Natamani kurudi kwa mpenzi wa zamani ila nilimuumiza sana

Kisa chako kimenikumbusha mbali sana, my first guy aliniacha vibaya nikiwa first year tena katikati ya UE hapo yeye yupo kazini kakutana na warembo wa maofisini.... Sitasahau nilizimia kwenye mtihani nakulazwa juu ila nilijitahidi nikamsahau, sasa kilichomkuta tangia hapo aliishia kuzalisha mahousegirl watatu tofauti, kazi alifukuzwa ana maisha magumu hadi huruma... Huu ni mwaka wa saba ananiomba turudiane lkn ata sura yake sitamani niione nilishamchukulia kama amekufa
 
Acha kudanganya wenzako hao ni wanawake wajinga wachache ulokutana nao.
Madam usijifariji, huu ndo ukweli ingawa ni mchungu. Mshkaji wako wa zamani uliyeachana naye akiamua kukutafta anakupata tu; simple like that.
 
Ulivyokuwa ukimtendea ameapa hatakusahau kamwe maana hata sisi majirani zake hatukuwa tunafurahia tabia zako na tumemshauri asikurudie abadani, ww umeona mambo yake yameanza kumnyookea ndio unataka kurudi huna lolote...tabia ni km maji sikuzote huwa hayasahau ubaridi. .!!!!
 
Wanajamii habari zenu?

Baada ya kukaa na mpenzi huyu ambaye sasa kila kukicha naonja joto la jiwe, sasa nimeanza kumkumbuka mpenzi wangu wa zamani ambaye alinijali kwa hali zote, alinikuta nikiwa sina lolote lakini alinipenda toka ndani ya moyo wake.

Nakumbuka kuna kipindi nilijisikia kumchukia tu bila sababu. Nikawa nasababisha ugomvi kila mara. Na mara zote ni yeye aliyeniomba msamaha ingawa ni mimi niliyesababisha kutoelewana.

Kuna siku nakumbuka nilikuwa kwenye matatizo ya kikazi, ni yeye aliyesimamia kila kitu kuanzia kula yangu mpaka madeni yangu. Baada ya kumaliza shida zangu na kurudi kazini, nilimpigia simu na kumwambia nilikuwa namtumia tu na wala simpendi. Muda huo sikujisikia vibaya. Ila leo najutia kwa kitendo hicho.

Natamani nirudi mikononi mwake na kutulia maisha yangu yote kutokana na upendo na kujali kupindukia.

Mungu anisamehe kwa kumuumiza sana.

Kama wengi walivyosema omba msamaha.
Ila kitu muhimu mpe pia muda maana wengine wanaomba msamaha na kutarajia jibu hapo hapo. Mtu anayekupenda yes inauma, na kwa vile kila mtu alisha move on, anahitaji muda wa ku reflect na maumivu yatarudi siku tu akisikia sauti yako au kuona sura yako. Then, hopefully graph itashuka taratibu na mungu akipenda utasamehewa after few days or weeks.

Maana na nyie, who knows km kweli unajutia au uchumi umebana sasa unakimbilia green pasture ? Wengi wenu ni utoto na ulimbukeni, kutokuangalia outside the box.

Usiombe msamaha leo then kesho unaomba hela ya luku au kodi ya pango !!. Pia kuwa tayari kwa majaribio, mm mfano naweza kurudia rudia kila mara machungu hayo, yaani ulichonifanyia ili kukupima km kweli unajutia moyoni- yaani utarudia nakuonekana unajuta au utafyatuka tena! Nakupa othr side ya coin ili ujiandae haswa...
 
Mda wote huo kashapata mwingine kweli naamini sasa malipo hapa hapa
 
Ina maana siku zote anakusubiri wewe tu, umuumize afu uhangaike huko weee den urudi kwake, yeye anakusubiri wewe tu.
Kwani watu wenye real love hawapo? Au yeye ni mbaya kiasi gani mpaka asipate mtu kwa muda wote.
Wewe ushachezea shilingi chooni, kama ni kwenda kuomba msamaha ukaombe tu ili msalimiane ila khs mapenzi wewe humfai. Wewe deal na watu kama huyo anaekuonjesha joto la jiwe ndio saizi yako.
Mtu unaonyeshwa mapenzi na kujaliwa basi unajiona una bahaaati kupindukia.
Sasa hapo umepata dawa unywe ili upone ugonjwa wako wa kujisikia.
 
