Natamani niwe mtu fulani hivi fair saana katika maisha yangu

KimpaGhasha

Member
Jun 21, 2020
39
125
Habari zenu wakuu,

Aisee bila kupoteza muda, kuna tabia fulani hivi jamani natamani na naomba Mungu siku zote niwe nayo ila naona kama inachelewa saana kwangu kunifikia.

Yaani natamani nisiwe na wivu katika maisha yangu, nisiwe na kinyongo hata kidogo juu ya mwingine, niwe na huruma saana juu viumbe, niwe na tabia yakujitoa juu ya shida ya mtu mwingine, nikiwa na kidogo nigawane na yule ambae hana kabisa.

Yani hivi vitu ninavyo ila ni kwakiasi kidogo saana naona haitoshi au haijafika pale ninapohitaji mimi.

Hii tabia nilikuwa nayo tangia utotoni ila ilipotea nahisi nilivofika miaka kam 13 sijajua kilitokea nini mpaka ikapotea ila nahisi kutengan kwa wazazi wangu kulichangia maana baada ya hapo niliishi namama mlezi kwahiyo kulikuwa na baadhi ya vitu kwangu havikuwa Sawa.

Nakumbuka mi ilikuwa nikikuta mtu kalala halafu anaumwa nilikuwa sitoki pale alipolala mpaka nifuatwe nyumbani au nisindikizwe nyumbani.

Pia nilikuwa nikikuta mtu anapigwa au wanapigana moyo wangu unaniuma kama napigwa mimi.

Pia nikiwa na kitu kidogo na niko na wenzangu sili mpaka wote wamepata

Ila vyote vilipotea yaani sina navyo kabisaa ila napenda niwe navyo aisee.

Kama kuna mtu anaweza kunipa mbinu tabia ikajirudia anambie au ndo baasi tena siweziiii?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom