Natamani kufanya kazi usiku na kupumzika mchana

Tanganyika1

JF-Expert Member
May 10, 2011
422
86
Jamani wana jf nawapenda sana na natambua uwepo wenu katika harakati za mapambano dhidi ya matatizo tulionayo watanzania.
Binafsi napenda kutoa rai kuwa ajira imekua tatizo kubwa hapa tanzania hasa kwa vijana baada ya matatizo ya malaria, vifo vya watoto na wa mama wajawazito, bila kusahau ajali za barabarani.
Katika kutafakari kwa muda nimegundua kuwa tunaweza kujikwamua kwa kugawana muda wa kufanya kazi. Ni kawaida kwa watu kwenda kazini kila asubuhi na kurejea majumbani mwao jioni kwa mapumziko....sasa nadhani ingekua ni jambo jema na la busara kama baadhi ya watu ambao hawana kazi lakini sifa za kufanya kazi wanazo basi serikali na mashirika binafsi yange ongeza muda wa kufanya kazi na hivyo basi kuruhusu watu wafanye kazi usiku na kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wetu............ni mtazamo tu waungwana.
 
Mkuu..... KK Security, Night Support, etc. wanatangaza kazi karibu kila mwezi..... kama vipi jaribu kucheki nao, wana kazi nyingi sana za usiku. hata vigezo vyao ni rahisi tu. Hawahitaji kukufanyia interview mbilimbili kama wafanyavyo wengine, NSSF and the like.
 
Jamani wana jf nawapenda sana na natambua uwepo wenu katika harakati za mapambano dhidi ya matatizo tulionayo watanzania.
Binafsi napenda kutoa rai kuwa ajira imekua tatizo kubwa hapa tanzania hasa kwa vijana baada ya matatizo ya malaria, vifo vya watoto na wa mama wajawazito, bila kusahau ajali za barabarani.
Katika kutafakari kwa muda nimegundua kuwa tunaweza kujikwamua kwa kugawana muda wa kufanya kazi. Ni kawaida kwa watu kwenda kazini kila asubuhi na kurejea majumbani mwao jioni kwa mapumziko....sasa nadhani ingekua ni jambo jema na la busara kama baadhi ya watu ambao hawana kazi lakini sifa za kufanya kazi wanazo basi serikali na mashirika binafsi yange ongeza muda wa kufanya kazi na hivyo basi kuruhusu watu wafanye kazi usiku na kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wetu............ni mtazamo tu waungwana.

Ni sawa lakini inahitaji mkakati,kwa mfano walimu wanawezaje kufundisha usiku shule za kata n.k.But the whole idea is good
 
Kuna institutions nyingi ambazo zinafanya kazi masaa 24, mfano migodi, mahosipital etc, hoja yako ni implementable lakini ninavyojua wabongo mhhhh watakua wanaenda na bia kazin na pia watachapa usingizi kikamilifui!!!!!!!!
 
good idea..problem is hela za kuwalipa hao new staff

Nafikiri pesa za kuwalipa sio tatizo maana mtu anpofanya kazi ni kwamba anazalisha, na hivyo naamini endapo wazo hili litachukuliwa itasaidia kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi na sio kuongeza mzigo kwa waajiri.
 
Mmh natamani ningejua unapataje kazi bandari...mana nimejaribu mara kadhaa bila mafanikio.
 
umesoma Port Management(ngazi ya diploma) au Port Operations(ngazi ya certificate) kutoka Chuo cha Bandari?
hao ndio wanaohitajika TPA, na nilisikia watatangaza nafasi za ukarani this year, nashangaa mpaka leo wapo kimya. Ila washaanza ku-operate masaa 24.
 
ole wenu muufanyao usiku kuwa mchana maana ufalme wa mungu si wenu!!!

Mmmh yeah kwa upande wa imani inakua shida kama huto elewa mandiko..........sijui ila sina hakika kama Mungu kuna sehemu amekataza kufanya kazi usiku...naamini itakua kuna maana ya ndani Zaidi na tofauti na wale ambao hufanya kazi zao za halali wakati wa usiku.....
 
Back
Top Bottom