Natamani mhimili Wa Bunge ufutwe

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
713
1,136
Kila nikiwaza na kufikiria kwa kina nakosa kabisa kazi tangible za bunge ambazo mwananchi anaweza kufaidika nazo.
Kazi kuu za Bunge ni kutunga sheria eti na kuisimamia serikali. Lakini kwa uoni wangu sioni kama hizo kazi zinafanywa na bunge badala yake ni Bunge kupitisha miswada iliyoletwa na serikali Bungeni. Kwa ujuha wangu naona kazi ya kutunga sheria inafanywa na serikali kisha inapelekwa bungeni kama formality tu.
Lakini pia kwenye kuisimamia serikali hilo jambo haliko clear sana kwani wabunge hao hao hujigeuza kuwa mawaziri na hivyo kutetea maslahi ya serikali kuliko ya wananchi na wabunge. Ni mara ngapi tumeoma wabunge mawaziri wakitetea serikali huku wakijua kabisa serikali imekosea.
Hata hao wabunge wa majimbo wara zote kama si mara nyingi wanaitetea serikali kwenye hoja nyingi badala ya kuiadabisha.
Kitendo hicho kinaikosesha jamii imani ya kuwa bunge ni chombo chao cha uwakilishi.

Lakini pia serikali inatumia fedha nyingi sana kiwahudumia wabunge ambao kwangu ni non productive agency kwani wanapata mishahara na marupurupu mengi Sana bila kazi yao kueleweka. Ni kwa mantiki hiyo Zitto Kabwe alikataa kupokea posho ya vikao kwamba hakuna haja ya kulipwa kwa shughuli hiyo kwani ndio kazi yenyewe waliyo omba.

Lakini pia ubunge imekuwa kama kichochoro cha kupata fedha za haraka kama vile za kuuza madawa ya kulevya. Ni kutokana na utajiri huo wa haraka ma professor ma Dr, Wachungaji, Masheikh, walimu, mapolisi, wanasheria na kada nyingi wameamua kuacha shughuli zao na kukimbilia huko wakijua walicho kikosa kwa miaka 20 au 30 watakipata ndani ya mwaka mmoja . Si mmesikia mishahara na stahiki za mbunge kwa mwaka mmoja ni zaidi ya million 230 na hapo ni bila ya sitting allowance. Sasa piga hesabu hiyo mara wabunge karibia 370 hapo ndoo utaelewa hoja yangu.

Lakini pia ubunge imekuwa ni bidhaa adimi sana hivyo kuifanya kugombaniwa,kupiganiwa,kufitiniana,kurogana na kuchongeana. Kwa sasa maskini hana nafasi tena ya kuwa mwakilishi hata kama anajua kujenga hoja kama YESU KRISTO NA MTUME MUHHAMAD (SAW).
Kinachoangaliwa ni what you have in your pocket and not in your head. Maskini kuwa mbunge ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
Kutokana na hayo bora mhimili wa bunge ufutwe kwa mujibu wa sheria na katiba tubaki na mihimili ya Serikali na Mahakama tu. Itafanya kazi bila shaka yeyote. Hizo kazi bunge lilizokuwa likifanya zitahamishiwa kwenye hiyo mihimili mingine . Na kwa jinsi serikali ya awamu ya tano inavyo jinainisha kwenye kupunguza gharama za uendeshaji wa nchi hapo ni sehemu nyingine ya kupata mapato kwa ajili ya kuhudumia wanyonge wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachokiongea ni sahihi kwasababu tumebaki na wabunge wachache wanatetea wananchi kulinganisha na wanaotetea masilahi yao binafsi
 
Pesa za nchi hii zinapotea sehemu nyingi sana ,hizo za bungeni ndogo sana ukilinganisha na ufisadi unaofanywa na ccm ya wanyonge .Vipi kuhusu manunuzi ya wabunge na wapinzani hayapotezi pesa ,uchaguzi za marudio , ununuzi wa ndege feki Vipi haupotezi pesa ,uendeshaji wa shirika la ndege hasara tupu , gharama za wakubwa kwenda kufanya kazi Dodoma halafu kulala dar kula Siku hazipotezi pesa, na vyeo visivyo na tija kwa nchi RCs na DCs vyote ni kupotezea pesa za nchi .
 
Bunge dhaifu sana hili- Rubber stamp ya Serikali

Kwa nini Bunge likubali kufyeka FAO LA Kujitoa?

Bring back FAO LA KUJITOA

Ni aibu Serikali yenye madini, bandari na utalii Kupora pesa za wanyonge
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom