WANAJF:
Kwa heshima na taadhima napenda kuutangazia Umma wa Watanzania popote walipo chini ya Jua kwamba nimeamua kwa dhati kabisa bila kushawishiwa na mtu yeyote bali ni kwa msukumo wa Uzalendo na upendo nilionao kwa nchi yangu ya Tanzania, ambayo imekuwa na hali mbaya sana na inazidi kuwa mbaya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kisiasa kila kukicha. Na mbaya zaidi hali ya maisha kwa wananchi walio wengi inazidi kuwa mbaya, kwani gharama ya maisha inazidi kupanda kila sekta.
Nimekuwa mwanachama wa CCM mwaminifu toka nilipozaliwa na sasa yapata miaka 33 na tawi langu ni Ubungo. Mwaka 2005 nikiwa chuoni, nilikuwa kati ya watu waliomfanyia kampeni Rais wangu Kikwete ili kuweza kuwa Rais wa Tz. Kwanza kabisa katika harakati za kupata mgombea wa CCM kule Chimwaga Dodoma, siku hiyo nilishinda kwenye TV nikiomba JK Kikwete ashinde. Na siku hiyo hata vipindi sikuweza kuhudhuria kwasababu ya msisimko niliokuwa nao na kutaka hasa Kikwete aweze kuwa mgombea kwa tiketi ya CCM, na ndivyo ilivyotokea. Hakika nilifurahi sana na mara moja nilianza kuhamasisha vijana wenzangu na hata ndugu zangu vijijini ili kumpigia Kikwete kura. Mwisho wa siku alishinda na hakika ilikuwa furaha yangu kuu sana, LAKINI, LAKINI, LAKINI!!!
Mara tu Rais wangu alipoingia madarakani na nikaanza kupima uwezo wa utendaji wake, teuzi zake ambazo nyingi hazizingatii vigezo bali zimejaa walakini, na mwelekeo wa nchi kiujumla, hakika nilianza kupoteza matumaini na Rais wangu na serikali yake kwa ujumla. Hatahivyo, niliendelea kuwa mwanachama wa CCM mwaminifu nikiwa na matumaini kwamba ipo siku Rais wangu akipata Uzoefu katika ngazi ya Urais, ndipo ataanza kuleta mabadiliko makubwa katika ngazi zote hasa za kiuchumi na maendeleo. Nilitoa kama miaka 3 kwa Rais wangu ili apate Experience, lkn sikuona faida ya huo uzoefu na hata sasa ana uzoefu wa miaka karibia 7 kwenye Urais lkn hakuna faida,na badala yake Tz imefanikiwa kuingia kwenye 3 Bora ya nchi zinazoongoza kwa Ombaomba Duniani,tukiwa na Iraq na Afghanistan.
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana kuhusu OMBAOMBA hasa TZ yenye rasilimali lkn sipati majibu, je ni kweli hatuna kabisa watu makini ambao wanaweza kusaidia uchumi wetu kuimarika? Jibu nililo nalo ni kwamba TZ ina watu wazuri sana lkn tatizo liko kwenye mfumo wa taasisi zetu mbalimbali na serikali yetu kiujumla. Pia nikasema na ninaamini kwamba RAIS wangu hakuwahi, hana, na hatakuwa na VISION ya wapi anataka kuipeleka Tanzania.
Ndg. Wanajf naomba nisiwachoshe na maneno mengi lkn naomba niseme hili, kwamba naomba msamaha kwa wana-CCM wenzangu ambao nimekuwa nao kwa kipindi chote hicho akiwemo marehemu baba yangu aliyewahi kuwa Kiongozi wa CCM na serikali katika ngazi ya Kata na Kijiji kuhusu maamuzi haya ya kuachana na CCM na kujiunga CHADEMA, chama ambacho kinaonekana kuwa na vision ya kuibadilisha Tanzania. Naomba wale wote nitakaowakwaza kwa maamuzi yangu haya wanisamehe na kamwe wasinilaumu kwasababu si mimi niliyeamua BALI NI MSUKUMO WA UZALENDO NA UPENDO KWA NCHI YANGU TANZANIA ndiyo maana nimeamua Kuvua Gamba na Kuvaa GWANDA.
KWAHIYO: Kuanzia leo tarehe 01.06.2012, Mimi TELO, nikiwa na akili zangu timamu na kwa uwezo wangu wote na kwa upendo na Uzalendo nilionao dhidi ya nchi yangu Tanzania, Natangaza Rasmi kwamba Nimekuwa Mwanachama wa CHADEMA.
WITO: Nawaomba Watanzania wote popote mlipo chini ya JUA, tuungane kwa pamoja kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu. Na huo muungano ninauongelea hapa ni kwa kujiunga na CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
Natanguliza shukrani sana, kwani hatimaye NIMEKUWA HURU; TENA HURU KWELI KWELI baada ya kuachana na maumivu ambayo nimekuwa nayo tangu mwaka 2005.
Ni mimi,
TELO
01.06.2012