TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 4,974
- 15,310
Siku hizi simu zote za ghali utakuta zina material ya kioo nyuma (battery cover). Hii ni kwa simu zote kuanzia iphone 8, samsung s8 kwenda mbele zote mfuniko wa nyuma ni kioo. Kwangu mimi naona kuweka kioo nyuma ya simu ni wazo la hovyo kwa sababu zifuatazo;
1. Kioo kinateleza. Simu yenye kioo mbele na nyuma haishikiki, yaani mda wowote inaponyoka na ikianguka lazima ipasuke ama kioo cha mbele au cha nyuma.
2. Kioo huvunjika na kukibadilisha ni gharama. Pamoja na kudai wanatumia sijui gorilla glass lakini binafsi sijawahi kuangusha simu ikaacha kupasuka.
3. Kioo hushika uchafu kirahisi sana hasa fingerprint na vumbi.
Mimi nafikiri hawa watengenezaji wa simu lengo lao ni simu ipasuke ili ununue nyingine sijaona kama wana hoja yoyote ya msingi, hasa ukizingatia miaka ya nyuma tulikua na simu za plastic na aluminium na hazikua na shida yoyote.
Mwenye hoja kinzani namkaribisha anitoe tongotongo.