Natamani kuona Polisi wakienda kulinda amani mataifa ya nje (Peacekeeping)

Foxhound

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
28,038
74,438
Salaam;
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya tisa, ibara ya 147, kifungu kidogo cha (4).

Tanzania ina majeshi manne ambayo ni:
1. Jeshi la Ulinzi
2. Jeshi la Polisi
3. Jeshi la Magereza
4. Jeshi la kujenga taifa.

Sasa kwanini kwenye Peacekeeping waende Jeshi la Ulinzi pekee yao wakati tuna majeshi mengi hapa nchini? Natamani walau siku moja nije nione au kusikia Kuna kikosi cha jeshi la polisi kimekwenda Congo au Sudan kwa ajili ya Peacekeeping au kusikia kuna Contigent ya jeshi la polisi ipo Sudan.

Kwa maana polisi nao ni jeshi la polisi na inatambulika duniani kote kuwa Tanzania kuna jeshi la polisi. Au nyie mnaonaje? Kwenu wadau.
Cc popoma03
Saguda47
 
Polisi wanaenda nje ila sio wengi kutoka na usaili wao unadili sana na professional. tofauti na Jwtz ambao wanaenda tu .
Wao wanakwenda kule sana sana hawazidi wanne na sio kama wanachokwenda kukifanya profession yake jeshini haipo bali ni kwa maelekezo ya UN. Namaanisha waende wao kama wao battalion yao nzima, isiwahusishe jw, kwani nao si jeshi la polisi?
 
Ni mgawanyo wa majukumu wao hudili sana na ulinzi wa ndani,sio kanakwamba watashindwa kufanya kazi wanazofanya jwtz ,ni simple kuliko unavyofikiria wewe.

UN huwahitaji kwa ajili ya professional zao na usaili wao ni mgumu sana,
Jwtz mpaka la saba huenda na form asiyekua na professional yoyote wanaenda.
Profession ipi kwa mfano wanayoifanya ambayo kwenye jw haipo? Ni kwa maagizo ya UN.
Ukiweza kunitajia hata moja tu ambayo haipo kwenye jw nitakusadiki
 
Jeshi ni moja tu,Jeshi la ulinz la wananchi wa Tanzania zingine zote ni Idara tu,Popote Dunian Nchi huwa inakuwa na Jeshi moja tu,hakuna kitu kinachoitwa eti Jeshi la polis sjui jeshi la magereza hizo ni mbwembwe tu,ila kuna Idara ya Polis ,Idara ya Magereza
Kwa mujibu wa katiba, maana katiba ndio msingi mama wa miongozo yote, unasemaje juu ya hilo?
 
Natamani walau siku moja nije nione au kusikia Kuna kikosi cha jeshi la polisi kimekwenda Congo au Sudan kwa ajili ya Peacekeeping au kusikia kuna Contigent ya jeshi la polisi ipo Sudan. Kwa maana polisi nao ni jeshi la polisi na inatambulika duniani kote kuwa Tanzania kuna jeshi la polisi. Au nyie mnaonaje? Kwenu wadau.
Cc popoma03
Saguda47
Polisi wetu wanaenda sana. Wako huko Dafur muda mrefu tu.
 
Sitaki kuamini kama somo la uraia limefutwa mashuleni, hii ni hatari sana

Mleta thread hujui majukumu ya hizo idara?

Naungana na Rais mstaafu Bw Benjamen Mkapa kwenye kuanzishwa mjadala wa kitaifa kuhusiana na hatima ya elimu ya Tanzania
 
Sitaki kuamini kama somo la uraia limefutwa mashuleni, hii ni hatari sana

Mleta thread hujui majukumu ya hizo idara?

Naungana na Rais mstaafu Bw Benjamen Mkapa kwenye kuanzishwa mjadala wa kitaifa kuhusiana na hatima ya elimu ya Tanzania
Nao ni jeshi, sio idara. Ni kwa mujibu wa katiba, najua majukumu yao ipasavyo lakini neno jeshi linawahadaa na kuona kuwa wao ni jeshi, hii yote imetokana na kiswahili kukosa misamiati yake inayojitegemea, kokote duniani polisi wanaitwa polisi, ni Tanzania pekee jeshi la polisi, sasa je vp kuhusuna wao kuandaliwa battalion yao ya peace keeping?
 
Mimi ninavyojua wako wengi tu. Huko Dafur kama wamebaki wanne inashangaza lakini najua walikuwa wengi.
Je wao kama wao wapo kikosi kizima? Wanachukuliwa wachache kwa maelekezo maalum ya UN, nilichosema mimi ni kuwa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania Polisi ni jeshi la polisi, je vp na wao kuhusu kunzishiwa utaratibu wa kwenda peace keeping, kuwa na battlion yao.
 
Jeshi ni moja tu,Jeshi la ulinz la wananchi wa Tanzania zingine zote ni Idara tu,Popote Dunian Nchi huwa inakuwa na Jeshi moja tu,hakuna kitu kinachoitwa eti Jeshi la polis sjui jeshi la magereza hizo ni mbwembwe tu,ila kuna Idara ya Polis ,Idara ya Magereza
usilo lijua aisee ni usku wa giza nimechekaaaa sana kwann hata msitulize sisi ambao tupo huku. ...nmechekaa apo eti Polisi ni idala hehehehe kwanza umetumia criteria gani kutafsiri maana ya jeshi. ..**** majeshi ya ulinzi na majeshi ya usalama Polisi ni jeshi la usalama mafunzo yao yote wanayopita nibyakijeshi na ndomaan majeshi yote yanadahili kutoka JKT...sasa hapo kulingana na udahili utaenda jifunza proffesional yako kijeshi kulingana na jeshi ulilolopo nandomaaan wote wakitoka JKT wanaenda depo 6 months uwe jeshi la polisi au ulinzi. ......afu kulinda amani jeshi la Polisi pia huwa wanakuepo na wanafanya kazi kule pia
 
Back
Top Bottom