Natamani sana kila member humu wa JamiiForums atumie jina na pamoja na picha yake halisi

zink

JF-Expert Member
Sep 18, 2021
717
1,000
Leo nimetafakari sana juu ya hili jambo, kwa maana wanachama wa humu wa JF wakitumia majina pamoja na picha zao halisi kutaleta faida zifuatazo:

1. Kutaongeza kuheshimiana, endapo kila member humu atatumia jina pamoja na picha yake halisi kutapelekea kuheshimiana kwa kuwa member wengi humu wanachukuliana poa kwa kuwa ID sio halisi kwahiyo unaweza kuta katoto ka mwaka 2000 kanamtimulia vumbi mtu mzima tena wa miaka 70 huko.

2. Kutapunguza idadi ya watu kutumia ID zaidi ya moja , kama mjuavyo wengi humu wana ID's hata 10 kwa ajiri ya maslai yao binafsi hivyo kama mtu ili afungue account lazima atumie jina pamoja na picha yake original itakua ngumu mtu huyo kuwa na ID's zaid ya moja.

3.Kutarahisisha upanikanaji wa mchumba, mpenzi humu jukwaani, Hii naisema kwa kuwa wanawake wengi humu jukwaani wanachukulia sana poa wanaume wa humu jukwaani kwa kuwa awajawaona wanavyofanania, hivyo kama members humu wakitumia utambulisho wao halisi itakua ni rahisi kumpata mchumba tena ata mke humu jukwaani.

4. Kutapunguza utapeli, wengi humu wanatumia ID ambazo hazima taarifa za ukweli kwa ajiri ya kufanya utapeli hivyo endapo kama members humu watatumia majina na picha zao itakua rahisi ata kuwapata kwani picha na jina ni halisi.

Ni hayo tu wakuu kama kuna sehemu nimesahau kugusia unaweza kuongezea nyama

NAWASILISHA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom