JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Salamu wanajamvi!
Awali ya yote ningependa kutoa salamu na pongezi zangu za dhati kabisa kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ndugu JPM.Ni matumaini yangu kuwa akiendelea hivi bila sha Historia itamuweka kundi moja na viongozi mashuhuri walio pata kutokea dunia hii.pamoja na mambo yote mazuri uliyo ifanyia Nchi yetu mpaka sasa, natamani sana ungefanya na haya yafuatayo.
Mosi, bila kujali itikadi yako ya kisiasa utakuwa umeitendea haki sana Nchi yetu na Demokrasia kwa ujumla kama utaamuru uchunguzi wa kina wa watu walio muua ALFONCE MAWAZO kufanyika na wote watakao bainika wafikishwe mbele ya sheria.imefika wakati sasa jamii ijifunze kufanya siasa za kistaarabu na kuvumilia lakini tukihakikisha amani inatamalaki.Nakuombea kwa Mungu upate nguvu, ujasiri na hekima na uliamuru jeshi la polisi wakamilishe upelelezi haraka ili haki itendeke.
Pili, juzijuzi tumemsikia kiongozi mmoja mwandamizi akiahirisha uchaguzi wa meya wa jiji la Dar huku akitoa sababu kuwa kuna zuio la kimahakama, jambo ambalo mahakama ilikanusha kuwa haikutoa zuio kama hilo.Mimi nilitegemea mahakama ingetoa hati ya kumtaka kiongozi huyu afike mbele ya hakimu atoe maelezo kuthibitisha kupokea zuio la kimahakama vinginevyo sheria ifuate mkondo wake. Uongo ni jambo moja baya sana katika jamii.
Kwakuwa mahakama imeamua kukaa kimya nakuomba uamuru uchunguzi ufanyike ili kama kuna hila zozote ziwe za kisiasa au vyovyote vile ukweli ujulikane ili Taifa lisimame katika haki na katika njia ya mabadiliko ya kweli.