Natangaza rasmi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan

84 ya Magu
5 ya Samia
1 ya Tundu, Zito na wenzao😅😅😅
10 zilizobaki unamoa Nani?
Kumbuka ni mapema kujimilikisha Samia maana huyu ni mzenji halisi hivyo hatabiriki Kama masoud alivyomfanyia sheni
 
Jina lake ni Samia=nimesikia, Suluhu=upatanisho, Hassan=mwema.

Wahenga wanasema jina huumba, utakuta mtu anazaa mtoto anamwita Shida, Taabu, Bure, Nyama yao, Chibuku, Chimpumu nk, majina ya ajabu!!!, mtoto akiwa hovyo anaanza kumshutumu anasahau kwamba ni yeye ndio sababu kwa kumpa jina bovu.

Mwingine anamwita Mtoto majina ya ulevi eg Pombe mtoto akianza kuropoka ropoka kama mlevi unalalamika.
 
Amani iwe nanyi wana JF!

Mwaka 2017 nikiwa mwanachama wa CCM niliamua kuacha kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi baada ya kugundua kuwa sera zake chini ya aliyekuwa Rais JPM sizingetufikisha popote kimaendeleo kama Taifa.

Sera za kukumbatia uchumi wa kijamaa wa kutaka serikali ndo ifanye biashara huku akiwatesa Wawekezaji na kufanya mamilioni ya Watanzania kupoteza na kukosa ajira zilisababisha niache kumuunga Mkono Magufuli na CCM kwa ujumla.

Tabia zake za kupenda sifa binafsi huku akitaka atukuzwe na akipoteza watu wote waliokuwa wakimpinga au kumkosoa kwa kuwaua na kuwapa kesi mbaya kulisababisha niache kabisa kufuatilia siasa zake.

Hayo yote tisa, kumi ni tukio la jaribio la mauaji ya Tundu Antipass Lissu. Pamoja na kuwa Mimi nilikuwa CCM ila nilikuwa nakubali michango ya Tundu Lissu Bungeni hasa kwenye mambo ya Sheria, haki na demokrasia, Tundu Lissu alileta michango mizuri na inayojenga bungeni Kama wabunge wenzake wa CHADEMA.

Tangu Rais Samia Hassan Suluhu ashike usukani wa kuliongoza Taifa letu nimesikiliza hotuba zake kama nne. Na kwenye hotuba zake zote nilizozisikiliza, nimegundua pamoja na elimu yake ya kawaida sana, ni mtu mwenye exposure ya kiwango cha juu sana hasa linapokuja suala la maendeleo. Nimesema haya kutoka moyoni kwa sababu zifuatazo;

1. Mama Samia ameonesha kujua tatizo kubwa linaloikabili nchi yetu kwa sasa ni ajira kwa vijana wetu na kuwa hili ni bomu ambalo kama halitashughulikiwa ipasavyo, basi nchi yetu itajikuta kwenye sehemu mbaya sana kiutawala siku si nyingi. Tanzania yenye watu karibu Mil 60 , kila mwaka inazalisha wahitimu wa vyuo mbalimbali wanaofikia elfu 25. Hawa watu wasipowekewa mazingira mazuri wakaajiliwa na kujiajiri basi nchi inaweza kufika pabaya sana miaka michache tu ijayo. Hotuba zake zilizojikita kwenye kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuwekeza kwenye miradi ya kimakakati ya kukuza ajira imenifanya nione kuwa ni mtu sahihi tunayemuhitaji kwa sasa

Kwa kugundua hili Mama Samia ameweka msisitizo na nguvu kubwa katika kubadili mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi ambao watatengeneza fursa za ajira na kujiajiri kwa vijana wetu. Kwa hotuba yake ya leo, nimehitimisha kwa kuliona hili jambo kwa asilimia 100.

2. Anawekeza zaidi katika kutumia akili kwa kiwango kikubwa na nguvu kiasi jambo ambalo Nina uhakika litakuja kumpa matokeo mazuri sana hapo mbeleni. Kwenye hili nimeona anavyosisitiza hasa kwenye masuala ya mfumo wa kodi na uwekezaji akisema anataka kuboresha mfumo wetu wa kodi ili watu wengi zaidi walipe kodi na kiwango cha kodi kuwe stahimilivu ili wote tuchangie maendeleo ya nchi yetu bila kuumia huku tukijenga uzalendo kweli. Kwenye hili nampa pia pongezi Mama Samia Kwa sababu kwa kufanya hivi Nina uhakika atapata support kubwa si kutoka Kwa wananchi tu bali hata Kwa walipa kodi wa hapa nchini.

3. Maono yake ya kuboresha namna ya ufugaji wetu na Makazi ya wananchi. Mama Samia ni mwana Ccm wa pili niliyemsikia alizungumzia hili baada ya Prof Muhongo kwenye hotuba yake ya kuomba ridhaa ya CCM kuhombea uraisi pale mwaka 2015. Katika dunia ya sasa ni aibu Kwa ufugaji unaofanywa na jamii za kitanzania Kwa sababu kwanza unahatarisha mazingira kwa kuharibu uoto na kueneza ukame, lakini Pia ufugaji wetu unatuweka kwenye hatari kubwa ya kupoteza uoto wetu wa asili kama Taifa katika miaka michache ijayo. Njia pekee ya kubadili aina hii ya ufugaji ni kuwapa teknolojia mpya wafugaji kuwawezesha kufuga kibiashara katika mazingira madogo. Hili litaokoa sana mazingira yetu na kufanya tuwe na nyama Bora ambayo tutaiuza kwenye masoko ya nje yenye ushindani.

Kwa haya mambo matatu niliyoyaona kwa Mama Samia hadi leo, Mimi Lord denning napenda kusema baada ya kuachana na siasa za Chama cha Mapinduzi kwa miaka karibu 4, sasa Mama Samia Suluhu Hassan, amefanikiwa katika kurudisha imani yangu tena juu ya Chama hiki Kwa sababu nimeona kumbe bado kuna watu wenye akili ambao wanaweza leta kweli mabadiliko chanya hapa Tanzania.
CCM ni chama kinachoungwa mkono na watu wa aina tatu. 1.wenye njaa wanaojali matumbo yao 2. wakristo wenye siasa kali 3.wendawazimu.
 
Back
Top Bottom