Natamani kupamba jarida la FORBES tatizo nitoke vipi?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
17,828
31,818
Kila nikiingia kitandani hunichukua muda mrefu kupata usingizi kutokana na mawazo yaliyojazana kichwani mwangu...
Hili limezidi hili na lile limezidi hili.....
Sitaki chochote zaidi ya utajiri
Yaani iwe iwavyo nitakacho toka nacho ,lazima mwishowe kiniingizie mapesa tena sio mfukoni bali benki...
Naamini pesa ya kweli haihesabiwi nyumbani bali kwenye vitabu vya benki...
Sasa hiki ndicho kitamani na ndicho kinachoninyima usingizi...
Kila nikiufikiria msemo unaosema "tengeneza pesa za kutosha mapema iwezekanavyo ili uweze kufanya mambo mengine katika maisha"....ndio huwa nachoka kabisa....
Siyo siri roho huwa inaniuma ssna nikisikia hadithi za mafanikio ya vijana wadogo...najiuliza hivi nibeba. Zege hadi lini...??
Kuna wakati napata wazo la kugundua kitu kitakacho niingizia
pesa Ndefu na kuwa mfano kwa wengine...
Au niwe mganga wa kienyeji itanilipa..?? Au niwe mchungaji..???....nikicheki wingi wa makanisa najikuta nachoka kabisa.....
Nikifikiria kufanya uvumbuzi kwenye teknolojia naona kama najidanganya tu...maana hakuna jipya lililobaki...
Kuigiza siwezi ,kuimba ndio kabisaaaaa....sasa nitatokaje mimi...yaani ndio sina kabisa kipaji....???
Nikijitazama kwenye kioo najiona kabisa naweza kuwa
bilionare...
Sasa wanajamii nitoke vipi...???
Nataka kutokea kwenye jarida la FORBES...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ukweli ni kwamba hao wanaopamba hayo magazeti utajiri wao sio wa halali.Ni ukwepaji kodi,Magendo,rushwa na uharamia ndio vyanzo vya utajiri.Hauna tajiri tanzania ambaye labda alianza kuuga kuku,Akawa na soko kubwa,akaanza kuzalisha chakula cha kuku wake,labda aanzisha kiwanda cha kusindika kuku au kutengeneza madawa ya kuku n.k. na kupitia miradi hiyo akapata mafanikio wabia wakajitokeza.hakuna wenye historia hiyo.
 
Kwa hiyo mkuu unanishauri vipi....???
 
huwezi kufikiri vile vile then ukawa tofauti.
CHANGE THE WAY YOU THINK.
THINK BIG.
 
Duuh. Pole sana. Piga usingizi bana maisha mafupi. Ongeza maujanja kwenye kazi unayoifanya pata hela ya kula na investment kidogo and live life
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom