Natangaza kugombea ubunge 2015 - ROMBO kwa tiketi ya CHADEMA

Ni kweli kaka Wananchi wa Rombo hawachezewi.

Ekellei,

Thanks

Leyana Lesindamu,

Hongera kwa kutumia haki yako kidemokrasia.Tujenge chama kwanza.Nina imani Rombo watajitokeza wagombea zaidi ya 30 hadi ifike 2015

Ila sikumbuki kuongea na mtu mwenye jina hili kuhusu jimbo la Rombo

Ben unafiki kwangu mwiko na nitasema kweli daima.Joseph Selasini ameshindwa kutatua changamoto za Rombo.Nilienda kikazi kule mwaka jana watu wengi wa kule wanamlaani.Ila nilifurahishwa na kitu kimoja kwamba wananchi wana imani kubwa na CDM kama chama lakini sio Selasini.Jitahidini kuzidi kuimarisha chama huko na hakikisheni mnaandaa vijana kugombea nafasi za udiwani ili 2015 muongoze halmashauri.Lakini andaeni mgombea wa ubunge anayefaa kwa haki Selasini hafai.Nawasilisha.
 
Nimekupata kamanda.
 
Mkuu Leyana, sawa kabisa. Anza mikakati mapema hasa ya kuvalishwa makamanda magwanda ili wakati ukifika upite kwa urahisi.

Vipi Meku, nasikia huko Kilindic - Tanga Mashamba ya kilimo yanapatikana na yana rutuba. Vipi ni bei gani kwa heka? Title deed inapatikana?

Je barabara zinapitika? Tafadhali naomba unipm
 
haahaha, ebana eee, Beni kumbe upo kamanda!! LaLesindamu kazi inahitajika sana kule rombo, madiwani wanatakiwa wa kutosha anza sasa kujijenga
 
haahaha, aisee kumbe tupo wengi hivi? duh kweli tunahitaji kujipanga sana.... OK Mkuu LaLesindamu, usigombee kwa sababau umeombwa kugombea ila gombea kwa sababau umeona gap (ombwe) katika uongozi uliopo, na uje hapa utumabie umeona nini na umejipanga vipi kukabiliana na hitaji hilo! sasas hii ya kutuambia ohhh umetumiwa ujumbe na watu wazee, ugombee, sory I berg to differ! Mwisho wa siku utatuambia si mliniomba wenyewe, kwanza sikutaka kugombea!!!

Any way nakutakia kila la heri tukutane kwenye uchukuaji wa form!!! hahahahahah...

Kwa kweli siasa za Rombo ni ngumu sana hasa ukizingatia changamoto zilizopo, kina salakana watakuambia kulichowakuta, Mzee Pesambili naye pamoja na kujitahidi sana ingawa sio kama matarajio ya wengi watu walimpiga chini... Pale Rombo si pa kusubiri uombwe kwa kweli panahitaji ukomavu wa hali ya juu katika medani ya siasa na jinsi gani utawasaidia wana ROmbo kupata Maji ya kuaminika, muhimu Kuinua Uchumi wa watu wa Ukanda wa chini!!

Mungu Ibariki Rombo, Mungu Ibariki Tanzania!
 
ok sasa sisi wana jamii tukushauri nini?wakati umeamua?asilimia kubwa ya watanzania wanataka vyeo kwa ajili wasifiwe,au wapate mali kwa urais au wapate wanawake(pamoja na wake za watu) kukwepa kodi na kuonekana kwenye luninga watu wajue we ni shujaa,na kuweka watu ndani kwa mamlaka yake n.k,Ila ni vizuri kama unagombea uwe umeguswa na matatizo ya watu na umefikiri jinsi ya kutatua na umeona kuwa unaweza kuwasaidia,sasa mi naona ingekuwa vizuri uandae profile,alafu proposal sasa utuombe ushauri.
Wengine walikuja hivyo hivyo wakapata ubunge na mpaka uwaziri lakini wanachofanya ni kwenda kulala bungeni,wazee hawana jipya,tafuta wataalam wakushauri,wazee wameshauri lakin miaka hamsin hakuna kitu,alafu pia lazima uwe na source ya fund rising na ufanye projection kujua ita cost how much.
OMBA USHAURI KWA VIJANA PIA NI MORE THAN 50% YA WANANCHI WOTE

Nimekupata kamanda.

heshima kamanda Ben! Hivi yule kilaza anayejiita nuclear1 alokuwa anataka kutumezesha sumu za majungu na fitina kwamba ww hufai yupo wapi siku hizi? Au kapigwa ban nn?
Kaka usikonde tuendeleze mapambano mpaka kieleweke.
Solidarity forever
Shardcole@Tabora1
 
Nimekupata kamanda.

