Natamani sana kupata hata mtoto mmoja tu

kitororondo

JF-Expert Member
Jan 17, 2018
598
698
Imeshapita miaka kadhaa nyuma ila kuna post nimeisoma hapa ikanikumbusha maumivu fulani ya moyo niliyowahi kupata hapo nyuma

Miaka ya nyuma nikiwa na rafiki zangu kama wa nne tumeshibana gafla siku zinavyoenda wenzangu wakawa wamebahatika kupata watoto wa wenzi wao, aise ilinipa kiu ya mimi kupata mtoto kwakweli nilijitahidi kwa wanawake wengi na wapo pia waliotamani kunizalia ila mambo yaka hayafanikiwi.

Mwisho nikaona huwenda ninamatatizo mbona wanawake hawa hawa nikiachana nao tu wakiingia kwenye mahusiano mengine wameshapata mimba kwakweli iliniumiza japo sikusema kwa mtu wala kumshirikisha mtu,

Na nilishaachwa na wanawake zaidi ya watatu ambao wenyewe shida yao ilikuwa mtoto walipotega na kutega wakaambulia patupu mwisho walivunja mahusiano(inauma acha tu)na nadhani hii ndio ilipelekea kuingia kwenye mahusiano na watu wazima kwakuwa wao hawana mpango wa kuzaa tenad

Basi bhana wakati nimekata tamaa kabisa nikakutana na bint mmoja tukawa kwenye mahusiano ndani ya mwezi tu akaniambia anahisi ni mjamzito moyo ulishtuka nikavuta kumbu kumbu za wanawake wa nyuma nafsi ikaniambia brother hapa unaibiwa,kusema ukweli nilikataa ile mimba,

Baada ya miezi minne ya kutafakari nikaona hata kama na zingiziwa bora kama kweli sinauwezo wa kuzalisha si heri nikubali kuficha aibu yangu

Bahati nzuri yule binti alnitafuta tena huku anauzuni kuwa anahangaika peke ake kulea mimba na kwao anaonekana ni malaya kubeba mimba isiyo na baba,

Basi nikamwambia usijali shetani alinipitia nikajirudi nikamtunza vizuri wazazi wangu wakaenda kwao basi majadiliano yakafika kuwa binti akishazaa tuanze maandalizi ya ndoa
Mungu mwema binti akajifungua salama ila mtoto hakuwa ridhiki baada ya siku tatu akafariki japo alizaliwa akiwa na afya njema sijui kilitokea nini?

Haikuniuma wala sikujali sana sijui kwakuwa nilikuwa mbali ila nikarudi kumfariji mke japo nilikuta wameshazika baada ya week nikarudi tena dar kuendelea na majukumu na pia kuanza maandalizi ya ndoa

Baada ya miezi sita binti akaanza usumbufu bebi nimekumic rudi japo ukae hata week yaani aling'ang'ania nirudi mpaka nikashangaa

Kwakuwa nilikuwa busy nikakaza baada ya mwezi ule usumbufu ukakata nikasema afadhari kanielewa nikavuta miezi mingine miwili ndio nikapanga safari ya kurudi
Ila ajabu nilipomtaarifu narudi hakuwa amepokea taarifa zile kwa furaha ila nikapotezea nikajua ni hasira za kutorudi kwa wakati

Duh! Kufika home nakuta binti anakitumbo kikubwa namuliza imekuwaje analia tu nakuomba msamaha kuwa ni bahati mbaya

Sikumaindi sana kwakuwa hata mi nilikokuwa nilimsaliti tena kwa kiwango cha juu kabisa nikamwambia usijali kwani ujauzito unamiezi mingapi akasema minne,
Sindio akiri ikanikaa sawa kuwa miezi mitatu nyuma ndio alikuwa analazimisha nirudi kwahiyo kama ningerudi tu ningebambikiwa mimba

Nikatafakari nikaona huu ujinga nikamuomba ajiandae nimrudishe kwao japo aligoma ila ikabidi niwe mkali
Basi nikamrudisha kwao nikawambia binti yenu kanishinda japo sikuwaambia alichofanya nikasepa mengine nikawajibu atawaeleza mwenyewe,

Ajabu mtoto kazaliwa kampa jina ambalo Baba yangu alipendekeza nikiwa na mtoto wakiume nimuite Baraka yeye kampa jina mtoto wake mbaya na jina la ukoo ametumia langu kuanzia kwenye kadi

Nipopata taarifa hizo nikamtafuta kwa simu akasema hakujua aandikishe jina gani maana hata aliyempa mimba hamjui walizoeana gafla wala hajui atampatia wapi ajue jina lake
Yaani nikaamua kukausha mpaka leo na sababu ya kukaa kimya mpaka leo sijabahatika kupata mtoto hivyo naogopa kupaniki afu mwisho nikajikuta namuhitaji huyo mtoto japo sio wangu ila anatumia majina yangu ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akilinjema, Bado sijaoa na huyo mwana mke yupo Iringa na mimi nipo Dar kwa saa,,,na nimeokoka tarehe25 mwezi uliopita baada ya kuudhuria mkesha wa cristmass Mchungaji alisema atakae kubali kuruhusu Yesu azaliwe moyoni mwake atambadilisha maisha yake na kufuta historia mbaya ya maisha ya nyuma atamfanya kuwa mpya nikaona isiwe kesi wacha nimkubali tu Huyu Yesu huwenda atatenda na kwangu pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado sijaoa na huyo mwana mke yupo Iringa na mimi nipo Dar kwa saa,,,na nimeokoka tarehe25 mwezi uliopita baada ya kuudhuria mkesha wa cristmass Mchungaji alisema atakae kubali kuruhusu Yesu azaliwe moyoni mwake atambadilisha maisha yake na kufuta historia mbaya ya maisha ya nyuma atamfanya kuwa mpya nikaona isiwe kesi wacha nimkubali tu Huyu Yesu huwenda atatenda na kwangu pia

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ndipo ulipopotea njia. Umeamua kumwamini mtu badala ya Mungu
 
Mtu anayekuambia kuwa ukachukue vipimo nadhani hakutakii mema. Wewe chukua mkeo ila mkalishe kikao kuwa, kama ana haja ya kuongeza mtoto basi akuambie ili umtafutie nduguyo wa karibu ili hata ukimrithisha mali ziwe ziko kwenye ukoo. Usitake aende mwenyewe huko na huko atakuletea jambazi.
Hakuna mtoto mwenye uhakika na babake. Mama ndo anaujua ubini wako weye.
 
Mtu anayekuambia kuwa ukachukue vipimo nadhani hakutakii mema. Wewe chukua mkeo ila mkalishe kikao kuwa, kama ana haja ya kuongeza mtoto basi akuambie ili umtafutie nduguyo wa karibu ili hata ukimrithisha mali ziwe ziko kwenye ukoo. Usitake aende mwenyewe huko na huko atakuletea jambazi.
Hakuna mtoto mwenye uhakika na babake. Mama ndo anaujua ubini wako weye.
Ushauri mzuri ila unahitaji moyo kuufata kwanza sitawahi kuwambia kama nnatatizo la uzazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom