Natamani Mbunge wangu ajiuzulu!

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,596
5,787
Faida za mbunge wangu kuachana na siasa uchawara zama hizi.
1. Wilaya yangu itakuwa maarufu kama Igunga.
2. Vyombo vya habari vitahamia huko, wananchi wataweza kueleza shida zao, zikaandikwa, pia zikasomwa na wananchi wengine.
3. Viongozi wastaafu mf. Mkapa watafika wilayani, na kusifia maendeleo ya ccm.
4. Viongozi wa vyama vya siasa mf. Nape, Slaa, Mbowe watafika ndani ya wilaya yangu.
Kwakweli Wilaya Yangu itakuwa maarufu sana.
Serikali imeshindwa kutumia rasilimali zilizopo kuifanya iwe maarufu.
Nakuomba mbunge wangu ajiuzulu ili nasi tuwe maarufu.
 
4.Viongozi wa vyama vya siasa mf. Nape, Slaa, Mbowe watafika ndani ya wilaya yangu.

Mbona Maalim Seif hujamtaja inamaana yeye si kiongozi wa chama cha siasa! Au amewakilishwa na Mume ccm!
 
Unamaanisha mbunge wa jimbo gani?mbona ujamtaja unakuwa unaweka mafumbo tu au wewe ni muimba mashairi kama mzee yusuph.
 
Wazo zuri, kila mwezi ajiuzulu Mbunge mmoja kwa kila jimbo, kufika 2015 majmbo mengi yatakuwa yamefikiwa na kuwa maarufu!!!
 
Mi naomba mbunge wangu Cyril Chami ajiuzulu kutokana na kashfa ya kujimilikisha vitalu vyetu huko mufindi ili nao viongozi waje huku Moshi kutalii kwan tumewamis sana huku Moshi
 
Hivi wewe unajua utamu wa posho za vikao?

Hivi unajua mafao ya mbunge baada ya miaka mitano?

Hebu nyamaza tu ndugu yangu
 
Kwa hilo mkuu sahau kabisa uliwahi kuona wapi, kupe anajiudhuru kumnyonya ng'ombe?
 
Nadhani ndo stye nzuri ya kupata maendeleo haraka huko mikoani. Ikiwezekana wabunge wajitoe mhanga kwa ajili ya majimbo yao. Good views!!
 
Back
Top Bottom