Nimefuatilia huu mjadala toka mwanzo.Hakika Rombo inahitaji damu mpya.Rombo inahitaji aina ya wabunge machachari mfano wa kina Mnyika,Zitto,Nassari,Sugu,Wenje na wengineo wengi.Huyu Selasini hajawahi kufanya mikutano ya kujenga chama jimboni kwake hata ile ya kushukuru wananchi.Rombo imelala kana kwamba haiko kaskazini yenye muamko mkubwa wa mageuzi.Frankly Speaking niko nyuma ya wale vijana wapiganaji watakaojitosa kwenye kura ya maoni ndani ya CDM kumng'oa huyu vinginevyo CDM itakuwa inaweka jimbo rehani 2015
 
Nimempata vizuri mtoa mada,huenda hana nia ya kugombea rombo ila alitaka cdm itambue ya kuwa aliyepo rombo sio mtu sahihi,ni ukweli cdm rombo haitabiriki..bado kuna kazi kubwa.
 
usisahau kufika TARAKEA kijiji cha mbomai juu nikupe kikombe cha kahawa kabla hatujaanza safari ndefu ya ukombozi
Asisahau NDUWENI, KASIRWA, REHA na NAYEME as hayo maeneo kwa pamoja ndiyo yaliyompa Selasini Ubunge as alipojua huko ndiko kulikokuwa na wapiga kura wengi alimrudisha Slaa kule mara ya pili baada ya kushauriwa na ma-strategist wa CDM ili kukolezea.....
 
2005 tano ulikuwa umefanya nini? kwa sasa sawa! lakini usichanganye maelezo
 
Natangaza rasmi 2015 nitagombea ubunge-Rombo kupitia CDM. Nimeamua kufanya hivyo baada ya kutafakari kwa mda mrefu maombi ya makundi mbalimbali ya jamii ya wana Rombo kugombea tangu mwaka 2005 na hivi juzi ujumbe wa wazee watatu wa Rombo walinifuata Kilindi-TANGA ninakofanya kazi wakinitaka nisiwaangushe 2015. Wadau nishaurini.
Kwako LEYANA LESINDAMU,

Nakutakia kila la heri katika kusudio lako la kutaka kuwa Mbunge wa Rombo, nina kutakia kila la heri kwani ninaamini wewe ni mwanachama hai wa CHADEMA.

Mbali na kukutakia heri hiyo ningependa unifahamishe yafuatayo ili nikitaka kukushauri namna utakavyoupata Ubunge huo wa Rombo niwe na maelezo ya kutosha:

1) wewe kama mwanachama hai wa CHADEMA, umechangia nini ili kumuwezesha Mbunge wa sasa wa CHADEMA kufanikisha malengo ya kuwaletea maendeleo watu wa Rombo kama ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA ya 2010 inavyoelekeza?

2) Hao wazee ambao wamekufuata na kukushauri ukagombee ubunge huko Rombo 2015, je. umebahatika kuwauliza wamejishughulishaje kumsaidia Mbunge wa Sasa wa Rombo kufanikisha azma ya kuijenga Rombo kimaendeleo?

3) Je, umejiridhisha vipi kuwa hawa wazee waliokufuata wana nia njema na wewe pia na Chama chako cha CHADEMA?

4) Kwa kuwa lengo la CHADEMA ni kuongoza nji hii mwaka 2015, na hili litawezekana kama watapata wabunge wengi wa kuchaguliwa, je ni kwa nini hufikirii kugombea maeneo ambayo CCM inaongoza majimbo kiubunge?
 
Hili ni jambo jema sana kwani vijana wanahitajika sana kujihusishwa moja kwa moja na siasa kwani ndio njia rahisi ya ku influence sera na mipangilio ya nchi yetu na rasilimali zake ambazo kwa kiasi kikubwa wazee tuliotegemea watengenezee vizazi vijavyo mazingira bora zaidi, badala yake wamekuwa wanatafuna kila kitu. Ni muhimu kwa vijana kuchukua hatua sasa na sio baadae.

Ukumbuke daima pia kwamba hiyo ni haki yote kikatiba na ni vizuri kuomba ushauri kutoka kwa vijana wenzako humu, hasa ukizingatia kwamba unaweza pengine kukuta wapo vijana wengi humu wenye uzoefu au ufahamu na jimbo lako kikazi na pengine hata kimakazi.

