Natangaza kihama kwa vibaka wa Tegeta kwa ndevu

Pole sana.Kama ulikuwa unatafuta sympathy nadhani sawa umepata.
otherwise kuna vibaka wangapi wanatumia JF ndo ukaamua uwaambie?Je ujumbe huu utafikaje kwa hao vibaka?
Wala hajakosea mkuu wanasema "Cry with someone. It's more healing than crying alone"
 
Kaangalie zile series za Death Wish by Charles Bronson utawamaliza wote na watakaobaki watakimbia mji
 
Nimecheka sana ..ila pole sana ndiyo maisha,nakumbuka nilibiwa mitaa ya mwenge simu pamoja na pesa sikuamini kama ni mie maana nilirudi kumsaka mwizi wangu tena usiku nikiamini kuwa nitamkamata,baada ya week kupita ilibidi nijikubali na maisha yanabidi yaendelee.

Shida niliyoipata nimwelezea kila ndugu,jamaa,marafiki zangu na hata wafanyakazi wenzangu kuwa nimeibiwa badala ya kunitia moyo wakawa wananicheka tu.
 
waendee kimya-kimya ndio mbinu ya kumshinda adui, sasa wewe unataka uwabandikie tangazo!

Siwezi kuwawekea tangazo, ila huyu jamaa nilimjibu tu hivyo kwa kuwa niliona kama anafanya kejeli.
 
Pole sana inatia hasira sana!hasa kama hela ya jasho lako!kama umekwapua kazini au hizo za deal ambazo kila siku mnazipata makazini ,hiyo ni sadaka!
 
Pole sana inatia hasira sana!hasa kama hela ya jasho lako!kama umekwapua kazini au hizo za deal ambazo kila siku mnazipata makazini ,hiyo ni sadaka!

Mkuu hiyo ni pesa ya jasho langu.
 
Mkuu asikwambie mtu, bora kama ingepotea kwenye mazingira ya kutatanisha, lakini hii ni dhaili kabisa vibaka wameiba.

Kama unavyojua leo weekend mafundi huwaambii kitu, inabidi wapate pesa.
Pole sana mkuu. Eneo lile linatisha na sijui kwa nini polisi wamepacha pawe kituo cha kuunganishia magari/usafiri badala y kule T/Nyuki. Vijana wenye nguvu na afya hawataki kufanya kazi zaidi ya kujidai wapiga Debe ili waibe. Ila Mkuu Next time weka pesa yako kwenye Tigo auM/PESA.
 
ushauri mzuri ila hiyo sentesi ya mwisho inautata japo imeeleweka kiasi.
 
ushauri mzuri ila hiyo sentesi ya mwisho inautata japo imeeleweka kiasi.
Yaani kuliko kubeba pesa taslimu aziweke kwenye huduma ya Tigo au M Pesa akazitoe huko mbele ya Safari kwa kuwa huduma hizi siku hizi hupatikana kila sehemu ya Dar es salaam.
 
Wewe utapandaje bus kama msukukule unatakiwa kabla hujapanda bus unakuwa care na kama ni asubuhi kwenye kugombania weka vitu vyako imara na usiwe unaangali tu mbele mwizi ukimwangalia machoni haji tena hata kama kavaa suti yani mm hakuna kitu ambacho niko nacho makini kama kuibiwa yani hupati kitu na usipo angalia nakupigia kelele mtaa mzima
 
Ndugu zangu leo imekuwa siku mbaya kwangu.
Nikiwa Tegeta kwa Ndevu nasubiria gari kwenda Bunju kuonana na mafundi (site), katika pulukushani za kupanda daladala jamaa wakaiba 480,000 kutoka kwenye mkoba wangu.
Nimekuja kushutuka baada ya kuingia ndani ya gari.
Sasa ntangaza vita ya mtu mmoja (Solo War), dhidi ya vibaka wa Kwa Ndevu.

Ukiwa na fedha nyingi, tumia hata bajaj ingefaa, pole sana.
 
Back
Top Bottom