Natamani kusikia kauli ya jussa khs vurugu za zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani kusikia kauli ya jussa khs vurugu za zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sifongo, May 28, 2012.

 1. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,593
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Habari za majukumu wana JF naomba niseme kwamba ni mara yangu ya kwanza kupost topic humu barazani ila nimekuwa nikisoma sana post za wenzangu na kuelimika pamoja na kujua mengi juu ya hatma ya Nchi yetu mikononi mwa ccm na makuwadi wa siasa pamoja na baadhi ya wanasiasa uchwara kama Shibuda.....mniwie radhi kama sitaeleweka vizuri maana uandishi ni taaluma na hii sio taaluma yangu. Nimependa kusikia kauli ya Jussa kwa sababu kwa muda mrefu sana nimekuwa nikisoma kupitia magazeti au humu jf ama kumsikia katika redio akitoa matamko yenye utata khs muungano, nashukuru kwamba msimamo wake upo wazi maana hata kwenye baraza la wawakilishi msimamo wake unafahamika kuhusu muungano.
  Najua wapo viongozi wengi wa CCM, CUF na hata wa kijamii huko zanzibar wenye mitazamo kama ya Jussa japo wao hawajajiweka hdharani km mwenzao, ama kwa woga au unafiki na kutokuwa na misimamo na wanachokiamini.
  Natamani nisikie kauli ya Jussa maana makanisa yamechomwa moto zanzibar, makanisa na muungano vinahusiana nini, kwani hakuna wazanzibar wakristo au kama wapo wao hawatakiwi kusali? hata katika serikali ya aliyekuwa rais wa Irak Sadam Hussein alikuwepo waziri mkristo japo ni nchi ya kiislam, hata misri makanisa yapo japo ni nchi ya kiislam, natamani kauli ya jussa maana mawazo yangu yananiambia tatizo sio Muungano pekee bali na udini wa baadhi ya wenzetu wanzanzibar, nataka nisikie kama jussa atakemea kuchomwa kwa makanisa na kuunga mkono harakati za kuvunja muungano au atakemea yote mawili.*
  Kwa kumalizia niseme sio nyinyi peke yenu tu wanzazibar musioutaka muungano hata huku bara wapo baadhi ya wabara wasioutaka muungano ila wanaongozwa na busara, hekima na ubinadamu, hawavunji misikiti wala makanisa hawachomi gari la Padri wala Sheikh kwa ufupi wanathamini utu, kama ni kuuvunja Muungano watafuata taratibu mwishowe talaka itaandikwa lakini pia mkukmbuke maneno ya Mwalimu kwamba mtawafukuza wabara mwishowe mtahamia wapemba........fikirini kabla hamjaamua kutenda itawasaidia mbele ya safari.
   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Unataka kujua kauli ya Mh. Jussa Ladha, mbona ameshaitoa siku nyingi nitamu-quote. "Vurugu zilizotokea Zanzibar Jumamosi na Jumapili zimesababishwa na kuwepo Makanisa na Watanganyika wengi Zamzibar" mwisho wa kunukuu.
   
Loading...