That being said, kwa mtazamo wangu, katika hatua ya sasa, unachotakiwa kusema ni kwamba unatangaza nia ya kuomba kuchaguliwa kuwa mgombea ubunge katika mchakato wa kura za maoni kupitia chama cha demokrasia na maendeleo 2015. Wazee kukuhitaji ni sehemu tu ya mchakato, una kazi kubwa zaidi ya kupitishwa na vikao husika vya chadema kwani pamoja na kwamba Chadema ina malengo ya kuongeza viti vyake bungeni, nadhani kuna taratibu zinazotumika na chama ili kuwapata wagombea ambao chama kinaona wana sifa zinazo hitajika. Ushauri wangu ni kwamba fanya utafiti kuhusu mchakato mzima; pili kama ulivyoshauriwa, siasa za rombo sio lele-mama, tafiti ili ubaini changamoto zilizowakabili wagombea wengine kama kina mramba, ngalai na hata selasini ambae inasemekana 2010 alimshinda mramba kwa kura sita tu.

Mbali ya haya, anza kujihusisha na shughuli zinazowagusa wananchi husika - ambao unatarajia kuwaomba ridhaa yao wakutume bungeni ukawawakilishe iwapo utafinikiwa kukiridhisha Chadema kwamba wewe ndio unastahili kuibeba bendera yake katika uchaguzi mkuu 2015 katika jimbo la Rombo; muhimu zaidi, kwa sasa anza kujihusisha na chama chako (chama unachotarajia kujiunga nacho?) katika jimbo lako lakini bila ya kumvunjia heshima au kumwingilia kazi mbunge wako wa sasa; jitahidi sana kukaa mbali na majungu na fitina kwani mwisho wake itakuwa ni malumbano yasio na tija kwa wananchi wa rombo, hasa katika nyakati hizi ambazo wanahitaji mbunge wao wa sasa awe na focus kwa asilimia mia. Vinginevyo again, una haki ya msingi ya kikatiba kuwania nafasi hiyo kama alivyokuwa raia mwingine yeyote, hivyo usione wengine watakaojitokeza kama maadui. Ni hayo tu machache hoping yatakusaidia japo kidogo katika kipindi hiki cha mikakati. Kila la kheri.
 
Asisahau NDUWENI, KASIRWA, REHA na NAYEME as hayo maeneo kwa pamoja ndiyo yaliyompa Selasini Ubunge as alipojua huko ndiko kulikokuwa na wapiga kura wengi alimrudisha Slaa kule mara ya pili baada ya kushauriwa na ma-strategist wa CDM ili kukolezea.....

asisahau kufika pia kelamfua,makiidi,mengwe,manda,ngoyoni,ibukoni,keni aleni,mkuu,mamsera,mrere,kiboro na kwingineko,selasini hamna kitu mangi,tumeshamchoka
 
Wewe bwana huwez kuwa mbunge wetu,unakaa Tanga unataka ubunge Rombo?MBUNGE wa Rombo 2015 lazima awe anayajua vizuri mazingira ya sasa ya jimbo na sio vinginevyo.njoo rombo tukuone.
 
asisahau kufika pia kelamfua,makiidi,mengwe,manda,ngoyoni,ibukoni,keni aleni,mkuu,mamsera,mrere,kiboro na kwingineko,selasini hamna kitu mangi,tumeshamchoka
Mkuu mamaya! Salute sana. Mie last week nimetoka Rombo kumalizia
my feasibility study and afta that ntajua ni nini cha kufanya.......wote waliotangaza nia at least i knw em na nina mpango wa kukutana nao so as to separate wheat from the chaff! Tushirikiane wadau coz rombo ikiwa juu ni mafanikio yetu sote na ndo tukitakacho.........all the best makamanda.!
 
Kwako LEYANA LESINDAMU,

Nakutakia kila la heri katika kusudio lako la kutaka kuwa Mbunge wa Rombo, nina kutakia kila la heri kwani ninaamini wewe ni mwanachama hai wa CHADEMA.

Mbali na kukutakia heri hiyo ningependa unifahamishe yafuatayo ili nikitaka kukushauri namna utakavyoupata Ubunge huo wa Rombo niwe na maelezo ya kutosha:

1) wewe kama mwanachama hai wa CHADEMA, umechangia nini ili kumuwezesha Mbunge wa sasa wa CHADEMA kufanikisha malengo ya kuwaletea maendeleo watu wa Rombo kama ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA ya 2010 inavyoelekeza?

