Natarajia kufunga ndoa, nipe maneno ya hekima yatakayonisaidia

haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
837
1,550
Habari wakuu,

Mimi ni ME, wiki chache zijazo natarajia kuingia katika ndoa, naomba wenye uzoefu na wanaofahamu mambo wanipe maneno ya hekima yatakayonisaidia kwenye maisha ya ndoa. Usiniambie kataa ndoa kwakua nimeshafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa.

Natanguliza shukran zangu za dhati.

1684825507527.png

Simama kama mwanaume ndani ya nyumba yak0...Usichekelee jamb0 la kipuuzi hata likiwa d0g0 mana Ukilichelea litakuwa kuja kuwa kubwa....Acha gubu la chakula...Balance upend0 hakikisha usizidi na usipungue sana....Usiweke simu paswed iache huru...Ukiwa na mchepuk0 sajili lain ya ingine na hakikisha mchepuk0 hapajui kwak0....Usimpige mke0 us0ni....Ukimfumania Mke0 muache taraka 5 usimpe nafasi ingine msaliti......
 
Maisha ya ndoa hayana formula ndugu. Uzuri na ubaya wake hutegemeana na utakaeoana nae.

Kikubwa ni ustahamilivu. Kuna kipindi ndoa inakera mpaka unafikia kujuta kuoa lakini ina raha zake pia.

Jaribu kujishusha inapobidi hasa kwa makosa madogo madogo yasiyokuwa na athari kubwa kimaisha. Neno Samahani huepusha mengi sana katika ugomvi wa kwenye ndoa.

Kumbuka unaweka rehani uhuru wako. Yale unayoweza kufanya sasa ukiwa single hutoweza yafanya tena hivyo ni wakati muafaka kumaliza makando kando yako yote.

Ndoa sio utumwa kusema mmoja awe juu ya mwingine. Hakuna kazi za kike ama kiume za nyumbani. Kuna kipindi kusaidia kukunja nguo zilizofuliwa tu ama kumtaarishia mwenzio kikombe cha chai kunaweza ongeza upendo mwingi baina yenu (it's the smallest of things that matter and count the most).

Jaribu kutatua tofauti zenu nyie wenyewe pasi kushirikisha watu wa nje. Si kila anaekushauri kuhusu ndoa yako anafanya hivyo kwa upendo. Wengine wanakushauri ovyo sababu hawapendi ndoa yenu.

Na si kila lile mnaloweza samaheana linaweza sameheka na wengine. Kitendo cha kushirikisha wengine katika tofauti zenu kunaweza jenga chuki baina ya mmoja wenu na ndugu/jamaa mliowashirikisha katika hitilafu zenu hata baada ya nyinyi wenyewe kusameheana.

Jaribu kuweka mipaka baina ya marafiki na ndoa yako. Si kila jambo lenu liwe wazi kwa marafiki. Mengine yabaki kuwa siri yenu wawili tu.

Yaliyobaki utajifunza ukiwa ndani ya ndoa. Mola afanye ndoa yako iwe yenya heri na faraja.
 
Habari wakuu,
Mimi ni ME, wiki chache zijazo natarajia kuingia katika ndoa, naomba wenye uzoefu na wanaofahamu mambo wanipe maneno ya hekima yatakayonisaidia kwenye maisha ya ndoa.
Usiniambie kataa ndoa kwakua nimeshafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Hongera sana kwa maamuzi ya kuoa umewashinda kundi la Vijana wanaoendesha vibe la kataa ndoa eti ndoa ni utapeli ,ushauri wangu kwako unatokana na maana ya neno lenyewe ndoa;

N~Neno la Mungu,neno la busara na hekima lijae kwa wingi kwenu.
D~Daima mtegemee Mungu usitegemee status yako status haina garantee yaweza shuka au ikapanda zaidi na kuleta tafrani usiotatajia.
O~ Ombaneni msamaha mnapokeseana
A~ Amani itawale maisha yenu siku zote,Amani ndani ya ndoa yenu ndio iwe kipaumbele namba moja usikubali amani itoweke uipambamie kwa gharama.zote ndipo utafurahia maisha ya ndoa

Nawatakia maisha mema na ya baraka tele kwenye maisha ya ndoa yenu.
 
Habari wakuu,
Mimi ni ME, wiki chache zijazo natarajia kuingia katika ndoa, naomba wenye uzoefu na wanaofahamu mambo wanipe maneno ya hekima yatakayonisaidia kwenye maisha ya ndoa.
Usiniambie kataa ndoa kwakua nimeshafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Ujue tu ndoa ni kama kiumbe kisichoonekana. Kinatunzwa.

Pia ndoa ni kama mlima ambao lazima uupande kila siku na unapopanda lazima nyote wawili muwe mmeshikana mikono, ili mmoja akichoka mwingine amsaidie, na hivyo mnaendelea kupanda wote. Msiposhikana mikono ndoa lazima ife, maana mmoja atachoka na atajiondoa.
 
Weka akilini kuwa kuna sku utamfumania... Itakuepusha na mengi ( kuchapiwa ni Siri ya ndani )
 
Simama kama mwanaume ndani ya nyumba yak0...Usichekelee jamb0 la kipuuzi hata likiwa d0g0 mana Ukilichelea litakuwa kuja kuwa kubwa....Acha gubu la chakula...Balance upend0 hakikisha usizidi na usipungue sana....Usiweke simu paswed iache huru...Ukiwa na mchepuk0 sajili lain ya ingine na hakikisha mchepuk0 hapajui kwak0....Usimpige mke0 us0ni....Ukimfumania Mke0 muache taraka 5 usimpe nafasi ingine msaliti......
Mbona una substite o na 0? S
 
Habari wakuu,
Mimi ni ME, wiki chache zijazo natarajia kuingia katika ndoa, naomba wenye uzoefu na wanaofahamu mambo wanipe maneno ya hekima yatakayonisaidia kwenye maisha ya ndoa.
Usiniambie kataa ndoa kwakua nimeshafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Tambua ya kwamba mwanamke ni binadamu ana matamanio ya kimwili so kigegedwa na wanaume wengi ni jambo la kawaida. Usije ukavunja ndoa eti kisa mke katombwer huko nje
 
Back
Top Bottom