Natamani Tanzania tufike hapa; Urusi kujenga viwanda viwili vya nishati ya nyuklia Nigeria


MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Messages
772
Likes
476
Points
80
MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2017
772 476 80
_98568201_c2c5fad2-f073-45e3-ad05-2f989150222e.jpg


Urusi imetia saini mkataba wa kujenga viwanda viwili vya nishati ya nyuklia nchini Nigeria huku taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika likiweka mikakati ya kumaliza matatizo yake ya umeme.

Kampuni inayomilikiwa nchini Urusi Rosatom itajenga kituo kimoja kusini na chengine katikati kulingana na duru katika tume ya nishati nchini Nigeria.

Thamani ya makubaliano hayo haijulikani, ijapokuwa ripoti zinasema kuwa huenda inakaribia $20bn.

Ni mojawapo ya viwanda vya kinyuklia ambavyo kampuni hiyo ya Urusi imekuwa ikilenga kujenga barani Afrika.

Kampuni hiyo pia imeanza mazungumzo ya kujenga vituo kama hivyo nchini Ghana na Afrika Kusini.

Makubaliano ya wali ya kampuni hiyo kujenga kituo kama hicho nchini Afrika Kusini yalikataliwa na mahakama ya taifa hilo mapema mwaka huu.

Makubaliano hayo nchini Nigeria yaliafikiwa baada ya muda mrefu wa majadiliano huku mataifa hayo mawili yakitia saini makubaliano ya kwanza ya ushirikiano wa kinyuklia kati ya serikali mbili 2009.

Nigeria inatumai kiwanda hicho ambacho opersheni zake zitaendeshwa na Rosatom kabla kukabidhiwa serikali ya Nigeria kitasaidia kukabiliana na uhaba wa umeme wa taifa hilo.

Kulingana na takwimu za benki ya dunia, zaidi ya asilimia 40 ya taifa hilo halikuwa na umeme 2014.

Nigeria ndio taifa lenye utajiri mkubwa wa mafuta barani Afrika lakini utajiri wake wa mafuta umetumiwa vibaya kwa miaka mingi.

Ufisadi umeliwacha taifa hilo bila fedha na kutoa kiwango kidogo cha umeme ambacho raia milioni 180 wa taifa hilo wamekuwa wakihitaji.

Ujenzi wa kiwanda hicho kipya unatarajiwa kuanza katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
 
R

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
15,270
Likes
20,280
Points
280
Age
21
R

Retired

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2016
15,270 20,280 280
Ulaya ya magharibi wanataka ku phaseout mambo ya ishati ya nuclear, sisi ngozi nyeusi tunakimbilia huko
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
29,070
Likes
75,309
Points
280
Age
18
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
29,070 75,309 280
Tulio hai sasa hivi tutarejea kwa muumba wetu hayo tunayoyasema na kutaka yafanyike itakuwa bado ndoto
 
Rodwell mTZ

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2012
Messages
320
Likes
141
Points
60
Rodwell mTZ

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2012
320 141 60
Kwa nchi yetu ya Tanzania tuna vyanzo vingi vya umeme vya asili ambavyo kama vitatumika kama ilivyopangwa tutakuwa na umeme wa kutosha na ziada itakuwepo,kwa hivyo basi havna uhitaji na hayo manyuklia sababu yanahatari sana,rejea ajali ya kinu cha nyuklia cha chenobil urusi mwaka 1986 na ile ya japan miaka michache iliyopita,ni majanga hiyo miradi ya umeme wa nyuklia haifai hata kuifikiria.
 

Forum statistics

Threads 1,237,390
Members 475,533
Posts 29,286,823