Natamani wazee wangejiajiri watupe mifano!!

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Kuna dhana imejengeka nchini ya wazee kuwashauri vijana wajiajiri badala ya kutafuta kazi baada ya kumaliza masomo yao kwenye kada mbalimbali.
Wazee walioko kwenye utumishi wa serikali na sekta binafsi wanahusika katika hili.wazee wanauzoefu wa kazi na maisha.wanamitaji.kwanini wasiwaachie vijana ofisi wanazozishikiria makazini. watoe mfano kwa vitendo wa kujiajiri.
utafiti umefanywa wa kuridhisha kuwa suruhisho la ajira kwa vijana ni kujiajiri? unauhalisia huo utafiti kwa mazingira ya nchi yetu(Taxregime na kilimo cha kutegemea mvua) kwa mujibu wa utafiti wa uanzishaji wa biashara ndogondogo hapa Tanzania asilimia 90 zinakufa ndani ya miaka mitatu toka zilipoanzishwa kutokana na changamoto kibao zikiongozwa na Moja wapo ambayo ni kodi ya pango(Rent)

Sector nyingi zinachangamoto nyingi mnoo.Natamani wazee waanze kujiajiri watoe demonstration vijana tuige kutoka kwao. hata BIBLIA inasema Mzee mwenye hekima huwaachia wana wa wanawao urithi.urithi mliotuachia vijana ni upi mpaka sasa? ni ule wa kushindwa kutengeneza ajira na kututaka tujiajiri?
Taratibu wazee msitwike vijana nira/kongwa ambalo hamuwezi kulibeba.
God is watching you senior citizen
 
Mkuu unamaanisha Juma Mwapach haajirikia au hawezi kujiajiri mpaka kufukuzia uwaziri wa mambo ya nje?
 
Naona una utani na Steven Wasira
huyo ni.mmojawao!.hasa wanatunga sera na kukaa pembeni bila kuzijaribu!
any investment is risky taking,it is irreversible when you make it.watuonyeshe tunatokaje hapo? wao mbona mpaka miaka 80 wanahangaikia kazi sio kujiajiri?!!
 
Mkuu unamaanisha Juma Mwapach haajirikia au hawezi kujiajiri mpaka kufukuzia uwaziri wa mambo ya nje?
mkuu huyo Mzee ni wa kumsamehe bure.hajui alitendalo.anazidi kutoaminika.
 
Mada hii imebeba ukweli
Kuwa maji ufuata mkondo.
Wazee wetu hasa waliosoma, sio roll model ktk dhana hii ya kujiajiri.
Ila janbo hili halitondolei wajibu wetu wa kupambana ili kujiletea ufanisi na tija ktk maisha yetu.
Idadi ya watanzania wasomi na watumishi wa umma ni asilimia chache sana, ila wananchi wenye elimu ya msingi na sekondari ndo walio wengi.
Na group hili la pili ndio mfano mzuri kwetu vijana.

Lazima tuache kujitetea tu, wako wazazi wetu hawajaenda shule ktk maisha yao ya kupigana wamezeeka na waliweza hata kutuachia nyumba yenye vyumba vitatu na kutusomesha mpaka tumefka elimu ya juu.
Kwa uzoefu huu tunaamini juhudi na maarifa uvuta mafanikio.

Tatizo la vijana wasomi hasa tuliofika vyuo vikuu, mfumo wa elimu umetufanya kuwa watumwa ki fikra,
Unatufundusha kujiona sisi km watu special ambao tunapaswa kufanya kazi za namna fulsni hivi. Uku tukijiwekea tabaka hilo na ndg zetu ambao tunasema hawakwenda shule.

Hii changamoto kubwa kuikabiri kwani mfumo umetumia miaka kama kumi -20. Kukuprogram kuwa tegemezi.

Hivyo lazima mthubutu kuvua hiyo mantal slave thru changing your attitude.

Kisha jitambueni,
Muwe wavumilivu
Muwe na bidiii
Muwe na nidhamu
Maarifa mliyoyapata yawe mtaji wa kuyakabiri mazingira.

Aksanthe kwa kuelewa.
 
Mkuu unamaanisha Juma Mwapach haajirikia au hawezi kujiajiri mpaka kufukuzia uwaziri wa mambo ya nje?
kingunge naye aliahidiwa waziri ofisi ya rais kazi maalum, mungu apishe mbali huu ujinga.
 
Mada hii imebeba ukweli
Kuwa maji ufuata mkondo.
Wazee wetu hasa waliosoma, sio roll model ktk dhana hii ya kujiajiri.
Ila janbo hili halitondolei wajibu wetu wa kupambana ili kujiletea ufanisi na tija ktk maisha yetu.
Idadi ya watanzania wasomi na watumishi wa umma ni asilimia chache sana, ila wananchi wenye elimu ya msingi na sekondari ndo walio wengi.
Na group hili la pili ndio mfano mzuri kwetu vijana.

Lazima tuache kujitetea tu, wako wazazi wetu hawajaenda shule ktk maisha yao ya kupigana wamezeeka na waliweza hata kutuachia nyumba yenye vyumba vitatu na kutusomesha mpaka tumefka elimu ya juu.
Kwa uzoefu huu tunaamini juhudi na maarifa uvuta mafanikio.

Tatizo la vijana wasomi hasa tuliofika vyuo vikuu, mfumo wa elimu umetufanya kuwa watumwa ki fikra,
Unatufundusha kujiona sisi km watu special ambao tunapaswa kufanya kazi za namna fulsni hivi. Uku tukijiwekea tabaka hilo na ndg zetu ambao tunasema hawakwenda shule.

Hii changamoto kubwa kuikabiri kwani mfumo umetumia miaka kama kumi -20. Kukuprogram kuwa tegemezi.

Hivyo lazima mthubutu kuvua hiyo mantal slave thru changing your attitude.

Kisha jitambueni,
Muwe wavumilivu
Muwe na bidiii
Muwe na nidhamu
Maarifa mliyoyapata yawe mtaji wa kuyakabiri mazingira.

Aksanthe kwa kuelewa.
kweli mkuu.mitaala inakuandaa uwe boss nafasi serikalini ni chache lakini sector binafsi ikiwekewa mazingira mazuri itachukua wahitimu wengi kuliko kumsomesha mtu humpi ajira.umemkopesha hela hata deni anashindwa kulipa.mzunguko wa kurudisha hela na kusomesha watu wengine utatoka wapi? tukubali kuwa wajibu wa serikali ni kutengeneza ajira au mazingira rafiki kwa mhitimu kutumia taaluma yake.kwasasa bado hali ni mbaya.huwezi ukabadili mtizamo wa mtu kwa mwaka mmoja uliyemjengea kwa miaka 20
 
yes , wao wanataka vjana tu wajiajiri, kusema rahisi kuliko kutenda
kweli kabisa.sawasawa na kuwatuma vijana vitani wakati wazee wamekaa nyuma na kula mema ya nchi. enzi zao.wakisomeshwa bure na Nyerere! hawana mikopo ya kulipa.wameharibu uchumi kwa kuiba matokeo tunakopeshwa ili tusome mkimaliza ujitafutie kazi kwa kujiajiri.ulipe na mkopo na riba.
 
Mitaji wanayo, nyumba walishajenga, mashamba wanayo, gari wanazo. Ofisini wanang'ang'ania nini?
wanabaki kuongea.kwa kebehi.kuwa wahitimu hawajiongezi!.kumbe wazee wamekalia fursa zote.wanaboa sana.
 
Back
Top Bottom