Natamani kusikia ni namna gani wasomi wetu watatumika katika matumizi sahihi ya rasilimali zetu

amigod

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
345
264
Habari za wakati huu kwenu JF,

Natamani kusikia Wagombea wetu wa nafasi ya Urais wakija na vipaumbele vya taifa hili kama ni jinsi gani watawatumia wasomi wetu kwenye gesi na mafuta Ziwa Rukwa, mafuta yaliyopo Kilwa. Tutawatumiaje wasomi wetu kuchimba ulanga Morogoro. Wajiolojia wapo, tutawatumiaje kuchimba shaba iliyopo Dodoma mpaka Kigoma.

Tutawatumiaje wataalaamu kuchimba chuma cha pua Songwe, chuma cha Liganga Njombe na Mchuchuma badala ya kununua mataluma sisi tuwauzie majirani mpira.

Arusha tuwe na tairi zetu badala ya kuagiza nje kila wakati tukiachia walivyopora mabeberu kama dhahabu, almasi, nk. Hivi vinawezekana kututoa hapa tulipo na kufungua wigo mpana wa ajira kwa taifa letu. Chama chochote kiseme hayo nitaunga mkono.
 
Back
Top Bottom