Natangaza rasmi kuachana na masuala ya Siasa, nina ya kujutia mengi

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Nimekuwa naandika Sana kuhusu mambo ya siasa,
Nimekua napewa baadhi ya tetesi nazirusha hapa,

Nimekuwa na Mlengo wa Chama Cha Mapinduzi kwa Muda mrefu

Kuna muda nimeshabikia mambo ya Kinyama yaliyofanywa na Chama changu cha Mapinduzi

Nayakumbuka Matukio

1.Nimeshiriki sana Kuiba kura za wapinzani

Nimeshiriki Mafinga,Bukoba vijijini, Nimeshiriki Hata kura za kitaifa, mbinu nyingi CCM wanazitumia kuiba kura,

2.Nimeshirika Cyber war kwa kipindi cha Kampeni za Magufuli, na kushiriki kuwachafua viongozi wa upinzani

3.Nitaandika Nitaandika mengi ila naishia hapa kwa sasa


Suala linaloniuma na Kujuta ni la Mheshimiwa Lissu Kupigwa Risasi nikafurahia, lakin kadri muda ulivyopita nika kaa na kuwaza kwamba tuweke chuki pembeni tutangulize ubinadamu
Sitashiriki Kampeni yeyote ile
Sitashiriki Siasa kivyovyote vile


Nitabakia kuwa Mtazamaji tu

Britannica,
Vladivostok, Russia
 
Hongera kwa uamzi mzuri na mgumu kama ni kweli unachokisema!, ila ningekuomba usiache siasa ila fanya siasa safi, nyeusi wambie watu kuwa ni nyeusi na kama ni nyeupe waambie watu ni nyeupe!.

Naamini unayo yafahamu ni mengi katika siasa za nchi yetu, ukifanya hilo nililo kushauri watu wataelimika, watapona na kujua siasa za nchi yetu!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom