SoC01 Natamani ningejua haya mapema ili kuepuka msongo katika mahusiano

Stories of Change - 2021 Competition

Fannjosh

Member
May 28, 2016
35
46
Utangulizi
Katika karne ya sasa, watu wengi wamekumbwa na misongo ya mawazo kutokana na hali tofauti tofauti wanazokutana nazo katika mahusiano. Baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana na kushindwa kudhibiti kiasi cha msongo. Wengine wapepoteza ndoto zao, familiya, kazi, masomo na hata kudhoofika kiafya kwa kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya kwasababu ya kuzidiwa na msongo wa mahusiano.

Katika Makala hii, tutaangalia ni nini ufanye ili kuepuka msongo unaotokana na mahusiano.

  • Kama umpendaye akiondoka maishani mwako, tambua yeye si “ALFA NA OMEGA”.
Maneno “ALFA NA OMEGA” hutumika kuelezea sifa za Mungu ikiwa ni pamoja na “Aliyekuwepo, Aliyeko na Atakayekuwepo”.

Hakuna mwanadamu wala kiumbe chochote chenye sifa hii isipokuwa Mungu peke yake, yaani “kutokuwa na mwanzo wala mwisho”. Ikiwa wewe mwenyewe una mwanzo na mwisho wako, kwanini ulie kwasababu ya mapenzi ambayo wewe mwenyewe umeyaanzisha? Kwanini ujiue kwasababu ya mtoto wa mtu ambaye yeye mwenyewe ana mwanzo na mwisho wake?

Unaweza ukalia sana na kuona giza la mapenzi kwenye maisha yako endapo yule uliyempenda, kumjali na kujitoa kwake akaamua kuachana na wewe katika wakati usiotarajia. Hali hii isikupe shida kabisa. Ni kweli inauma, lakini lazima siku zote uruhusu akili itawale hisia ili ufanye maamuzi sahihi katika maisha yako.

Ikiwa ataondoka kwenye maisha yako, basi tambua haikuwa riziki yako, hivyo mshukuru Mungu kwa kuruhusu aondoke kwamaana riziki yako iko njiani na nzuri Zaidi kuliko aliyeondoka.

Ukitambua uliyenaye katika mahusiano si “ALFA NA OMEGA”, basi hutopoteza hisia zako kulia mwezi mzima kwasababu yake, hutopoteza uhai wako kwa kunywa sumu au kujinyonga kwasababu yake, wala hutoacha masomo, kazi au kuua ndoto zako kwasababu yake, na msongo wa mawazo hautakusumbua kamwe.

  • Epuka kudai Risiti kwa mwenzi wako.
Watu wengi wapo katika mahusiano ila wengi wanapenda kutendewa vizuri na wapenzi wao huku wao wakitenda kwa kiwango kidogo. Mfano, unaponunua zawadi kwaajili ya mwenzi wako, haijalishi wewe ni mwanaume au mwanamke, basi toa zawadi hiyo kwakuwa unampenda mwenzi wako, usitoe ili kutegemea kitu Fulani kutoka kwake, na pia usihesabu kila unachokitoa kwake.

Moja kati ya kanuni za upendo, ni kutokuhesabu mabaya au kutohesabu kila ulitendalo kwa mwenzi wako. Ikiwa utahesabu kila unachokitoa kwake, kila chema unachofanya kwake, basi yeye asipofanya kama wewe unavyofanya, lazima utaumia na utaanza kupata msongo ambao hauna ulazima.

Ile kanuni ya “Ukitoa dai risiti” usiishi nayo kwenye mahusiano. Ukitumia hiyo kanuni, basi jua utapata msongo utakaoumiza afya yako. Furahia Zaidi pale unapotoa kwa mwenzi wako kuliko pale unapopokea kutoka kwake, ili hata kama wewe ukitoa vyote kwaajili yake na yeye asikupe chochote, bado furaha yako itakuwa pale pale.

  • Epuka kuwa omba omba wa mapenzi.
Hapa nina maanisha kwamba, kuna mtu akipenda, yeye analazimisha hisia za yule ampendaye zifanane na za kwake, matokeo yake anaanza kuomba apendwe, anaomba akumbukwe, anaomba atumiwe ujumbe (SMS) mara kwa mara NK.

