamuzi wa busara basi ataendelea kushikilia kiti chake. CCM hawatampokea Kafulila kutokana na ushawishi wake au nguvu aliyo nayo bali watampokea kwa sababu wana uzoefu wa kutosha wa watu wenye tuhuma kama za Kafulila i.e Wanafiki, Waasi. hivyo naamini wao wataweza kukaa naye na kumnyoosha vizuri ili awe katika kundi kama wengine.

  Ni wito wangu kwa vijana ambao wapata kupata dhamana sehemu mbali mbali wajaribu kuishi kwa mikakati, subiri na uvumilivu waingereza wana mithali yao "patient mind conquers all" ni nadhani hili neno "umaarufu" lisituvae kwa namna tunayo idhani sisi subira na uvumilivu viwe mwongozo wetu manake musa utafika tu.

  Naomba kutoa hoja....... Merry Xmass Mh. Kafulila (as he then was)  mwenye e
   
 2. k

  kiomboi JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  pole sana, ndugu kafulila!!
   
 3. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Merry christmass and happy new year kafulila uache utoto wa kisiasa ulifikiri chadema wanakuonea sasa Nccr ni majembe hawarembi full kazi unazani wanapenda ruzuku kule politics za majitaka Na ole wako urudi ccm Yuko wapi Ngawaiya wa Tlp amechoka kisiasa kwelikweli .
   
 4. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Tunasubiri mgogoro wa DANDA NA MBATIA
   
 5. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  sishirikiani na wanafiki na watovu wa nidhamu kamwe
   
 6. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,078
  Trophy Points: 280
  kulewa madaraka uko kaka, wacha awe kapuku kama sisi, arudi kijiweni kama sisi tu.
   
Loading...