Wakati ninaishi ughaibuni miaka kadhaa iliypiota, jirani yangu kutoka Kenya alinisimulia hali iliyokuwepo kisiasa nchini Kenya baada ya utawala wa Rais Moi na serikali yake kupitia chama cha KANU. Alinieleza hasira zilizokuwa kwenye mioyo ya wananchi kutokana na ufisadi wa viongozi wa serikali na chama cha KANU kwamba wananchi walikuwa tayari kuchinja hata kuku mtaani aliyekuwa na jina au harufu ya uhusiano na jina la KANU. Wakati huo, niliona hilo haliwezekani kwa chama cha TANU/CCM ya Tanzania. Kwa sasa hivi nina maoni tofauti. Nikifuatilia maoni ya watu kwenye mitandao ya kijamii kufuatia clips za video za viongozi wastaafu na ndugu/jamaa zao naona ni muda muafaka chama hiki, the Grand Old Party ya Mwl. Nyerere ipasuke vipande kutoa nafasi mawazo mapya ndani ya chama chenyewe, upinzani na taifa kwa ujumla, kama ilivyopasuka KANU ya Mzee Jomo Kenyatta na Arap Moi. Natamani ipatikane CCM mpya kwa jina jipya inayoendeleza mawazo ya Mwl. Nyerere ikiongozwa na Mh. J. M. Magufuli na wafuasi vijana kama akina Bashe, Msukuma, Molel, Bashiru na wengine wote wenye mwelekeo wa progressive agenda. Natamani akina Kinana/Makamba and Sons & Friends waendelee na lichama lao la Grand Old Party then tuone uungwaji mkono wa wananchi kama wanavyo amini akina Membe. Nafahamu Tanzania siyo Kenya, na kwa maana hiyo CCM mpya ya Magufuli (au jina lolote lile) si lazima iwe na mwelekeo wa KANU iliyozaa Jubilee ya Uhuru Kenyatta. Sasa ninaamini pasipo shaka maneno ya Mwl. Nyerere kuliko wakati mwingine wowote ule kwamba upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM.
Note: Kama nimekukwaza kwa mtazamo wangu una uhuru wa kutoa povu bila matusi.
Note: Kama nimekukwaza kwa mtazamo wangu una uhuru wa kutoa povu bila matusi.