Elections 2010 Natangaza rasmi nia ya kugombea udiwani

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Wakuu,
Leo nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nimechoka kuwa vuvuzela na badala yake naingia ulingoni kugombea udiwani katika kata moja ya huko Kwetu kwa tiketi ya Chadema.

Hivi ninavyoandika hapa nimeshachukua fomu na niko katika mchakato wa kupata wadhamini 25 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za chama changu.

Nimechoka kukaa nikilalamika tu hapa JF lakini nimedhamilia kuwa mpinzani wa kweli wa serikali ya Kikwete. Sihitaji kuwa Vuvuzela hapa JF, bali nataka kufanya kwa vitendo.

Nawashauri wana JF wengi tujitolee kuingia katika uwanja wa mapambano haya bila uoga. Wanahitajika wabunge na madiwani wengi tu sasa. Nchi yetu inatuhitaji sana kama wakombozi. Si vema kuendelea kupiga kelele hapa bila kuchukua hatua.

Kwa wale wana Chadema walio nje ya nchi na wanaweza kuja kuingia katika vita hii ya October waje tushirikiane. Wale wasioweza watu support kwa shekeli au waje wawe mawakala wetu.

Tuendelee kuombeana ushindi.

MF
 
Hongera kwa hatua hii kuwa sehemu ya mapambano,good.
Ila kuasehemu nataka kukusahihisha kidogo,Nadhani ukishinda utamsaidia Slaa kuongoza Tanzania ,Kikwete uraisi wake unakoma 0ctober31,2010 so hutakuwa mpinzani wa kikwete tena ingawa kwa sasa you're.
Kwa mara nyingine tena hongera kwa hatua yako
 
Kila la heri na mafanikio Mkuu katika kampeni zako.
 
Kila la kheri katika safari yako. MS nikuase kidogo kuwa kila jambo linaanza na idea, na huenda baadhi ya idea ndani ya JF ndizo zimekupa msukumo wa kwenda mstari wa mbele kimapambano, hivyo si vema kusema kuna mavuvuzela. Ni kaushauri ka kukupa kasi na kukutia jazba na hamasa huko uendako. Kila penye nia kuna njia, basi mwenyezi akupe baraka zake.
 
Nguruvi3, hapo kwenye red usimchanganye huyu mtu na Malaria Sugu!...Nadhani ulimaanisha MF.
Hata hivyo jinalako limeniacha mdomo wazi, maana kikwetu linamaanisha MUNGU!

By the way, MF huo ni uthubutu-chanya!.Nakupongeza sana kwa hatua hiyo, na nitakusaidia kimawazo!
 
Ahsante PakaJimmy, nilimaanisha MF kama ulivyoanisha. All in all kila la heri MF.
 
Wakuu,
Leo nachukua fursa hii kutangaza rasmi kwamba nimechoka kuwa vuvuzela na badala yake naingia ulingoni kugombea udiwani katika kata moja ya huko Kwetu kwa tiketi ya Chadema.

Hivi ninavyoandika hapa nimeshachukua fomu na niko katika mchakato wa kupata wadhamini 25 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za chama changu.

Nimechoka kukaa nikilalamika tu hapa JF lakini nimedhamilia kuwa mpinzani wa kweli wa serikali ya Kikwete. Sihitaji kuwa Vuvuzela hapa JF, bali nataka kufanya kwa vitendo.

Nawashauri wana JF wengi tujitolee kuingia katika uwanja wa mapambano haya bila uoga. Wanahitajika wabunge na madiwani wengi tu sasa. Nchi yetu inatuhitaji sana kama wakombozi. Si vema kuendelea kupiga kelele hapa bila kuchukua hatua.

Kwa wale wana Chadema walio nje ya nchi na wanaweza kuja kuingia katika vita hii ya October waje tushirikiane. Wale wasioweza watu support kwa shekeli au waje wawe mawakala wetu.

Tuendelee kuombeana ushindi.

MF

hongera sana ni haki yako ya kikatiba na ya msingi,kazi buti maana ccm si mchezo
 
Hongera mzee. Nilipokuwa naona michango yako nilikudhania kuwa unafaa zaidi kuwa mbunge. Lakini serve it, Kwa sasa anzia na udiwani...
 
Back
Top Bottom