Juzi Sky Eclat alileta thread usimwombee Adui Yako maradhi wala nini mwombee tu kupenda asipopendwa maana ni mateso yake ni jehanam ndogo nadhani alikuombea moto umemuona

Sikushauri umrudie maana ulimuacha kwa maneno magumu sana na sisi wadada kusahau ngumu ila muombe msamaha upate Amani

No kurudi nyuma mambo ni mbele kwa mbele Mkuu
 
Unaufahamu ugumu wa kuishi jana?! Muombe msamaha then mwache aende zake ww ubaki na memories nzuri zake ili iwe fundisho kwa utae mpata ila ukisema mrudiane possibility ya kuwa fake rlshp Ni kubwa ww utakua guilty feelings yeye atakua na mistrust in a long run it's not worth it
 
Wanajamii habari zenu?

Baada ya kukaa na mpenzi huyu ambaye sasa kila kukicha naonja joto la jiwe, sasa nimeanza kumkumbuka mpenzi wangu wa zamani ambaye alinijali kwa hali zote, alinikuta nikiwa sina lolote lakini alinipenda toka ndani ya moyo wake.

Nakumbuka kuna kipindi nilijisikia kumchukia tu bila sababu. Nikawa nasababisha ugomvi kila mara. Na mara zote ni yeye aliyeniomba msamaha ingawa ni mimi niliyesababisha kutoelewana.

Kuna siku nakumbuka nilikuwa kwenye matatizo ya kikazi, ni yeye aliyesimamia kila kitu kuanzia kula yangu mpaka madeni yangu. Baada ya kumaliza shida zangu na kurudi kazini, nilimpigia simu na kumwambia nilikuwa namtumia tu na wala simpendi. Muda huo sikujisikia vibaya. Ila leo najutia kwa kitendo hicho.

Natamani nirudi mikononi mwake na kutulia maisha yangu yote kutokana na upendo na kujali kupindukia.

Mungu anisamehe kwa kumuumiza sana.
Omba msamaha ila uliumiza xn moyo wake na cjui kwa nn uliamua kumwmbia hadharan ivo! Labda ulikuw under 20
 
Waliotangulia wamesha kushauri vizuri ila my point is kama una uhakika umebadilika kweli na si yule wa zamani then uendelee na mpando wako wa kurudi kwake ila kama bado unahisi hujayafanyia kazi matatizo yako its better usirudi kwake
 
Wanajamii habari zenu?

Baada ya kukaa na mpenzi huyu ambaye sasa kila kukicha naonja joto la jiwe, sasa nimeanza kumkumbuka mpenzi wangu wa zamani ambaye alinijali kwa hali zote, alinikuta nikiwa sina lolote lakini alinipenda toka ndani ya moyo wake.

Nakumbuka kuna kipindi nilijisikia kumchukia tu bila sababu. Nikawa nasababisha ugomvi kila mara. Na mara zote ni yeye aliyeniomba msamaha ingawa ni mimi niliyesababisha kutoelewana.

Kuna siku nakumbuka nilikuwa kwenye matatizo ya kikazi, ni yeye aliyesimamia kila kitu kuanzia kula yangu mpaka madeni yangu. Baada ya kumaliza shida zangu na kurudi kazini, nilimpigia simu na kumwambia nilikuwa namtumia tu na wala simpendi. Muda huo sikujisikia vibaya. Ila leo najutia kwa kitendo hicho.

Natamani nirudi mikononi mwake na kutulia maisha yangu yote kutokana na upendo na kujali kupindukia.

Mungu anisamehe kwa kumuumiza sana.
pumbavu
 
Omba msamaha ili uwe huru nasiyo kurudiana nae .....Mungu ni wawote ameshampa anayemfaa
 
Back
Top Bottom