Natamani 'Jamii' ingeijua sababu iliyosababisha nikafanya vile, Japo hadi leo nashindwa kuelewa kama nilikuwa sahihi au lah!

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
My True story.

Kisa hiki kinaanzia miaka kadhaa nyuma wakati nikiwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho kimasomo katika shule moja ya sekondari nchini.

Nilikuwa nafanya juhudi kubwa sana katika masomo na asilimia kubwa marafiki zangu shuleni walikuwa ni wale wanafunzi ambao 'wanajitambua' na wanafanya juhudi kimasomo.

Hivyo sikuwa maarufu kwa kitu kingine tofauti na taaluma pale shuleni mfano skendo za mapenzi shuleni nk. Nilikuwa mmoja wa mifano bora kitaaluma enzi hizo.

Nyuma ya pazia sio kwamba sikuwa na mahusiano, hapana, nilikuwa nayo na nilikuwa katika uhusiano serious na binti mmoja ambae hakuwa mwanafunzi katika ile shule. Alikuwa anasoma mkoa mwingine na tulipendana sana sana.

Katika shule niliyokuwa nasoma nilikuwa Day scholar na wanafunzi wengine walikuwa wanaishi boarding. Kwa wale mliosoma boarding naamini mtakuwa mnafahamu umaarufu wa couples mbalimbali za wanafunzi wa bweni.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa na moja ya couple maarufu pale bwenini ilikuwa ni couple ya huyu Jasmin (sio jina lake halisi) ambae ndie mhusika wa huu uzi.

Kwa mara ya kwanza nakutana na Jasmin ilikuwa ni katika Tuition center kipindi cha likizo ya December kama huu. Tulikuwa tunasoma shule moja na darasa moja (tofauti ni combinations) lakini hatukuwahi kufahamiana japo kwa sura.

Jasmin hakuwahi kumuona Fohadi pale shule na mimi Fohadi sikuwahi kumuona Jasmin. Shule ina wanafunzi wengi ( O & A levels) na ukizingatia sikuwa mtu wa matukio na maarufu kwa mambo mengine isingekuwa rahisi kujulikana kwa wanafunzi wengine tofauti na combination yangu.

Nilimkuta Jasmin amekaa na rafiki yangu ambae nasoma nae combination moja, kama ilivyo kawaida, niliwasalimia na kuendelea na ratiba zingine za kusubiri muda wa somo langu ufike.

Muda wa kipindi ulipofika nilishangaa kumuona rafiki yangu akiingia darasani peke yake na Jasmin akibaki nje. Kwajinsi nilivyowakuta asubuhi ilionekana ni kama watu wanaofahamiana sana mda mrefu lakini nikawa najiuliza imekwaje huyu rafiki yangu kumfahamu Jasmin, wakati rafiki yangu anatoka mkoa mwingine na alikuja katika huu mji kwajili ya shule na anakaa boarding.

Asilimia 99.9 ya maisha yake hapa mjini ilikuwa ni katika kuta za shule na alikuwa mwanafunzi wa bweni. Nilijiuliza swali hili kwani nilipowasalimia asubuhi huyu rafiki yangu alinitambulisha kuwa Jasmin ni mwanafunzi wa Jangwani girls.

Kumbe kitu pekee ambacho sikujua ni kuwa rafiki yangu alinificha mda huo, Jasmin alikuwa ni school mate wetu na alikuwa mwanafunzi wa bweni ndio maana walikuwa wanafahamiana sana.

Huu ukweli nilikuja kuugundua wiki kadhaa mbele ila hadi naondoka tuition mda ule nilimuaga rafiki yangu na nikamuaga Jasmin nikijua kabisa ni mwanafunzi wa Jangwani sec. Bahati mbaya, sikuweza krudi tena tuition kwa muda kama wa wiki 2 maana nilipata msiba.

Shangazi yangu alifariki na ikabidi nikatishe tuition. R.I.P. Hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza kuonana na Jasmin na sikumuona tena hadi shule ilipofungua.

Sikujua kiliendelea nini kati ya rafiki yangu na Jasmin kuhusu mimi ila nakumbuka siku ya kwanza tu niliyofika shule baada ya likizo, huyu rafiki yangu alinishika mkono akanambia nimsindikize sehemu.

Sikubisha, tuliondoka na moja kwa moja kituo kilikuwa katika mlango wa darasa moja la combination tofauti. Nilivyoingia tu nikakutana uso kwa uso na Jasmin na kwa kumuangalia tu nikagundua ni mwanafunzi wa hostel maana pale shuleni kwetu kulikuwa na alama katika uniform iliyomtenganisha mwanafunzi wa day na bweni.

Ni siku hii ndipo nilipofahamu kuwa Jasmin hakuwa mwanafunzi wa Jangwan na nikagundua kwanini alikuwa amezoeana sana na rafiki yangu kule tuition center.

