President Elect
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 693
- 212
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu wananchi, tunawajibika kuandamana kwa amani nchi nzima kupinga adha tunazopata kutokana na ugumu wa maisha uliokithiri.
Kuanzia kesho saa nne asubuhi wananchì wa mkoa wa Dsm tutaandamana kwa amani tukiwa tumeshika vitambaa vyeupe kuanzia Manzese darajani hadi viwanja vya Jangwani. Nitaendelea kutoa ratiba kwa maandamano kama haya kwa mikoa yote nchi nzima kwa muda wa siku saba kuanzia kesho.
Inshallah, kwa pamoja tutaweza kubadilisha na kuboresha mustakabali wa nchi yetu. Hakutakuwa na haja ya mabango, kitambaa cheupe kinatosha, pamoja kwa amani tutapita pembezoni mwa barabara bila kubugudhi magari ambayo maskini wala hayana mafuta, na bila kuharibu mali au kuleta uvunjifu wa amani.
Asanteni kwa ushirikiano wenu.