Natamani Watanzania wayasuse makampuni ambayo Rostam na mafisadi wenzake wana hisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani Watanzania wayasuse makampuni ambayo Rostam na mafisadi wenzake wana hisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by theophilius, Mar 12, 2011.

 1. theophilius

  theophilius Senior Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 151
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa nini Watanzania wanaochukia rasilimali za taifa kuibwa na mafisadi tusichukue hatua dhidi ya mafisadi, angalau wale wanaojulikana. Tunaweza kuanza kwa kususia bidhaa na huduma za makampuni ambayo ama rostamu na mafisadi wenzake wanamiliki (au kuwa na hisa) ambayo kwa kadri habari zinavyoendelea kujipambanua, rasilimali (wafanyakazi/magari/fedha) za makampuni hayo zinatumika katika vitendo vya kifisadi.

  Ikiwa watanzania wataonesha chuki dhidi ya Vodacom, New Habari na mengine wanahisa wasafi wengine wa makampuni hayo watafukuza mafisadi kutoka makampuni hayo vinginevyo yafe kwa kukosa biashara hapa nchini.

  Vinginevyo, mafisadi hawa wataendelea kupeta wakichota huku na huku kwani hakuna anayeweza kuwapeleka mbele ya sheria maana wameitia serikali mfukoni, ni budi sasa 'Nguvu ya Umma' itumike na kwa hakika ikifikia mahali ikatumika watakimbia wenyewe nchi na litakuwa funzo kwa wengine!
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Aisee, hii ni idea nzuri sana. Naunga mkono kwa asilimia 100. Tuanze kwa kutonunua magazeti ya fisadi rostam.
   
 3. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Magazeti ya kipuuzi kama Mtanzania, Dimba na Rai niliacha kusoma zamani sana.
   
Loading...