Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,470
- 5,477
Najua kuna ambao watashangaa ninachotaka kusema hapa.
Namzungumzia mtu anayeitwa Rugemalira wa Escrow. Huyu ni mmoja kati ya matajiri wa nchi hii ambao historia ya utajiri wao iko wazi. Ni mtu ambaye pamoja na serikali kutaka kumfanya aonekane ni muhalifu, uwezo na ushawishi wake katika kufikia malengo yake ni wa kuigwa mfano.
Rugemalira kwa sasa amekuwa branded kama tapeli, mwizi na muhalifu jambo ambalo binafsi naweza sema kwamba ni kweli kwa mujibu wa mfumo wetu wa uchumi ambao ili mtu fanikiwe anatakiwa asubiri mshahara, aibe, au astaafu ndiyo apige hatua.
Huyu mzee Ruge alifanya jambo la kipekee katika historia ya nchi hii. Jambo hili nina hakika wafanyabiashara wengi wanalifanya. Jambo lenyewe ni la kutafuta fursa; kutafuta wenye mtaji, kuunganisha dili, kuisimamia na kuhakikisha inafanikiwa na kisha kuchuma faida na kuendelea na maisha.
Yeye aliona fursa ya kufua umeme, akatafuta wawekezaji, akatafauta wakopeshaji, akafanya kazi kama alivyotakiwa. Kulipotokea sintofahamu akafuata mfumo wetu wa kisheria mpaka akapatiwa haki yake. Ndiyo inawezekana kuna ujanja ujanja katika kuhakikisha anafanikiwa lakini tukubali kwamba huwezi kufanikiwa bila kuwa mjanja mjanja.
Ninawaombea vijana wote mjifunze kitu kizuri kwa huyu mzee mpambanaji ambaye pamoja na serikali kumuweka lupango bado focus yake iko kwenye pesa zake ambazo bado anadai huko duniani.
Wito wangu kwa Magufuli na serikali yake: Achaneni na huyu mzee maana hakuna hela aliyokula ambayo hakufanyia kazi. Kamata hawa ambao wanakula pesa za umma bila kibali cha Bunge kama kina..., na wale ambao utajiri wao ni wa mashaka kama kina....