Natamani kukutana na Dr. Slaa baada ya uteuzi wa baraza la Magufuli

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Dr Slaa alisema kumkaribisha Lowassa Ukawa ni sawa na kuchukua "kinyesi" ukapeleka chumbani! Bila shaka pamoja na hasira za kukosa urais alitaka kuwaaminisha watanzania jinsi gani anauchukia ufisadi. Lakini akasema ukiwapima Lowassa na Magufuli kwa kuwaangalia usoni utagundua Magufuli ndiye mwenye nia ya dhati ya kupinga ufisadi.

Leo baada ya Magufuli kuwarudisha watu wenye tuhuma za ufisadi sijui atatwambia ni sawa na kuchukua kitu gani kukipeleka chumbani.Katibu wangu mkuu wa zamani amekuwa akiongelea mambo yanayoendelea nchini basi na yeye aongee kitu basi. Lipumba tumemsikia, tunakusubiri wewe baba
 
Mwakyembe na muhongo wametia doa la kwanza la mh.jpm lazima hapa kuna kundi kubwa la watanzania imani imeanza kupungua kwake.
Sijui anatafisiri vipi uhusika wao ktk kashifa ya escrow na mabehewa mabovu.
 
Ndiyo maana tunataka kujua maoni ya yule mtetezi wao
 
Hata Magufuli si mlisema fisadi. subiri muone utendaji. Kwa Lowasa si mlisema amesingiziwa assume na hao pia walisingiziwa ufisadi.
 
Ebu tukumbusheni kale kanyimbo chenu..
mtasubiri sanaaaa na badoo
wapinzani watasubiri sanaaaa na badoo

sasa ndo mda wenu wa kusubiri sana...
 
Mlipomchagua lowasa baada ya kutuaminisha miaka saba ni fisadi mlituhoji kama fisadi mbona hajafikishwa mahakamani..na sisi tunahoji kama hao wana tuhuma za ufisadi mbona hawajafikishwa mahakamani..??na ccm pia wamebadili gia angani..
 
Ebu tukumbusheni kale kanyimbo chenu..
mtasubiri sanaaaa na badoo
wapinzani watasubiri sanaaaa na badoo

sasa ndo mda wenu wa kusubiri sana...

Tutasubiri nini? Wizara zenyewe kuzitaja mpaka upige push up kama aliyeziunda! Kazi, vijana, michezo, habari sijui na nini?
 
Mlipomchagua lowasa baada ya kutuaminisha miaka saba ni fisadi mlituhoji kama fisadi mbona hajafikishwa mahakamani..na sisi tunahoji kama hao wana tuhuma za ufisadi mbona hawajafikishwa mahakamani..??na ccm pia wamebadili gia angani..

Samahani wewe ni Dr Slaa, samahani lakini
 
say no to muhongo Hana nia nzuri Na wazawa Na rasilimali zao yuko tofauti Na wao anaamini ugeninishaji ni mzuri kwa Mgeni si kwa mtanzania .mi mi ningemuelewa endapo angezalisha Tajiri mmoja kwenye sekta hii ya mafuta Na Gesi
 
Mpaka Hugo Chaves umetokea? Kuvurunda kwa Magufuli kumewafukua wengi
 
Dr Slaa alisema kumkaribisha Lowassa Ukawa ni sawa na kuchukua "kinyesi" ukapeleka chumbani! Bila shaka pamoja na hasira za kukosa urais alitaka kuwaaminisha watanzania jinsi gani anauchukia ufisadi. Lakini akasema ukiwapima Lowassa na Magufuli kwa kuwaangalia usoni utagundua Magufuli ndiye mwenye nia ya dhati ya kupinga ufisadi.

Leo baada ya Magufuli kuwarudisha watu wenye tuhuma za ufisadi sijui atatwambia ni sawa na kuchukua kitu gani kukipeleka chumbani.Katibu wangu mkuu wa zamani amekuwa akiongelea mambo yanayoendelea nchini basi na yeye aongee kitu basi. Lipumba tumemsikia, tunakusubiri wewe baba
Kina nani wenye tuhuma za ufisadi?
Usichanganye vitu, kuwa na tuhuma na kuwa suspected na wapvmbavu ukawa!
 
Mlipomchagua lowasa baada ya kutuaminisha miaka saba ni fisadi mlituhoji kama fisadi mbona hajafikishwa mahakamani..na sisi tunahoji kama hao wana tuhuma za ufisadi mbona hawajafikishwa mahakamani..??na ccm pia wamebadili gia angani..

Kwa hiyo draw game?
 
Hivi mlifikiri magufuli angetoa mawaziri wapi kama si chungu kilekile kibovu.....tusubili utendaji wao labda hawataiba tena!
 
Back
Top Bottom