Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Kwa tuliobahatika kuushudia utawala wa mwl JKN ni wazi kabisa kuwa ni mashuhuda kuwa tuliishi maisha yasiyo na stress
Kuanzia shule ya msingi mpaka Chuo Kikuu ilikuwa ni bure, huduma za afya bure. Kulikuwa hakuna matabaka maana hakuna cha mtoto wa kigogo au kibopa kusoma shule tofauti na watanzania wenzako, kwa ujumla maisha yalikuwa ya raha. Tuachilie mbali setbacks zilizoukumba utawala wa Mwl JKN kwa ujumla alijitahidi sana
Lakini hii ni kwa sababu utawala wa mwl ulitumia vizuri mapato ya serikali ndio maana aliweza kuhakikisha huduma za jamii kama elimu, afya, zinamfikia kila mtanzania.
Kitendo cha serikali ya awamu ya tano kukusanya tril 2 huku matumizi ni tril 1.8+ ni ushahidi tosha kuwa sasa tunaweza kurudi kule alipotuacha Mwl JKN.
Ni wazi kuwa tutaweza kulipia huduma za msingi kama afya na elimu bure kwa watanzania wote. Tunaweza kuanza na elimu bure mpaka kidato cha sita, pia huduma za afya ziwe bure kwa wananchi wote.
Kisingizio kuwa pato la taifa ni dogo na hivyo cost sharing kwenye afya na elimu iwepo hakipo. Hivyo huu ndio wakati wa kuirudisha Tanzania aliyotuachia Mwl JKN.