Natamani ningekua nimezaliwa miaka 80 iliyopita!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani ningekua nimezaliwa miaka 80 iliyopita!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Aug 17, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Natoka kazini nafika nyumbani usiku saa 3,mke wangu nae ndo anafika kutoka kazini,nae amechoka,namwambia tukaoge ananiambia nitangulie kwani amechoka.Naenda kuoga narudi HG anaweka chakula mezani,namuangaza mke wangu namkuta amepitiwa na usingizi kwenye kiti sababu za purukushani za kazini,namwamsha kisha wote tunajongea mezani,chakula sio kitam kama kile anachopika mke wangu,siku hizi hapiki,anakua kazini.Tunaingia kulala nimechoka nilitarajia mke wangu anipoze na mahangaiko ya kutwa nzima kumbe nae anahitaji wa kumpoza,hakuna wa kumpoza mwenzake wote usingizi unatupitia,tunalala kama tumezirai,hakuna muda wa kujadiliana kuhusu familia na maisha yetu.Unyumba tunapeana kimazoea tu,hakuna zile hisia na ham kama zamani.Kukicha watoto nao wanalalamika hatuna muda wa kukaa nao,hg hajui kuwalea kama mama yao.Watoto wanatuona kama wapita njia tu.Ee Mungu wanangu hawa watalelewaje?Najikuta nayatamani maisha niliyokulia mimi,natamani ningekuwa na umri wa baba yangu!! . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Nyote mnaochangia hebu changieni kwa kushauri kulingana na changamoto hizi zinazotukabili,mtoa mada anaweza kuwa amewawakilisha wenye maisha yenye changamoto hiyo,sio lazima ahusike!
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Pole sana...maisha ya sasa hasa kwa wanaoishi jiji la Dar lenye foleni za kufa mtu yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Hivi karibuni nilipata nafasi ya kuzungumza na marafiki wanaofanya kazi sehemu mbali mbali jijini kuhusu wanachokifanya ili kuwahi kazini.

  Wengine wanadai kuamka saa 10 za alfajiri hupata kifungua kinywa ndani ya gari na wakimaliza kazi hawaingii majumbani mwao mpaka saa mbili za usiku au zaidi. Sasa saa ngapi utakuwa na nafasi ya kukaa na watoto, mume/mke na ilhali inabidi ukalale ili siku inayofuata uweze kuamka zile saa zako za saa 10 ya alfajiri.


   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Kujipaga na kuweka vipaumbele tu

  Kama satsifaction yako iko kwenye pesa basi tafuta pesa
  kama iko kwenye familia basi tenga muda wa familia.

  Wee ni introvert au extrovert??
   
 4. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kuwa introvert au extrovert inasaidia eh?
  Kwani mm unanijudge vipi kati ya hizo 2options? siwezi kuwa between?
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280

  hamieni mbagala, huko kimara, mbezi, tegeta, kibamba, mbweni, boko, tabata, ukonga ndo kunawaponza........... mie natarajia kuhamia charambe soon sitaki shida......


   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Jiji limebadilika sana kiasi ambacho hata raha ya kuishi jijini kama ilivyokuwa miaka iliyopita imepotea kabisa. Sasa inyeshe na mvua hapo ndio unazidi kulichukia jiji.


   
 8. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mie huku nilipo,'Tandahimba' wala sitamani kuzaliwa miaka hiyo,unavyovikosa mimi ndio ninavyovipata!!asbh twatoka saa 0815,dakika 5 tumefika kazini,saa 1430 tunatoka kazini pia dakika 5 tuko hom!!twafurahia maisha,pole
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Mnafanya kazi gani?
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  inasaidia sana kujijua unaangukia wapi.

  Ili ujue jinsi ya kukabiliana na mazingira unayokuwa.

   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  unaamini kuwa mazingira unayoishi ndio yanadetermine fate nayo au fate yako iko mikononi mwako??


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,869
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  mmmmh hapo kwenye mvua ndo patamu hapo..... utatamani upae kwa ungo hadi kwako.....



   
 13. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kama unaishi Dar ni sawa..
  Ila ukienda mikoani unapata muda wa kukaa na familia yako mpaka basi..
  Wakati mwingine tusiache mihangaiko ya maisha itawale kila kitu..utakuja kukuta mwana si wako!
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  We acha tu halafu pamoja na mfumuko mkubwa wa population jijini (wahamiaji toka mikoani) bado Serikali hii dhaifu haioni umuhimu wa kuboresha drainage system badala ya hii ya sasa ambayo ni ya mwaka 47. Ikitokea mvua kubwa nyingine basi kutakuwa na maafa ya kutisha.

   
 15. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Introvert is a person characterized by concern primarily with his or her own thoughts and feelings..a shy person.
  Extrovert is a person concerned primarily with the physical and social environment...an outgoing, gregarious person.
  Ahsante Kongosho umenirudisha darasani..lol!
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Haya ndo matatizowa ya binadamu.Yaani kama tatizo haliko kwake hilo sio tatizo,u-mimi tu ndo mwingi!
   
 17. sakapal

  sakapal JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,824
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  this is very naked true, kama unafamilia aisee sio ya kuichezea atii, tenga muda uipe nafasi pesa inatafutwa hata ikiisha utatafuta nyingine, hata ukiibiwa vitu na mali utatafuta nyingine, ukipoteza familia kwa kutafuta pesa lolest yako aiseee!!!
   
 18. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Mie nipo job hadi sasa
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kuna rafiki yangu mmoja hapo dar yeye huamka saa kumi iliafike kazini saa moja na nusu na jioni hutoka saa moja na kufika saa nne au saa tano..huwa namshangaa sana maisha gani sasa hayo hapo mke watoto watapata mapenzi ya baba kweli mama atapata haki yake kweli
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  BADILI TABIA,hujaelewa kitu hapo.Changamoto sio kuja usiku pekee zipo nyingi kwenye familia na maisha ya leo.Nakumbuka mwaka 1998 nilipata ajira kwenye kampuni moja,mkurugenzi na mkewe ni kama sio mtu na mkewe,katika miaka yangu 7 ya kufanya kazi pale ni wiki moja tu walikaa pamoja!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...