2) Hao wazee ambao wamekufuata na kukushauri ukagombee ubunge huko Rombo 2015, je. umebahatika kuwauliza wamejishughulishaje kumsaidia Mbunge wa Sasa wa Rombo kufanikisha azma ya kuijenga Rombo kimaendeleo?

3) Je, umejiridhisha vipi kuwa hawa wazee waliokufuata wana nia njema na wewe pia na Chama chako cha CHADEMA?

4) Kwa kuwa lengo la CHADEMA ni kuongoza nji hii mwaka 2015, na hili litawezekana kama watapata wabunge wengi wa kuchaguliwa, je ni kwa nini hufikirii kugombea maeneo ambayo CCM inaongoza majimbo kiubunge?

Excellent analysis........
 
Kuna msemo unaosema kama wote tunajenga nyumba moja hakuna haja ya kugombea fito.
Pia nyumba bora inategemea sana msing wake.
Kwa maana hiyo wadau wote ambao wameonyesha nia na watakaoonyesha nia ni kuanza kujenga misingi kule Rombo ili mwisho wa siku nyumba isimamame katika misingi imara.Wanasema fimbo ya mbali haiui nyoka,je tumewezaje kujisogeza karibu na tunaotaka watupe dhamana ya kuwawakilisha katika chombo cha kutunga sheria?
Tunashiriki vipi maendeleo ya Rombo kwasasa na hasa kutoa elimu ya uraia kwa vijana ambao ndio wapiga kura wetu wa kesho?
Tumejipanga kuwajibu nini warombo watakapotuuliza tumeifanyia nini Rombo?
Tumemsaidiaje Mbunge ambaye tunataka kumrithi katika maendeleo ya Rombo?
Wakati ni huu wa kumpa mawazo yetu na kushirikiana naye ili akishindwa kutekeleza au kuendana na kasi ya maendeleo tumwambie akae pembeni na kijiti achukue mwingine akimbize.
Hivi mmewahi kujiuliza miaka mitano ijayo nani watakua huko Rombo kama wimbi la vijana wanaokimbilia mijini litaendelea kama lilivyo?
Tusipofikiri njia mbadala ya kushawishi vijana wabaki pale Rombo kwa kubuni miradi mbalimbali tutajikuta tuakua WABUNGE wa WATOTO na WAZEE na nguvu kazi yote itakua mjini ikisaka shilingi.
 
Kwako LEYANA LESINDAMU,

Nakutakia kila la heri katika kusudio lako la kutaka kuwa Mbunge wa Rombo, nina kutakia kila la heri kwani ninaamini wewe ni mwanachama hai wa CHADEMA.

Mbali na kukutakia heri hiyo ningependa unifahamishe yafuatayo ili nikitaka kukushauri namna utakavyoupata Ubunge huo wa Rombo niwe na maelezo ya kutosha:

1) wewe kama mwanachama hai wa CHADEMA, umechangia nini ili kumuwezesha Mbunge wa sasa wa CHADEMA kufanikisha malengo ya kuwaletea maendeleo watu wa Rombo kama ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA ya 2010 inavyoelekeza?

2) Hao wazee ambao wamekufuata na kukushauri ukagombee ubunge huko Rombo 2015, je. umebahatika kuwauliza wamejishughulishaje kumsaidia Mbunge wa Sasa wa Rombo kufanikisha azma ya kuijenga Rombo kimaendeleo?

3) Je, umejiridhisha vipi kuwa hawa wazee waliokufuata wana nia njema na wewe pia na Chama chako cha CHADEMA?

4) Kwa kuwa lengo la CHADEMA ni kuongoza nji hii mwaka 2015, na hili litawezekana kama watapata wabunge wengi wa kuchaguliwa, je ni kwa nini hufikirii kugombea maeneo ambayo CCM inaongoza majimbo kiubunge?

.....Japokuwa ni Muda mrefu lakini hii nimeipenda.. Ni maswali tosha kwa huyu Mtangaza Nia (Kinyume na sheria za Tume ya Uchaguzi)
 
kumtoa Selasini ni kuonyesha udhaifu wa chadema kwani sku zote aliyeteuliwa na kamati kuu ya chama ndiyo yuko sahihi, kama vp jaribu uone utaipenda mwanangu
 
Back
Top Bottom