josephwaara
JF-Expert Member
- Jun 18, 2016
- 304
- 637
Watu wa jamiiforums tunatishiana mno buana!
Majigambo mengi, dharau kedekede na ujuaji usio na kikomo.
Naona nyuzi kibao sasa za majivuno na mashambulizi kwa watu wengine au kundi fulani la watu.
Utakuta mdau wa JF anajisifu kwamba ana IQ kubwa, anamiliki fedha, mchacharikaji, ni mjanja wa kuvaa, anamiliki gari, alipata ufaulu wa juu darasani n.k huku akiunganisha hayo mambo na dis kwa wengine.
Hivi kweli ikitokea dharura identity zetu zikawa wazi ghafla wangapi tutasalia humu JF?
Hizi tabia za kupangiana maisha au kudharau wengine zina tija gani?
Una maisha mazuri sawa, una akili kubwa sawa mshukuru Mungu maana hukujiamlia ni neema na rehema zake tu, tumia hiyo akili yako kusaidia wengine au jamii yako.
Na wengi wanaofanya haya ni vijana, tena wanaojisifu wamesoma vyuo vyetu pendwa Udsm n.k na faculties za sayansi n.k wakati hatuoni hata impact ya elimu zao kwa taifa zaidi ya kuzunguka na laptops tu.