Nilimsalimia Jasmin, tukacheka na nikamtania kwanini siku ile alikubali mimi nidanganywe kuwa anasoma Jangwan wakati alikuwa na uwezo wa kukataa. Ilikuwa ni siku nzuri sana na tuliagana kwa Jasmin kuniakaribisha tena darasani kwao namimi nikamkaribisha darasani kwetu.

Nilirudi darasani, na mambo mengine ya shule yaliendelea kama kawaida. Utambulisho private kwa Jasmin wala sikutaka kuutumia kam fursa za kibaharia.

Nilimchukulia kama rafiki mpya na wala sikuwa na mawazo yoyote juu yake. Maisha yaliendelea wiki ya kwanza na ya pili ikakatika shule ikapamba moto na ndoto za kujiunga na chuo kimoja kikubwa hapa nchini kwa ufaulu mkubwa nikawa nazipambania.

Kipindi nakutana na Jasmin kule tuition, sikujua kama alikuwa ni mmoja wa mabinti wenye couple maarufu pale hostel. Kutokana na mambo ya mahusiano, bwana ake Jasmin ambae alikuwa anasoma combination tofauti na Jasmin alikuwa ni wale vijana wenye 'makoloni' mengi mle hostel.

Alikuwa na mahusiano na mabinti wawili, mmoja ni Jasmin na binti mwingine pia. Hii hali ilimtesa sana Jasmin na aiku zote alikuwa ni mtu wa kulia na kuteswa na mapenzi.

Kwa haiba, Jasmin ni binti mpole na mstaarabu kwahiyo hakuwa na uwezo wa kupambania penzi lake kwa yule jamaa na wala asingeweza kushindana na yule binti mwingine.

Njia kuu kwake ilikuwa ni kulia na kumuomba mpenzi wake atulie lakini wapi. Mapenzi yalimvuruga, alikuwa ni binti wa kuugua na kuomba getpass kila mara ili aende kwao Kinondoni kutibiwa (sio eneo halisi).

Mpaka nakutana nae wakati wa likizo, bado alikuwa na migogoro ya kimapenzi. Hii hali iliendelea mpaka tunafungua shule.

Hiki kitu sikukijua kumbe baada ya kufungua shule tayari Jasmin alikuwa ameamua ku move on na moyo wake ulikuwa umemchagua Fohadi awe kama tulizo jipya na furaha yake katika mahusiano.

Kumbe ule utambulisho nilioenda kufanyiwa kule darasani kwa akina Jasmin ulipangwa makusudi lakini mimi Fohadi sikujua kitu chochote.

Jasmin alikuwa ameamua kuivunja couple yake maarufu ya hostel na tayari bila mimi kujua kumbe taarifa zangu zote Jasmin alikuwa anazipata kupitia yule rafiki yangu wa darasana na akafikia hitimisho la kunichagua mimi ili awe na furaha na pia ili alipe kisasi kwa mtesi wake kwa kutoka na mwanafunzi wa pale shule ila tofauti tu ni kuwa Jasmin na mtesi wake walikua hostel na mimi fohadi nilikuwa day scholar..........

Mpaka leo sijui kama nilikuwa sahihi ama la kufanya yote yaliyotokea..Mpaka leo natamani Jamii iitambue historia hii ili kila kitu kirudi kuwa sawa na kunielewa.... ITAENDELEA....​
 
Samahani mkuu mashahidi wa yehova wanasemaje juu ya hii story yako....?
 
Kwa wale wanaotaka summary aisee siwezi kuwasaidia..wale wanaozani hii ni hadithi kama zingine yenye parts nyingi wako wrong..hii sio hadithi bali hii ni scenerio ya ukweli ya mapenzi iliyowahi kunitesa na bado kuna mda inanipa changamoto..story haina parts nyingi na wala haina summary..najaribu kuiweka kwenye mpangilio wa uwazi na unaoeleweka ili mwenye kujifunza ajifunze kupitia 'makosa' yangu
 
Kwa wale wanaotaka summary aisee siwezi kuwasaidia..wale wanaozani hii ni hadithi kama zingine yenye parts nyingi wako wrong..hii sio hadithi bali hii ni scenerio ya ukweli ya mapenzi iliyowahi kunitesa na bado kuna mda inanipa changamoto..story haina parts nyingi na wala haina summary..najaribu kuiweka kwenye mpangilio wa uwazi na unaoeleweka ili mwenye kujifunza ajifunze kupitia 'makosa' yangu
sasa ulitesek vipi kaka maana kwa namna ulivosimulia ni kwa namna gani ulikuja kuingia kwenye mahusiano na huyo dada na ishu ni kuwa dada alionekana kuumizwa sana na mapenzi alikokuwa sasa ww uliumizwa vipi??just try to link paragraph to paragraph
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom