Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
Natamani Rais Magufuli kama mwenyekiti wa Chama Tawala Tanzania afuatilie na kuyachukua haya yanayotokea Israel katika uchaguzi mkuu wa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo.
Fikiria kwa nchi kama Israel ambayo imezungukwa na unyeti wa kila kitu kuanzia nchi yenyewe, siasa na utawala, ulinzi na usalama, na pia jicho kali la mahasimu wake. Lakini linapokuja suala la siasa za vyama nchi husimama kama nchi ya kidemokrasia inayoruhusu vyama vyote kufanya siasa bila vyombo vya dola kuingilia vyama pinzania kama ilivyo Tanzania ambayo ni nchi masikini kuanzia kichwani hadi miguuni.
Kinachovutia Uchaguzi huu wa Israel na kinachonisukuma nitamani Rais wangu mpendwa John Pombe Magufuli afuatilie uchaguzi huu, ni aina ya Wagombea kwa upande mmoja Jasusi Benjamin Netanyahu wa Chama cha Likud toka katika kikosi cha siri cha shirika la Ujasusi la nchi hiyo cha MOSSAD kiitwacho Kidon, na Jeneral wa Kijeshi kutoka katika kikosi imara cha jeshi la Israel kiitwacho Unit 269 – Sayeret Matkal bwanana Benny Gantz wa chama cha Nixes.
Licha ya Waziri Mkuu Benjamini Netanyahu kwamba angekuwa na nguvu zote za kufifisha ndoto za Jenerali huyu wa kijeshi kutumia haki ya kikatiba ya nchi hiyo kugombea urais lakini hakuthubutu kumtisha wala kumwingilia wala kumtaka ahamie chama chake kwahiyari ama kwa nguvu, Benny Gantz amekuwa ni mwenye nguvu na ushawishi kwa kiwango cha juu na kutishia uimara wa Netanyahu.
Uchaguzi umepita bila kupata mshindi jambo linalomlazimu Netanyahu kuunda serikali ya mseto, na kinachofurahisha nikuwa wakati wajumbe wa chama cha Nixes wakielekea kwenye kikao cha majadiliano leo, Netanyahu akapinga kuunda serikali ya mseto, huku mwanasheria wa Serikali akiwasilisha mahakamani kesi ya kula nyama na kukosa uaminifu, mashitaka haya yanamlenga Netanyahu kupokea rushwa. Na kwakiasi kikubwa yanaweza kumbomoa ikiwa uchaguzi utarudiwa.
Navuta picha uhuru na uimara wa mihimili na taasisi za kiserikali ulipo Israel ungekuwa uko Tanzania, Fikiria idadi ya misururu ya wagombea wa CCM ambao wangechukua fomu wakiongozwa na Bernard Membe 2020, Fikiria vyama vya upinzani vingekuwa na uwanja sawa wakufanya siasa bila kuingiliwa na chama tawala kupitia dola, nchi ingekuwa mbali sana.