Mfano. Unatuma ujumbe kwa mwenzi wako “Nimekumisi”, kisha yeye anajibu “Asante”, baada ya hapo unauliza “Wewe hujanimisi?”

Hali kama hiyo itakupa msongo usio na sababu. Ili mtu akukumbuke lazima awe na upendo kwako, na pia wewe mwenyewe utende mambo ambayo yatamfanya mwenzi wako akukumbuke.

Ikiwa unamkumbuka mwenzi wako mara kwa mara, basi tambua kuna mambo anafanya kwako yanayopelekea hali kama hiyo kutokea. Jambo muhimu hapa ni wewe kujihoji na kubaini mambo ambayo ukifanya kwake, basi atakukumbuka na kuwa tayari kukutamkia maneno uyapendayo au kuwasiliana na wewe kwa namna itakayokufurahisha.

Ikitokea mwenzi wako haonyeshi upendo kama unavyotarajia, acha kuwa na msongo, tambua kuwa upendo ni hisia na hisia hazilazimishwi, ni hiyari ya moyo wa mtu. Vuta subira na ikitokea hisia zake haziongezeki kwako basi jua huyo si riziki yako. Acha kujawa na msongo, fanya mambo yanayokupa furaha maishani mwako.

  • Jifunze kusamehe na kusahau.
Kuna watu wanapokosewa huwa hawapendi kuondoa makwazo mioyoni mwao. Kitu cha kukumbuka hapa ni kwamba, yote uyabebayo moyoni mwako juu ya mtu Fulani, hayamdhuru yeye ila yanakudhuru wewe mwenyewe. Kama una hasira na umebeba mzigo wa kuua, basi jua hatakufa yeye ila utajiua mwenyewe.

Hivyo, ili kuepuka msongo katika maisha yako ya mahusiano, penda kusamehe hata kama mkosaji hajaomba msamaha. Hii itakusaidia kujiweka katika Afya njema na kumfanya mwenzi wako ajifunze kitu Fulani kwako ambacho kinaweza kumbadilisha hata yeye siku moja.

  • Ishi uhalisia wa maisha yako, usiigize maisha katika mahusiano.
Wengi wamekwama hapa na wakajikuta wanaangukia katika shimo la msongo. Katika mahusiano na maisha kwa ujumla, jifunze kuishi maisha yako na si maisha ya mtu mwingine.

Kuna watu wanaigiza tabia na mienendo wakihisi kwa kufanya hivyo watapendwa Zaidi. Hii si sawa, na ikiwa mwenzi wako atagundua kuwa unaishi maisha yasiyo yako, kuna uwezekano mkubwa mahusiano yenu yakawa hatarini kuvunjika na utaishia kubeba furushi la msongo.

Ikiwa wewe maisha yako ni “A” kisha ukaigiza kuwa mtu wa maisha “B” na ukaeleza hisia zako kwa mwanamke au mwanaume ambaye anapenda mtu aliye katika maisha “A”, basi ujue utamkosa bila shaka. Lakini ukibaki kuwa katika maisha yako ambayo ni “A” kuna uwezekano mkubwa sana ukampata yule umpendaye.

Jifunze kuwa “wewe mwenyewe” na si “wewe yule”.

Hitimisho

Mahusiano ni mazuri sana katika kujenga Familiya, jamii na hata kuleta Afya ya akili, mwili na roho. Ila mahusiano haya pia huweza kubomoa kila kitu maishani mwako endapo utashindwa kutambua namna nzuri ya kuyaishi.

Ushahuri wangu ni kwamba, tumia akili Zaidi katika mahusiano ili kuepuka kufanya maamuzi yasiyofaa. Pia ikiwa una mwamini Mungu, basi usiache kumshirikisha katika uchumba au ndoa yako maana yeye anaongoza kila kitu katika maisha yetu. Asante kwa kusoma hadi mwisho wa Makala hii.

Weka komenti yako hapo chini ikiwa una swali au una jambo la kushibisha Makala hii.
 
Nimeelewa
 
Back
Top Bottom