Uchaguzi wa Kenya umekwisha,lakini mshindi wa kiti Cha urais aliyetangazwa na tume huru ya uchaguzi ,ya Kenya RUTO bado hajazibitishwa kwa kuwa mpinzani wake wa kitu hicho ,Raila Odinga , alikwenda mahakamani kupinga matokeo yao.Mahakama ya upeo itato majibu ya rufaa ya mzee Odinga siku ya Jumatatu ijayo.Hakika nchi ya Kenya imeonyesha DEMOKRASIA ya Hali ya juu Sana , ambayo unatakiwa iigwe na nchi za kiafrika.Kenya wamepiga hatua kubwa sana ya DEMOKRASIA.Hii inaonyesha kwamba wasomi wa Kenya wamesoma vizuri Sana na wakaelimika . Wasomi wa Kenya hawababaishi kabisa.Mvutano uliotokea mahakamani unadhibitisha usomi wa hali ya juu,na upeo mkubwa sana wa uelewa wa Mambo wa wasomi wa Kenya.Hili ni fundisho kubwa kwa nchi yetu ya Tanzania ambayo ni kubwa mara mbili ya Kenya ,kuanza kujifunza kutoka kwa majirani zetu .Ni muda muafaka Sasa tusipate washindi wa urais na wabunge wa Chupli Chupli.Tupate washindi halali ambao wataisaidia nchi yetu ,kusonga mbele.Itafurahisha sana kuona wasomi wetu ,wa Tanzania wa sheria wakibishana mahakamani ,na kuonyesha weledi wao wa hali ya juu.Huo mtindo wa viongozi kupatikana kwa mbinu mbali mbali ,unasababisha tuwe na viongozi wasio na weledi.Vyama vya upinzani vya Tanzania pia ni muda muafaka kuanza kujipanga vizuri ili tuwe na vyama vya kitaifa visiwe vya watu binafsi.Tusiwe na vyama vya watu binafsi ,kama tunavyoviona kwa Sasa .Vyama hivi binafsi vinasababisha CCM pia iwe na nguvu ya kuiba kura na kukataa kutoka madarakani.Tukiwa na vyama vya umma ,hata wagombea wetu wataonekana wenye upinzani wa kweli.Mungu ibariki Tanzania.